Monday, May 30, 2016

Miss Tanzania USA Atembelea Shule ya Kenton Dar

Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara akiongea na wanafunzi wa Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam siku alipotembelea shuleni hapo katika moja ya majukumu yake ya kuhudumia jumuiya. Miss Kamara anadhamini wanafunzi wawili shuleni hapo
Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akimkabidhi msaada mwalimu mipira siku alipotembela shule ya Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania USA Aesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wawili anaowadhamini kwa kuwasomesha shuleni hapo.
Picha ya pamoja

Saturday, May 28, 2016

Waziri wa Serikali ya Zanzibar Afumaniwa Gesti Akiwa na Binti yake wa Kambo!

video video
Aliyekuwa Mkuu wa Kkoa wa Kaskazini Pemba na Katibu Ikulu Ndogo ya Pemba Mh.Faki Dadi Faki.amekutwa guest akiwa na mtoto wa mke wake wa ndoa!

Iinasemekana ni mtu na mpenzi wake. Ila baada ya mtoto kutiliwa mashaka akajaribu kuficha ficha leo ametegwa na kunaswa kwenye mtego ulioshuhudiwa na mama yake mzazi (mtoto akikutwa kitandani na baba wa kambo) hayo yalifanyika katika hotel ya Excutive iliopo pembeni ya makao makuu ya uhamiaji.

Hali ya Sukari Tanzania sasa Shwari!

 
 
 
HALI ya upatikanaji sukari nchini, imeanza kuwa kwenye mwelekeo mzuri, baada ya tani zaidi ya 10,000 kuingizwa kutoka nje. Nyingine 31,000 zinasubiriwa kuwasili huku viwanda vya bidhaa hiyo pia vikianza uzalishaji wiki hii.
 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alitoa taarifa hiyo jana bungeni wakati mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukihitimishwa.
Akielezea sukari inayoingia kutoka nje, Mwijage aliwataka wafanyabiashara wote wanaojishughulisha na bidhaa hiyo, kujitambulisha kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ili wanayopewa Dar es Salaam, waifikishe kwa viongozi hao waione.
 
Kuhusu viwanda ambavyo awali vilitarajiwa kuanza uzalishaji Julai mwaka huu, Mwijage alisema, “Adha ya sukari iliyokuwepo, sasa inakwenda kuisha. Kuna sukari ya kutosha…kwani leo kiwanda cha Kagera Sugar kimeanza kuzalisha tani 250.”
 
Waziri Mwijage alisema pia Kiwanda cha Kilombero (K One), kimeanza kuzalisha na kitazalisha tani 600 kwa siku. Wakati matumizi ya nchi ni tani 1,200 za sukari kwa siku, Mwijage alisema tofauti iliyobaki ndiyo imeagizwa kutoka nje.
 
Aliwataka wabunge kutambua kuwa uamuzi uliochukuliwa na serikali, ulijenga imani na kuleta wawekezaji. Alisema hivi sasa, Kiwanda cha Sukari Kagera kinapanua eneo la Kitegule na kuzalisha tani nyingine 60,000 na pia kukiwa na mwekezaji kutoka Oman, ambaye ataongeza uzalishaji katika kiwanda hicho na kufikia tani 300,000.
 
Alisema adha ya sukari ambayo nchi inapitia sasa ni kwa ajili ya kudhibiti uingizaji sukari na kisha kuleta wawekezaji kwenye uzalishaji wa sukari. Mwijage alisema hali ya sukari ni ya kutosha na sasa wamechukua hatua ya kujenga kiwanda cha Kigoma Sugar katika eneo la hekta 47,000.
 
 Kutoka 

Friday, May 27, 2016

Vijana wa Parking Mjini Mwanza Walalamikiwa!

Gari la mmoja wa wagonjwa katika kituo cha afya cha Bio Health kilichopo mtaa wa liberty jijini Mwanza likiwa limepigwa cheni.
Na BMG
Vijana wanaokusanya ushuru wa tozo za maegesho ya magari jijini Mwanza, wamelalamikiwa kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kinyume na taratibu.

Vijana hao wamelalamikiwa kutokana na tabia yao ya kuvizia magari yanayoegeshwa katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza huku baadhi ya maeneo hayo yakiwa ni halali kwa ajili ya magari kuegeshwa kwa muda.

Katika mtaa wa Liberty jijini Mwanza, vijana hao wamelalamikiwa kutokana na kuvizia magari binafsi yanayowapeleka wagonjwa katika kituo cha afya cha Bio Health kwa ajili ya matibabu.
Picha Zaidi Bonyeza HAPA

Thursday, May 26, 2016

Anusurika Kifo Baada ya Kujirusha Kutoka kWneye Mnara wa simu Mjini Mwanza

Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Na BMG
Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo.


Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.

Sunday, May 15, 2016

Shukurani Kutoka Kwa Familia ya Michuzi - Msiba wa Maggid Muhidin

Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi inapenda kutoa shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki iliyopita na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.
Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu. Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko wengi mno.
Pamoja na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na familia yao yote, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa. TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...

Salamu zingine za kipekee ziwaendee watumishi wote wa Ubalozi wetu Afrika kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban kuja Dar es salaam. MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA...

Vile vile shukrani za kipeke ziwaendee Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima zote. ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...

Kwa Uongozi wa msikiti wa Maamur uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni pamoja na mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.
Tutakuwa watovu wa fadhila endapo kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote ambayo baba mfiwa Ankal ni mwanachama. Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas, RUBY 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani. TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA KWA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...
Mwisho, lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa shirikia la ndege la Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.

HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE...

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

AMIN!
Saturday, May 14, 2016

Mazishi ya Maggid Muhidin Leo

CODES:
Mwili wa marehemu ukiingizwa katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es salaam leo tayari kwa kuswaliwa kabla ya mazishi.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimfariji baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi.
Mama wa marehemu (aliyevaa nguo nyeupe) akiwa na ndugu wa karibu wakiomboleza.
Baba wa marehemu akiwa na viongozi wa dini wakiombea mwili wa marehemu dua.
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na ndugu wa marehemu.
Baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi akipata chakula.
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwasili msibani Wazo hill akiwa na baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi.
Baba wa marehemu akiwa na Balozi Cisco Mtiro na baadhi ya waombolezaji.
Baba wa marehemu (mwenye kofia), Ankal Issa Michuzi akipewa pole na baadhi ya waombolezaji mara baada ya maziko ya mtoto wake Maggid Muhidin Michuzi (18)yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akimpa pole Issa Michuzi.
Rais Mstaa mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akimfariji Ankal Issa Michuzi.
Issa Michuzi (mwenye kofia) akifuatiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe Ombeni Sefue. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo wakati maziko.
Waumini wakiomba dua.
Baba wa marehemu Issa Michuzi (katikati) akiwa na huzuni akiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde
Baba mkubwa wa marehemu, Ismail Issa Michuzi akitoa shukrani kwa walioshiriki mazishi ya mtoto wao.
Mroki Mroki ambaye aliyekuwa MC akitoa ya muongozo wakati wa mazishi.
Waombolezaji wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi akiweka udongo.
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akiweka udongo kaburini.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiweka udongo kaburini.
Baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi akiweka udongo kaburini.
Mwili wa marehemu ukiwekwa kaburini.
Mwili ukiwasili makaburini.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete akimpa pole baba wa marehemu, Ankal Issa Michuzi. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi. Picha zote na Francis Dande