Asante Kaka Beda Msimbe (Lukwangule Blog)Kampuni mama ya kutayarisha, kudurufu na kusambaza sinema Tanzania inayokwenda kwa jina la Tollywood Movies, imechukua dhamana ya kusambaza movie mpya ya kutisha iitwayo Roho Sita, Joseph Shaluwa anashuka nayo.
Roho Sita ambayo imetayarishwa na Koga Film chini ya Mkurugenzi wake Thomas Simon, itakuwa sinema ya kwanza ya kutisha ambayo matukio mengi yanaonekana halisi tofauti na nyingine zilizotangulia.
Mkurugenzi wa Filamu za Tollywood Movies, Hamie Rajab, aliliambia Ijumaa kwamba, katika sinema zote za kutisha za Tanzania, hakuna iliyowahi kuifikia ubora wa Roho Sita.
“Mpaka Tollywood tumeamua kuichukua basi mashabiki waamini kwamba kitu kimetulia, ni sinema ya kwanza ya kutisha ambayo kila kitu kinaonekana halisi, kubwa zaidi ni kwamba program iliyotumika katika uhariri ni ya kisasa duniani, ndiyo maana imeifanya kuwa bora na yenye kiwango cha Kimataifa.
Wadau wasubiri kidogo, siku si nyingi ngoma itaingia mtaani,” alisema.
Baadhi ya wakali walioonyesha uwezo wao katika kitu hicho ni pamoja na Ndumbangwe Misayo, Charles Magali, Juma Kankaa, Chuchu Hans na Evans Komu ambao wameigiza katika kiwango cha hali ya juu huku uhusika ikiwa ni kitu cha kwanza.
NB - Promo hii nimeinyaka kwa kaka abbycool ndani ya http://abdallahmrisho.blogspot.com/


