Showing posts with label Ashecliffe. Show all posts
Showing posts with label Ashecliffe. Show all posts

Sunday, January 27, 2008

Maelfu wajitokeza kwenye Casting Call Boston


Maelfu na maelfu ya watu wanaotaka kuwa Extras katika sinema mpya ya Martin Scorsese, Ashecliffe, walijitokeza jana Boston University. Watu walianza kupanga foleni tangu saa 12 asubuhi!

Mimi nilifika saa 8:30 (2:30Pm). Walikuwa wanaingiza watu kama 300 kwa mpigo kwenye ukumbini. Tulipewa lecture kuhusu kazi ya Extra. Siku inaweza kuwa ndefu masaa 12 hadi 16, fanya kama mnavoambiwa. Fika saa uliyopangiwa etc. Walitaja na bei ya malipo, dola $100 (Masaa manane) kwa siku plus overtime, kwa wasio union. Watapiga sinema maeneo ya Boston, Medfield na Taunton, Massachusetts kuanzia Machi 6 hadi mwisho wa Juni.

Baada ya hapo, watu walipanga foleni nyingine na kutoa fomu na kipigwa picha. Weusi walikuwa wachache sana kulinganishwa na idadi ya wazungu. Najua wengi wa weusi waliotokea watapata nafasi kwenye hiyo filamu.

Kufika mezani niliwapa Acting resume na headshot. Niliulizwa kama nimewahi kuactin kama Nurse. Nikawaambia ndio, niliwahi kuacti Nurse Malika kaitika sinema, Maangamizi the Ancient One.

Kama tunavyosema kwenye dunia ya acting, 'Break a Leg'. Kama kuna mdau aliyeenda huko karibu mtoe experience yako katika hiyo Casting Call.

Kwa habari zaidi soma:

http://wbztv.com/local/Martin.Scorsese.Leonardo.2.638533.html

Tuesday, January 22, 2008

Mnaotaka kuwa katika sinema ya Hollywod hii ni nafasi yenu!




Kwa wadau wanaosoma habari nazoandika hapa kwenye blogu wanajua kuwa nimewahi kuzungumzia suala ya Open Casting Call. Katika sinema mara nyingi waigizaji wanaitwa kufanya audition kupitia kwa agent. Zingine zinakuwa wazi, yaani mtu yeyote anaruhusiwa kwenda.

Mwongozaji sinema maarufu, Martin Scorsese atakuwa hapa Boston anatengeneza sinema ambayo inaitwa Ashecliffe kuanzia mwezi Machi. Hadithi enyewe inatokana na kitabu cha Shutter Island. Nimekisoma na kwa kweli ni kizuri. Nafasi za weusi zipo nyingi lakini kama wasaidizi hapo hospitalini.

Jumamosi hii kutakuwa na Open Call. Kwa vile inatangazwa kila mahala mtegemee kusimama kwenye foleni ndefu, maana watu watatoka New York, New Jersey, Rhode Island, New Hampshire etc. Sinema ya Scorsese si mchezo bwana! Halafu wanakuwa na bajeti kubwa za Hollywood.

Leonardo DiCaprio
atacheza kama mhusika mkuu, Teddy Daniels. Ben Kingsley atacheza kama Dr. Cawley.

Baadhiya sinema maarufu amabazo Martin Scorsese ameongoza ni, Goodfellas, Raging Bull, Casino, Kundun na The Departed.

Habari za Open Call ziko chini.

*********************************************************************************

Grant Wilfley Casting is opening a satellite office in Boston for the feature film ASHECLIFFE directed by Martin Scorsese and starring Leonardo DiCaprio. Filming begins in the Boston, Mass. area in March 2008. An open call will be held from 10am to 4pm on Saturday Jan. 26 at Boston University (George Sherman Union- Metcalf Hall) 775 Commonwealth Ave. Boston, MA 02215 to cast extras for the feature film.

This film is set in the 1950s in a mental institution with flashbacks to a WWII concentration camp. Casting for people to play mental institution staff (doctors, nurses, orderlies, guards), mental patients (including interesting, quirky or unusual character faces), the malnourished and emaciated concentration camp prisoners (many of whom will have their heads shaved), and people to play WWII American and German soldiers (young athletic types, people with military or law enforcement experience and knowledge of firearms, police officers, fire fighters, ROTC, etc). Seeking men who are willing to have their hair cut short and women with natural-looking hair color, no highlights. Specifically seeking Caucasian and African American people.

I
f you cannot attend the open call, you can mail in a recent picture and contact information to our NY offices - Ashecliffe Production Office, Attn: Grant Wilfley Casting, 51 Sleeper Street, 5th Floor, Boston, MA 02210 or email boston@gwcnyc.com.