Showing posts with label Harrison Mwakyembe. Show all posts
Showing posts with label Harrison Mwakyembe. Show all posts

Monday, June 16, 2008

WaBunge Waogopa Kukalia Viti Vyao! Vina uchawi!


Ilibidi nicheke baada ya kusoma hii habari hasa nikifikiria wabunge kwenye ukumbi wa bunge wakichunguza viti vyao. Hivi kweli unaweza kufuta uchawi/juju hivi hivi?

*******************************************************************

Ndumba Bungeni: Wabunge wahofia viti vyao
2008-06-16
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Ikiwa leo ni siku ya kwanza kwa wabunge kuingia tena ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya kuwapo kwa uvumi wa kunyunyizwa vitu vinavyodhaniwa kuwa ni vya kichawi kwenye viti vyao, baadhi ya wabunge wameonekana leo asubuhi wakiwa bado wanahofia siti zao na hivyo kulazimika kuangalia na wengine kuvipangusa na leso zaidi ya mara moja kabla ya kuketi.
Tukio hilo la wabunge kudaiwa kuwekewa vitu vya kichawi kwenye siti zao, limedaiwa kutokea katikati ya wiki iliyopita na kuzua hofu kubwa, hivyo kuilazimu ofisi ya Bunge, kupitia kwa Kaimu Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilillah kutoa taarifa kuwa ukumbi uko shwari na hakuna tishio lolote la usalama kwa waheshimiwa wabunge.
Hata hivyo, licha ya kuhakikishiwa kuwa hakuna hofu yoyote bungeni humo, bado baadhi ya wabunge walionekana wakiwa na hofu na kuchunguza sana viti vyao kabla ya kukaa.
Hata hivyo, hofu ya wabunge hao waliokuwa bado wamejawa na hisia kuwa pengine wamefanyiwa kitu mbaya kwa kuwekewa vitu vya kudhuru, iliondolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Samwel Sitta, ambaye alitoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na sakata lenyewe kabla ya kuwataka wasiwe na hofu na badala yake waendelee na majukumu yao bungeni humo kama kawaida kwani ukumbi ni salama.
Akizungumza wakati wa kikao cha asubuhi ya leo, Spika Sitta amesema vyombo vya usalama, ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa, vimefanya uchunguzi ukumbini humo na kumhakikishia kuwa hauna hatari yoyote.
Akizungumzia sakata lenyewe, Spika Sitta akasema lilianza kwa kuonekana watu wawili wakitangatanga bungeni humo siku ya Jumanne iliyopita, mishale ya saa 2:00 usiku. Akasema taarifa za kuwapo kwa tukio hilo, alizipata siku ya Alhamisi baada ya kuambiwa na Katibu wa Bunge kuwa kamera za usalama ndani ya ukumbi wa Bunge, zimenasa watu wawili wakitangatanga Bungeni.
Akasema picha hizo zikamuonyesha mtu mmoja kati yao akiwa na vitu mkononi ambavyo alikuwa akivinyunyiza sehemu mbalimbali.
Spika Sitta akasema siku hiyo baada ya kupewa taarifa wakati kikao cha Bunge kikiendelea, akatumiwa kimemo na Mbunge Victor Mwambalaswa, akimjulisha kuwa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa ameugua ghafla ndani ya ukumbi huo.
Akasema alipohusianisha matukio hayo, alihisi huwenda vitu vilivyoonekaka vikirushwa na mtu aliyenaswa na kamera za usalama ilikuwa ni sumu ya kisasa. Akasema hapo ndipo akachukua hatua ya kulikabidhi suala hilo kwa Polisi na Usalama wa Taifa ili kulifanyia uchunguzi wa kina.
Akasema Jumamosi ya juzi, Polisi na maofisa wa Usalama wa Taifa walimpatia ripoti ya uchunguzi, wakimhakikishia kuwa ukumbi huo ni salama. Akasema hata hivyo, suala la kuwabaini watu walionaswa na kamera wakitangatanga ndani ya ukumbi wa bunge, bado linaendelea kuchunguzwa na kuwa litachukua muda mrefu kidogo.
Akasema kuwa suala hilo linahitaji muda kwa vile uchunguzi wake unahitaji kurejea kwenye matukio ya nyuma kwa zaidi ya saa 72 ili kujua kilichotokea siku hiyo. Baada ya ufafanuzi huo, Bunge liliendelea na kikao chake kama kawaida, ambapo mjadala kuhusu bajeti ulianza na hadi tukienda mitamboni, wabunge 56 walishajiorodhesha kwa ajili ya kuchangia mjadala huo.

