www.chekanakitime.blogspot.com
NAWAKUMBUSHA TU JAMANI----- Naitwa John Kitime, nilianza kufurahia vichekesho mara baada ya kuzaliwa na kukuta watu wazima kila wakinichukua walijitahidi kunichekesha kwa kuanza kuonea lugha ambayo sijaijua mpaka leo, maana mara alikuja mmoja na kuanza ‘bujibujibujibujibuji,jigijigjigjigjijij, grugrugrugru’ na maneno mengine ya ajabu nilijitahidi kuwavumilia nisiwacheulie maziwa lakini baadae nikagundua heri niwe nacheka wakianza vituko hivyo, maana baada ya hapo walikuwa wanajiona wanajua kuchekesha watoto wachanga. Niliendelea kukua nikaanza shule nakukuta vituko vingi sana vya kuchekesha, kama vile watu kujikojolea darasani, hili bahati mbaya nililikuta linajirudia pia kuwakuta wakubwa wakijikojolea kwenye baa, na kilabuni, ene way, nilimaliza shule na kujiunga na vyuo mbalimbali nchini na huko nilijifunza utalaamu wa kunywa pombe na huko nilikutana na watu wengi wenye kujua kuchekesha, kucheka na hata wasiojua kuchekesha wakijitahidi kuchekesha, cha kushangaza si nikakuta wengine hawajui kucheka kabisa, au wanaweza kucheka mahala pasipo na kichekesho cha kuchekesha wachekaji.
Katika kiota hiki cha www.chekanakitime.blogspot.com , ntaweeleza mengi yaliyonikuta katika maisha yangu haya yaliyojaa furaha sana NAMSHUKURU MUNGU.
Pia mimi ni mwanamuziki napiga gitaa naimba kwenye bendi, lakini huwa sichezi, sijui kucheza, hasa Chacha ndio kabisa halafu siku hizi kuna hii inaitwa Kwaito, wakati najitahidi kujifunza imeanza Azonto, jamani si mngoje japo nijuwe staili moja ndio mbadili? Halafu huwa inanishangaza, mtu analipa kuingia muziki halafu anacheza kuliko sisi wanamuziki jamani, mnajua mngepewa majembe mlime badala ya kucheza mngesha maliza tatizo la njaa hapa nchini?
Showing posts with label John Kitime. Show all posts
Showing posts with label John Kitime. Show all posts
Monday, January 07, 2013
Monday, March 30, 2009
John Kitime na Anania Ngoliga
.jpg)

Wadau, wanamuziki wa kiTanzania, John Kitime na Anania Ngoliga wako katika Tour hapa USA. Ratiba yao iko chini.
************************************************************************************
Ujumbe kutoka kwa John Kitime:
Hallo, nimerudi tena tuko katika tour bus tunaelekea Redding, mpaka sasa maonyesho yetu yote yamekuwa full house, kundi zima tunapiga muziki ambao ulitokana na kukutana kwetu na mwanamuziki wa hapa Marekani Bela Flek ambae hupiga banjo na alikuja Afrika kama kupata historia ya banjo akatembelea Tanzania, Uganda, Mali, Madascar na South Africa. Akaweza kutengeneza documentary ya safari hiyo na pia kurkodi CD iliyoshirikisha wasanii toka nchi hizo. Hivyo maonyesho yetu ni yenye wanamuziki toka nchi hizo kutoka Tanzania tuko wawili mwenzangu Anania ambaye ni kipofu anapiga marimba wakati mimi napiga gitaa. Mpaka sasa mambo ni swafiiii
RATIBA/ SCHEDULE
Date Venue Location
3/26/09 The Colony Theater Pittsfield, MA
3/27/09 Playhouse Ridgefield, CT
3/28/09 R.P.I. Troy, NY
3/29/09 Music Hall Tarrytown, NY
3/30/09 Berks Jazz Festival Reading, PA
4/1/09 Shelton Concert Hall St. Louis, MO
4/2/09 Uptown Theater Kansas City, MO
4/3/09 Tennessee Theater Knoxville, TN
4/4/09 Music Festival Savannah, GA
4/5/09 University of Florida Gainesville, FL
4/7/09 Duke University Durham, NC
4/8/09 Ryman Auditorium Nashville, TN
4/9/09 State Theater
w/ Toumani Diabate, D'Gary, & Anania Ngoglia Fall Church, VA
4/10/09 University of Pennsylvania Philadelphia, PA
4/11/09 Zeiterion Theater New Bedford, MA
RATIBA/ SCHEDULE
Date Venue Location
3/26/09 The Colony Theater Pittsfield, MA
3/27/09 Playhouse Ridgefield, CT
3/28/09 R.P.I. Troy, NY
3/29/09 Music Hall Tarrytown, NY
3/30/09 Berks Jazz Festival Reading, PA
4/1/09 Shelton Concert Hall St. Louis, MO
4/2/09 Uptown Theater Kansas City, MO
4/3/09 Tennessee Theater Knoxville, TN
4/4/09 Music Festival Savannah, GA
4/5/09 University of Florida Gainesville, FL
4/7/09 Duke University Durham, NC
4/8/09 Ryman Auditorium Nashville, TN
4/9/09 State Theater
w/ Toumani Diabate, D'Gary, & Anania Ngoglia Fall Church, VA
4/10/09 University of Pennsylvania Philadelphia, PA
4/11/09 Zeiterion Theater New Bedford, MA
Subscribe to:
Comments (Atom)


