HONGERA STEVEN KANUMBA!
*****************************************************************************
Maelezo na picha kutoka Abdallah Mrisho Blog:
Kinara wa filamu za Bongo, Steven Kanumba (shoto), hivi sasa yupo katika shooting ya filamu nyingine mpya ambayo anatarajia kuwashirikisha wasanii wa Africa Mashariki, filamu hiyo itajulikana kwa jina la Hero Of The Church na itaongozwa na Director kutoka Nigeria, Feme Ogodegbe (pichani kulia). kati ni Princess Sheila Mvununje kutoka Uganda ambaye naye atakuwemo kwenye filamu hiyo.
Baadhi ya mastaa wa falamu za Bongo watakaokuwemo ndani ya filamu hiyo ambayo imeanza kurekodiwa jijini Dar. Mnamcheki 'dogo' Ben (kushoto hapo) alivyojazia siku hizi?


