Showing posts with label Barbershop. Show all posts
Showing posts with label Barbershop. Show all posts

Saturday, March 08, 2014

Barbershop Girls - Umalaya kwa Kinyozi

Mdau TJK ameleta hoja hii. Mnasemaje wadau? Je, ni kweli hao barabershop girls wanavunja ndoa za watu? Navyoona midume ndo inashindwa kujizuia!


 ******************************



Mwanzo ilikuwa ni vita na wahudumu wa bar. Wanawake walio kwenye ndoa
waliishi kwa hofu ya ndoa zao kuingiliwa na wadada warembo wanaovaa nusu
uchi kweye bars zilizopo karibu kila sehemu ya Dar es Salaam. Lakini sasa,
mambo yamehamia kwenye babaershops/salon za kiume.

Nadhani kila mtu anajua babershop ni nini, na pia anajua barbershop za siku
hizi sio kukata nywele peke yake,bali inajumuisha angalau lisaa limoja la
kufanyiwa scrub, massage, manicure, pedicure etc.

Tunajua wasichana hao wakati wa kutoa huduma hawawezi kuepuka kugusa wateja
wao so gently usoni wakati wa kufanya scrub na massage. huduma wakati
mwingine huenda zaidi ya huduma za kinyozi , wakati mwingine wateja
wanauliza kukutana na wasichana hawa baada ya saa za kazi. " Wakati
mwingine wasichana hulipwa fedha za ziada kwa kisingizio cha kuthamini
huduma waliyotoa.

Barbershops nyingi zimegeuka kuwa mahala pa biashara ya ngono. Wanaume
hawana muda tena na wahudumu wa baa, na hii ni tishio kwa ndoa nyingi hapa
mjini.

Je unalo la kusema kuhusu hili? Karibu tujadiliane!