Showing posts with label Kanye West. Show all posts
Showing posts with label Kanye West. Show all posts

Tuesday, March 09, 2010

Mzungu Am 'Kanye West' Mweusi kwenye Oscars

Umesikia kituko kilichotokea kwenye Oscars juzi? Huyo Roger Ross Williams alikuwa anapokea tuzo kwa ajili ya sinema ya 'Music by Prudence'. Ghafla katokea bibi wa kizungu, Elinor Burkett, na kuanza kusema, "mwache mwanamke aongee" na maneno mengine ambao watu hawakuelewa.

Sisi watazamaji tulishangaa sana inatokea nini. Kumbe huyo mzungu aliwahi kuwa producer wa hiyo sinema lakini waligombana na Williams. Burkett alimpeleka mahakamni lakini walisuluhisha nje ya mahakama. Burkett aklisem hakupenda jinsi sinema ilivyokuwa inaenda. Ajabu, jinsi ilivyoenda ndo ikashinda Oscar!

Lakini wadau , hii kituko kisingetokea tusingekumbuka habari ya hiyo sinema, Music by Prudence. Pia hao Williams nad Burkett wasingejulikana. Sasa hivi Letterman, Leno na wengine wanamtania huyo Burkett. Bila shaka na Saturday Night Live watamtania!

Pia wanamwita Burkett, Lady Kanye! Kumuka mwaka jana Kanye West alivyoingia hotuba ya Taylor Swift kwenye tuzo za MTV.

Saturday, November 24, 2007

Rappers wamtukana Dr. Jan Adams



Rappers hawana dogo. Wametoa wimbo wa kumtukana Dr. Jan Adams aliyemfanyia mama yake mzazi Kanye West, upasuaji wa urembo na kusababisha kifo chake.

- Dr. Jan Adams alikuwa na TV show kwenye Discovery Channel, Plastic Surgery Before & After
- Alikuwa siyo Board Certified
- Oprah amekaa kimya. Alimwalika kwenye show yake kama mtalaam wa upasuaji wa urembo kumbe jamaa ni feki! Watu wengi waliamini 'utalaamu' wake kwa vile alikuwa kwenye Oprah.

http://www.drjanadams.com/

Cheki website ya jamaa, mambo mengi eti yako "down for maintenance" LOL!

Kinachonisikitisha katika hii kesi ni kuwa huyo jamaa ni mweusi, alikuwa anaonekana kama mtaalamu wa mambo ya plastic surgery. Kumbe jamaa tapeli!

Wednesday, November 21, 2007

Dokta aliyempasua mama yake Kanye West amkimbia Larry King



Mama yake mzazi Kanye West alifariki dunia majuzi baada ya kufanyia opresheni ya urembo. Opresheni eneyewe ilikuwa ya kupunguza matiti (breast reduction), kupunguza nyama kwenye tumbo (tummy tuck) pamoja na kuondoa mafuta (liposuction). Daktari mwenyewe ni Dr. Jan Adams.

Navyoona walimfanyia huyo mama opresheni nyingi kwa mpigo. Kawaida wangefanya moja wasubiri, wafanye nyingine, halafu wasubiri tena. Lazima alikuwa na maumivu makali.

Kanye West mwenyewe amesema alikubali kulipa gharama za hiyo opresehni lakini alitaka mama yake aende kwa trainer. Alisema kuwa mama mwenyewe alisisitiza kuwa alitaka hiyo opresheni.

Jana Dr. Adams alialikwa kwenye show ya Larry King ili ajitetee. Alikaa dakika moja halafu alikimbia. Baada ya kifo cha mama Kanye, utalaamu wake wa kufanyia opresheni za urembo ulianza kuchunguzwa na bodi ya madaktari. Pia iligundulika kuwa Dr. Adams, alikamatwa na polisi akiwa anaendesha gari amelewa.
Pia baada ya kifo cha mama Kanye, wanawake wengi walijitokeza kulalamika juu ya huduma anayotoa. Wengine wanasema kuwa Dr. Adams aliwacheka baada ya kulalamika mfano matiti yameenda upande! Mwingine anasema alienda kwa Dokta mwingine na kukutwa kuwa Dr. Adams aliacha sponji ndani!
Unaweza kuona Video ya Larry King hapa:

Dr. Donda West alizikwa kwao Oklahoma City jana.

Monday, November 12, 2007

Mama yake mzazi Kanye West Amefariki


Kanye West na mama yake, Dr. Donda West

Kuna habari ya kusikitisha na ya kushangaza....mama yake mzazi, mwimba rap, Kanye West, amefariki dunia ghafla siku ya jumamosi.

Mama yake, Dr. Donda West, alikuwa na miaka 58. Habari za kuaminikia zinasema alikufa baada ya kufanyiwa opresheni ya urembo, lakini hawakusema ilikuwa ni opresheni ya aina gani.

Huenda ilikuwa ya kupunguza matiti, matako, uso, liposuction (kupunguza mafuta).

Mama yake alikuwa meneja wake. Alistaafu kazi ya kufundisha kiingereza Chuo Kikuu cha Chicago kusudi awe na mwanae.
Mungu amlaze mahali pema mbinguni. AMEN.

Kwa habari zaidi someni: