Showing posts with label George Hussein Obama. Show all posts
Showing posts with label George Hussein Obama. Show all posts

Saturday, August 23, 2008

Mdogo wake Obama anaishi kwa dhiki Nairobi


Mdogo wa mwisho wa Senator Barack Obama, ambaye anagombea urais wa Marekani, amaepatikana huko Nairobi Kenya. George Hussein Obama (26) anaishi kwa dhiki huko kwenye kitongoji cha Huruma.
Vyombo vya habari hapa Marekani vinamsema Obama. Wanasema kuwa Obama anaishi kwenye nyumba ya fahari, huko modogo wake anaishi kwenye eneo hatari na kwenye dhiki.
Lakini niulize, unadhani wazungu hapa watafurahi kusikia kuwa Obama mdogo kapata visa kuja Marekani? Wanafiki kweli! Hawapendi kuona weusi wanapata visa, walilamika kweli waHaiti na waSomali walivyopata visa kwa wingi kuja Marekani, lakini husikii wakilalamika kuwa wazungu kutoka Bosnia au Russia wanapata visa. Na ngoja, mtasikia wazungu wa Georgia wamepata kwa wingi. Hakuna atakayesema kitu.
Haya tuone Obama atamsaidiaje ndugu yake. Inaelekea kuwa ndugu zake wengine hawako karibu naye huyo kijana.
Kwa habari zaidi someni: