
Loh! Mgombea rais wa Republicans, John McCain kajikanyaga kweli. Kasema ata veto kila bia! "I will veto every beer..." Yaani badala ya kusema akiwa rais ata 'veto' bill kasema ata 'veto' beer. Huwa maSenator wanaleta bill kuhusu mambo mbalimbali kwa rais na ni juu yake kuzipitisha au anaweza kupinga. Akipinga inaitwa 'veto'.
Sasa watu wamekasirika. Wapenda bia wanasema kuwa ni bora wananyime kila kitu lakini wasinyimwe bia zao! Wengine wanasema kuwa sasa ni wazi kuwa McCain ni mzee mno na hafai kugombea urais. Wanasema kuwa yeye ni mjinga kama George Kichaka na wanamwita McBush.
Mnaweza kuona na kumsikiliza hapa:


