Showing posts with label Jada Pinkett Smith. Show all posts
Showing posts with label Jada Pinkett Smith. Show all posts

Saturday, August 30, 2008

Will Smith akutana na Rais wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar mh. Amani Abeid Karume akiongea na mcheza sinema wa Marekani Will Smith
Rais wa zanzibar mh. Amani Abeid Karume na mkewe Mama Shadya katika picha ya pamoja na Will Smith na mai waifu wake Jada Pinkett Smith leo huko Ikulu, Zanzibar.
Picha kwa hisani ya kwa mdau Othman Maulidi wa Zanzibar.

Tuesday, August 26, 2008

Will Smith safarini Bongo



(Picha kutoka Michuzi Blog)


Nimefurahi mno kuwaona akina Will Smith na mke wake Jada Pinkett Smith safarini Tanzania. Hasa baada ya kumwona Jada akikata mitaa ya Boston mwaka jana kwenye shuti ya sinema mpya The Women. Bahati mbaya sikuweza kushiriki kwenye hiyo sinema.

Haya papparazi wa Zanzibar tupeni Scoop! Natumaini Will Smith na Jada watapapenda Tanzania kiasi cha kutaka kushuti sinema huko. Mnakumbuka walishuti ile sinema ya Ali, Msumbiji na Ghana.