Friday, February 06, 2009

Salamu kutoka Anguilla

Salamu nyingi sana kutoka Anguilla. Hapa pichani niko sehemu inaitwa Sandy Ground Overlook, Anguilla.

Uchumi wa Anguilla unategemea utalii tena utalii wa hali ya juu, yaani High Class. Nilipita uwanja wa ndege wao jana na nikaona private jets tano zimeegeshwa. Matajiri na mastaa wengi wanakuja hapa maana hakuna usumbufu kama Jamaica, Bahamas, Barbados nk.

Ila ukienda dukani kila kitu ni imported, utadhani uko supermarkt USA. Niliona kagenge walikuwa wanauza ndizi, viazi na vitunguu tu. Ardhi hapa haina rutuba imejaa mawe na mchanga, lakini wana beach nzuri sana, mchanga laini, halafu mweupe!

Sehemu nyingi ziliharibiwa na kimbunga kilichopita.

7 comments:

  1. Umependeza sana!

    ReplyDelete
  2. Da Chemi najua huna hamu ya kurudi kwenye ubaridi wa Boston! Vacation njema!

    ReplyDelete
  3. Enjoy yourself Da Chemi. Kwani maisha ni kufurahi dada.

    ReplyDelete
  4. Da Chemi, umeolewa?
    (kwa nia njema tu)

    ReplyDelete
  5. Ndio maana baridi imezidi, rudi tugawane baridi letu:-) Vekesheni njema. Umependeza.....

    ReplyDelete
  6. ACHENI TAMAA ZA KIZINZI. KUONA HIYO PASPORT SIZE PIC TU UDENDA UNAWATOKA. HUYO NI MKE WA MTU ACHENI USHAMBA. TAMAA KAMA FISI!!!!

    ReplyDelete
  7. Da Chemi,

    Yaani si utani umenona kwa muda mfupi inaonekana hali ya hewa ya Anguilla imekupenda sana. Haya kila la kheri tuko pamoja.

    Apfle.

    ReplyDelete