Showing posts with label Graduation. Show all posts
Showing posts with label Graduation. Show all posts

Thursday, May 24, 2012

Mwanangu Apata Nondoz!

Wadau, nafurahi kuwatangazia kuwa mwanangu Elechi Henry Kadete amepata shahada, Degree of Bachelor of Arts' kutoka Chuo Kikuu cha Brandeis (Brandeis University), Waltham, Massachusetts.  Major yake ilikuwa ni Business.  Sherehe ilikuwa jumapili iliyopita. Kweli safari ilikuwa ndefu na kulikuwa na matuta mengi njiani, lakini kafika. Baba yake marehemu Prof. Henry Kadete, lazima anatabasamu kutoka mbinguni.

Brandeis ni Chuo Kikuu cha Wayehudi, lakini wanapokea wanafunzi kutoka nchi mbalimbali na dini mbalimbali.  Imam alisoma sala ya kufungua sherehe. Baadaye Rabbi wa kiyehudi, na Padre wa Kikristo walitoa sala za kufunga sherehe.


Hongera Elechi!


L-R Dr. Aleck Che-Mpomda (babu), Mimi, Elechi, Camara (kaka), Malaika (mama mdogo) na Mrs. Che-Mponda (bibi)  Watoto wadogo ni watoto wa Malaika
Mimi na Elechi
Elechi na Bibi na Babu yake

Mama na Mwana

Graduates wa  Bachelor of Arts wakitoka ukumbini
Elechi akiwa na siku tatu tangu azaliwe,, Hapa ni 21 Kileleni Road UDSM 1989
Imam akisuali kabla ya ceremony kuanza

Elechi na Babu yake, Dr. Aleck Che-Mponda

Monday, May 25, 2009

Hongera Mwanangu!


Wadau, ninapenda kuwajulisha kuwa mwanangu Camara Kadete, amepokea digrii (shahada) yake ya kwanza, Bachelor of Arts, kutoka McDaniel College, Westminister Maryland, juzi jumamosi. Baba yake ni mume wangu wa kwanza Prof. Henry Kadete (marehemu). Hongera sana!


Commencement 2009 McDaniel College


Proud Mama
Mimi na mwanangu Camara nje ya ukumbi.


Kushoto kwangu ni mchumba wa Camara, Bi Shalanda naye alipokea digrii Bachelor of Arts.

Tulimaliza kusherekea kwa keki, Camara na Shalanda wakizima mishumaa