Friday, June 13, 2008

Ugua Pole - Dr. Harrison Mwakyembe

Dr. Harrison Mwakyembe

Wadau huko wenye habari za kuugua kwa Dr. Harison Mwakyembe atupe. Dr. Mwakyembe na ripoti yake kiboko juu ya ufisadi wa Richmond ndo iifungua mlango wa kupiga vita ufisadi Tanzania.

Tunamwombea apone haraka.

******************************************************************************
Kutoka ippmedia.com

Dk. Mwakyembe: Hali yake bado tata

2008-06-13

Na Mwandishi Wetu,Dodoma

Hali ya afya ya Mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, Mhe. Dokta Harrison Mwakyembe bado haijaimarika na watu wake wa karibu wamesema bado anaendelea na matibabu.

Mbunge huyo aliyeibuka kuwa shujaa hivi karibuni baada ya kuiongoza kwa umahiri Kamati ya Bunge iliyoanika siri zote kuhusu dili za mkataba wa utata baina ya Serikali na Kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond, ameelezewa kuwa hali yake haijatengemaa tangu jana aliposhikwa na ugonjwa ghafla akiwa bungeni na kulazimika kutoka nje ya ukumbi.

Imeelezwa zaidi kuwa hadi sasa, kile kilichomfanya Dokta Mwakyembe azidiwe ghafla na kulazimika kutoka nje ya Bunge jana hakijafahamika. ``Bado hajawa ok kwa asilimia mia moja... ila anendelea vizuri,`` amesema mmoja wa watu walio karibu na Mbunge huyo.

Alasiri ilipojaribu kuzungumza na baadhi ya wabunge wenzie, imebaini kuwa Mheshimiwa Dokta Mwakyembe ameanza kupata nafuu kulinganisha na hali aliyokuwa nayo jana baada ya kulazimika kutoka kwenye ukumbi wa Bunge.

Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Mbunge wa Mbeya Mjini (CCM), Mhe. Benson Mpesya, amesema ni kweli Mbunge mwenzie huyo aliumwa ghafla jana wakati akiwa Bungeni, lakini hivi sasa hali yake inaendelea vizuri. ``Ni kweli Dkt. Mwakyembe aliugua ghafla... lakini ni kazi ngumu kuzungumzia afya ya mtu. Ila ukweli wa yote ni kwamba jana usiku, mimi nilikwenda nyumbani kwake kumjulia hali na akanithibitishia kuwa hivi sasa amepata nafuu kubwa,`` akasema Mhe. Mpesya.

Aidha, Mhe. Mpesya amesema wananchi wa Jimbo la Kyela na kwingineko nchini wasiwe na hofu na afya ya Mhe. Mwakyembe, kwani kwa kauli yake (Dk. Mwakyembe), ni kwamba hali hiyo ya kuumwa ghafla Bungeni jana ilitokana na ukweli kuwa hakuwahi kupata kifungua kinywa jana wakati akienda bungeni.

``Hali hiyo ilimssababaishia kizunguzungu na ndiyo maana akaumwa ghafla,`` akasema Mhe. Mpesya. Naye Mbunge wa Lupa (CCM), Mhe. Victor Mwambalaswa, ambaye lidaiwa kuwa ndiye aliyekuwa wa kwanza kubaini hali hiyo na kumuondoa ndani ya Bunge Dk. Mwakyembe huku akimshikilia, amesema si kweli kwamba alihusika kumtoa nje ya Bunge.

``Ndugu yangu, hata mimi nasikia tu kuwa Dk. Mwakyembe anaumwa... ukweli ni kwamba sijui hata alikolazwa na wala sijui anaugua nini,`` amesema Mhe. Mwambalaswa. Jitihada za mwandishi wa Alasiri kumpata Dk. Mwakyembe mwenyewe zilishindikana kwa jana na leo, hasa baada ya simu yake ya mkononi kutoweza kupatikana.

Dk. Mwakyembe ambaye umahiri wake umemfanya hivi karibuni awe miongoni mwa wajumbe walioandaa ripoti kuhusu mikataba ya madini nchini baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Jakaya Kikwete, ameripotiwa kuwa jana mishale ya saa 3:30 asubuhi, aliumwa ghafla wakati akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge na kukimbiziwa kwenye zahanati yao Bungeni hapo.

SOURCE: Alasiri

Thursday, February 07, 2008

Kampuni ya Richmond - Utapeli Mtupu!

Jamani, lazima niwakumbushe kuwa tangu hiyo deal ya Richmond itangazwe, wanablogu hasa kwa Michuzi walikuwa wanasema kuwa hiyo kampuni ni feki. Kuna wanablogu waliofanya uchunguzi wao kabisa. Lakini dili iliendelea! Wanablogu walichambua mpaka bei ya vifaa. Serikali ingewasikiliza tusingekuwa hapa leo tunaongelea hii habari ya kusikitisha.

Leo mambo ndo yameharibika kwa wahusika. Sijui kwa kimombo tuseme mambo yame 'explode' ame 'implode.'

Habari za Lowassa na Richmond imekuwa habari za kimataifa.


***************************************************************************

Kutoka http://abdallahmrisho.blogspot.com/

HAKUNA hapa nchini wala Marekani, kampuni iliyosajiliwa kwa jina la Richmond Development Company LLC. Bunge lilielezwa jana.

Mwenyekiti wa kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mchakato wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura ulioipa ushindi kampuni hiyo, Dk, Harrison Mwakyembe alibainisha hayo bungeni mjini Dodoma jana.

Akiwasilisha muhtasari wa taarifa ya kamati hiyo, Dk. Mwakyembe alisema uchunguzi umeonyesha hakuna kampuni yenye jina hilo iliyosajiliwa katika jimbo la Texas nchini Marekani wakati wa kusaini mkataba huo.

“Kamati teule imejiridhisha kuwa hakuna kampuni yenye jina la Richmond Development Company LLC iliyokuwa imesajiliwa JImbo la Texas wakati wa kusaini mkataba huo hadi tunapowasilisha ripoti hii…” alisema.

Alisema hitimisho lilifikiwa na kamati hiyo, linashabihiana kwa vigezo na ushauri wa kitaalamu uliotolewa na kampuni mashuhuri ya mawakili wa Virginia, Marekani inayoitwa Hunton & Williams LLP kwa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Oktoba mwaka juzi “katika ripoti yake yenye kurasa 10, kampuni hiyo ya mawakili imetamka bayana kuwa hakuna kampuni yenye jina la Richmond Development.

Company LLC kwenye masijala ya katibu wa Jimbo la Texas ambaye moja ya majukumu yake ni sawa na ya Msajili wa kampuni Tanzania.

Dk. Mwakyembe alisema, Humton & Williams LLP wameituhumu Richmond Development Company LLC kwa upotoshaji wa hadhi yake kikampuni na kutoa tamko lisilo sahihi kuhusu hadhi yake chini ya sheria za Texas.

Alisema ukaguzi wa kumbukumbu za katibu wa jimbo la Texas uliofanywa na kampuni hiyo Oktoba 2006 ulionyesha hakuna kampuni yenye jina la Richmond Development Company LLC iliyokuwa imeanzishwa na kuendesha shughuli zake jimboni humo.

Dk. Mwakyembe alisema wajumbe wa kamati hiyo, waliokwenda Marekani Desemba 10 hadi 16 mwaka jana, waliambiwa na Mohamed Gire, kuwa Richmond Development Company LLC ni jina mbadala la biashara la kampuni yake iitwayo RDEVCO LLC.

“Bwana Gire ambaye aliamua mkutano wake na wajumbe wa kamati Teule ufanyike ofisini kwa wanasheria wake, Duane Morris LLP waliopo 3200 Southwest Freeway, suite 3150, jijini Houston, alisisitiza kuwa sheria na Texas zinawaruhusu wafanyabiashara na kampuni kutumia majina mbadala au tofauti na yale yaliyopo kisheria kwa sababu za kibiashara alisema Dk. Mwakyembe.

Alisema kamati yake iliyazingatia maelezo ya Gire kwa ajili ya kuyafanyia kazi, kwa sababu kuna, majimbo mengi Marekani, likiwemo la Texas yanaruhusu matumizi ya majina mbadala katika biashara au huduma.

Lakini, Dk. Mwakyembe alisema, sheria zinaweka taratibu za kuzingatia ili kuepusha vitendo vya kitapeli katika matumizi ya majina mbadala ya kibiashara.

“Katika jimbo la Texas ambako Gire anaishi ni kosa la jinai kutumia jina mbadala bila kulisajili. Usajili wa jina mbadala unadumu kwa miaka mitano ambapo mtumiaji lazima asajili jina hilo upya kati ya januari mosi na Desemba 31 ya mwaka wa tano,” alifafanua Dk. Mwakyembe ambaye pia ni mbunge wa Kyela.

Alisema, Gire aliwakabidhi wajumbe wa Kamati hiyo hati ya uthibitisho ya Harris County, Texas ambayo kwa maoni yake, ilikuwa inathibitisha kuwa Richmond Devilopment Company LLC ni jina mbadala la biashara.

“Kamati Teule imeikagua hati hiyo kwa kina na kuona kuwa badala ya kumsaidia Gire, inazidi kuthibitisha kuwa si mfanyabiashara mwadilifu ila tapeli kwa sababu kuu mbili:
Mosi, mbali na kwamba hati hiyo ya Gire ni kivuli tu au nakala ya “hati” halisi (kama ipo), nakala ambayo haina uthibitisho wowote wa uhalali na uhalisia wake, ilikuwa ina saini ya ofisa mmoja mbadala ya wawili walioainishwa katika hati hiyo pili, badala ya hati hiyo kutamka kuwa RDEVOCO LLC imesajili jina la Richmond Development Company LLC kama Gire alivyotaka Kamati Teule ielewe, hadithi mpya kabisa inaanzishwa kuwa Richmond Development Company ni jina mbadala lililosajiliwa na Richmond Development Company LLC!

La kushangaza ni kuwa katika baadhi ya barua zake alizoiandikia TANESCO na wizara ya Nishati na Madini, Gire anatamka kuwa Richmond Development Company ni jina mbadala la biashara la RDEVCO LLC.
“Mtu anaweza akadanganyika akifikiri kuwa kiwango hiki cha ubabaishaji hakithibitishi utapeli pekee, bali vilevile elimu duni ya mmiliki wa kampuni hizo, Gire, inayomfanya asione hatari kubwa anayojitwalia ya hata kumfikisha jela kwa udanganyifu,” alisema Mwakyembe, Kwa mfanyabisahara mzoefu aliyejizungushia mawakili wa kumtetea mambo yakimwendea mrama, anajua analolifanya, hivyo Richmond Development Company LLC ni kampuni ya kimakusudi ya kimkakati ambayo haikamatiki, haishitakiki, haipigiki faini na haiadhibiki kwa lolote lile itakalolifanya kwani haina uhai wa kikampuni,” alisema.

Dk. Mwakyembe alisema, Richmond Development Company LLC, kwa maneno mengine, si kampuni ya mchana bali ya usiku, kampuni ya mfukoni ambayo shirika la umma TANESCO liliingia nalo mkataba wa mabilioni ya fedha ya walipa kodi wa Tanzania.

Rushwa, Vistisho, Uchongoanishi....




Kamati ya Dr. Mwakyembe ilifanya kazi pamoja na kwa walitishiwa na kufanyiwa mambo mengine mabaya!


SEMA, USIOGOPE, SEMA!

Nasema mkono wa Mungu umetembea, maana kuna majina mazito yametajwa mle! DUH!

*********************************************************************

" Mheshimiwa Spika, leo tunapowasilisha taarifa hii mbele ya Bunge lako tukufu, tunajisikia kuutua mzigo mzito sana ulioanza kutuelemea kutokana na kuzongwa kila kukicha na kila aina ya uzushi, uchochezi, uchonganishi na hata vitisho. Tumezushiwa kuhongwa magari ya kifahari na fedha taslimu; tumetuhumiwa kuendesha vita dhidi ya Waislamu na mara nyingine tuhuma hiyo ikageuka kuwa vita dhidi ya Wakristo ndani ya Serikali; tumesingiziwa kuibadilisha taarifa yetu mara mbili, baadhi wakisema kwa ushawishi wa fedha, wengine wakidai kwa shinikizo la Mhe. Spika na wengine kwa shinikizo la Waziri Mkuu; tumeshuhudia pilikapilika za usiku na mchana za kujipanga na kuwashawishi baadhi ya Mawaziri na Wabunge kuikana taarifa hii na mapendekezo yake kiasi cha wengine wetu kujiuliza: kulikoni mtu asiye na hatia kuweweseka?

Mheshimiwa Spika, naomba kwa niaba ya wajumbe wenzangu wa Kamati Teule, kukuhakikishia wewe binafsi na Bunge lako tukufu kuwa tumekamilisha kazi tuliyopewa kwa uaminifu na ujasiri mkubwa, dhamira safi, moyo wa uzalendo na kwa kumtanguliza mbele Mwenyezi Mungu katika kila tulilolifanya. "

KUSOMA RIPOTI NZIMA BOFYA HAPA:

Lowassa Ajiuzulu Uwaziri Mkuu!!!!


DAH! Yaani wadau kwa kweli mnisamehe, maana hii habari ya Mhesimiwa Lowassa nimesikia saa hizi, 9:56Am (EST). Nilikuwa busy na mambo ya audition ya sinema fulani.

Kwa kweli nimeshutuka sana na nimesikitika mno hasa chanzo cha kujizulu kwake. Ila nimefurahi kuona kuwa Tanzania kuna haki ya kusema siku hizi, FREEDOM OF SPEECH. Na safari hii uchunguzi ulifanyika na haikutiwa maji!

Dr. Harrison Mwakyembe, NAKUSIFU! Bado unaujasiri wa enzi zile! Ila uko salama kweli sasa?


Haya tuone nani atateuliwa kuwa Waziri Mkuu sasa. Any suggestions/predictions?



*******************************************************************************


HABARI TOKA DODOMA SASA HIVI ZINASEMA KUWA SPIKA WA BUNGE MH. SAMWEL SITTA AMETANGAZA KWAMBA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA AMEAMUA KUJIUZULU UWAZIRI MKUU.

MH. SPIKA BAADA YA KUTANGAZA HILO AMESEMA MJADALA WA RIPOTI YA RICHMOND, NA SIO MJADALA WA LOWASSA, NDIO UENDELEE. NA NDICHO KINACHOFANYIKA HIVI SASA HUKO BUNGENI.

HABARI ZAIDI ZINASEMA KWAMBA MH. LOWASSA AMESEMA KWAMBA INGAWA HAJAMTAARIFU JK UAMUZI WAKE HUO, AMEAMUA KUJIWEKA KANDO!

*************************************************************

KARAMAGI NAYE AOMBA KUJIZULU!

KARAMAGI NAYE AOMBA KUACHIA NGAZI

MH. NAZIR KARAMAGI AMEMALIZA KUJIELEZA NA AMELIAMBIA BUNGE KWAMBA NA YEYE LEO ASUBUHI AMEPELEKA BARUA KWA JK KUOMBA KUJIUZURU WADHIFA WAKE WA UWAZIRI WA NISHATI NA MADINI.

YEYE PIA AMEJITETEA KWAMBA HANA HATIA KATIKA SAKATA HILI!
******************************************************************

MSABAHA NAYE AJIUZULU!
MSABAHA NAYE AMWAGA MANYANGA

WAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI AMBAYE AWALI ALIKUWA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI DK MSABAHA NAYE KAMPELEKEA BARUA JK KUOMBA KUJIUZURU KWA MUJIBU WA MAELEZO YAKE ALIYOTOA DAKIKA HII BUNGENI

WHAT A SAD DAY IN TANZANIA POLITICS!