Monday, February 02, 2009

Safarini Anguilla

Wadau, niko safarini Blowing Point, Anguilla. Ni kisiwa katika bahari ya Caribbean.

Niliondoka Boston asubuhi sana. Nilipanda ndege hadi kisiwa cha St. Maarten. Kutoka huko nilipanda ferry kuja Anguilla. Customs yao uwanja wa ndege ni kama Bongo ulivyokuwa enzi za Mwalimu. Bahati nzuri hawakunisumbua sana.

Nina picha kibao, lakini sina access nzuri ya internet. Nitazibandika nikirudi Boston wiki ijayo.

Kuna wazungu wengi wenyeji wa visiwa hizi. Wamepikwa na jua. Wengine wana rangi ya brown, na wengine wekunduuu! Yaani baada ya kuzoea kuona wazungu weupe kama karatasi huko Boston lazima niseme niliwatazama hawa wa hapa mara mbili kuhakikisha kuwa ni wazungu.

14 comments:

  1. NAKUTAKIA VEKESHENI NJEMA. TUNASUBIRI HIZO PICHA.

    ReplyDelete
  2. wekundu kama damu au wanaelekea kwenye uwekundu

    ReplyDelete
  3. Nakutakia mapumziko mema, Da Chemi, tuko pamoja.
    Apfle.

    ReplyDelete
  4. Una maana gani enzi za Mwalimu.Sifa na hadhi ya Tanzania ilikuwa juu sana enzi hizo unazozibeza.Tulikuwa nuru kwa yote mazuri Africa.Kulikuwa hakuna ukabila,rushwa.Watu walisoma bure ikiwa pamoja na wewe.Usihadaike na wingi wa golgate.Utu wa mtanzania umepungua sana tokea enzi hizo.Ukiwa na shilingi mia ya mmasai na simba ilikuwa inatosha kununua vitu vingi tu.Tulikuwa na viwanda na vyote vimeuzwa au kufa.

    ReplyDelete
  5. enjoy your stay dada,tumekumiss siku hizi mbili mtandaoni.
    likizo njema
    mdau
    thessaloniki,ugiriki

    ReplyDelete
  6. vekesheni njema dada yetu, enjoy the sun.

    ReplyDelete
  7. Da Chemi tumekuelewa vizuri sana. Enzi za Mwalimu ukitoka ng'ambo kupitia Airpost Dar unatetemeka kwa jinsi watu wa customs wanavyokusumbua! Una nini? Kama una sharti jipya au kitu kipya utakoma, unatozwa kodi kubwa!Wanataka kukunyanganya vitu vyako. Walikuwa wezi kweli pale DIA. Sanduku unaweza usipate au una nusu! Watu wamesahau! Tumekuelewa!

    ReplyDelete
  8. Tunasubiri zawadi, ahadi ni deni. Safari njema na ya salama!

    ReplyDelete
  9. Dada Chemi huko ni wapi kusiko na mtandao? maana tunakumiss.

    Anyway safari Njema.

    ReplyDelete
  10. Bongo Pixs, mtandao upo, lakini sikuja na lap top. Pia nina shughuli nyingi za kufanya katika muda mfupi. Blog itarudi full speed jumatatu ijayo.

    ReplyDelete
  11. siku moja fanya safari kama hiyo kwenu MANDA- LUDEWA-IRINGA TANZANIA kuna mandhali nzuri ya ziwa nyasa au umeisahau?dagaa ,mbasa mbelele bado kwa wingi bila kusahau "mpunga"ulimwao kandokando ya mto nchuchuma

    ReplyDelete
  12. Anony wa 6:28pm, kwetu sijapasahau. Ugali wa muhogo na dagaa wa ziwa Nyasa...weeee! Nilifungasha kifurushi cha unga wa muhogo na dagaa na kuleta Boston nlivyokuwa huko mwaka jana.

    ReplyDelete