Showing posts with label Mel Gibson. Show all posts
Showing posts with label Mel Gibson. Show all posts

Friday, September 05, 2008

Sinema Edge of Darkness imepata pigo!

Robert DeNiro akiwa kwenye seti hapa Boston juzi

Wadau, ile sinema, Edge of Darkness ambayo nimo kama background (extra) policewoman imepata pigo. Moja wa waigizaji wakuu, Robert DeNiro, amejitoa ghafla kwenye sinema. Alikuwa ameshashuti scene kama mbili hapa Boston. Scenes zilikuwa kwenye golf course.

Yaani tunashangaa imekuaje tena. Watu walikuwa wamepania kweli kuwa kwenye scenes na DeNiro. Sasa itabidi wazishuti tena. Mimi sikuwepo kwenye hizo scenes zake za wiki hii.

Wanasema kuwa wanatafuta mwigizaji mwingine kuchukua nafasi yake. Kwa sasa inabidi wabadilishe ratiba ya kupiga sinema, na watashuti scenes ambazo character ya DeNiro (Darius Jedburgh) haimo. Mjue leo watu wamehaha kutafuta jeti kwenda Hollywood kutafuta star mwingine.

Jamani, Mel Gibson alimwudhi au Boston haijamfaa? Nilivyokuwa kwenye set nilimwona Mel kama mtu poa, mcheshi na alikuwa anajichanganya na sisi extras bila wasiwasi. Mpaka wakati wa kula alikuwa anakuja kula na sisi. Lakini hao stelingini wengine hutawaona wanakula na crew na extras au actors wengine. Wanapelekewa chakula kwenye trela yao ya kifahari au wanapelekwa kula hotelini. Na wengine hata wakati wa kushuti wanakaa mbali na wengine. Wakati mwingine mnaambiwa msiwatizame! (haki ya mungu!) Hebu fikiria Mel Gibson alivyokuwa poa, anagongana na sisi na wala hajali.

Kwa sasa wasemaji wa DeNiro wanasema kuwa kajitoa kwa ajili ya 'creative differences' yaani hakubaliani na jinsi sinema invyoenda, au staili ya mwongoza sinema. Wengine wanasema kuwa ni 'code' kuwa anaenda rihabu (yaani sehemu wanapoenda walevi wa madawa ya kulevya navitu vingine kupumzika).

Hollywood bwana! Nitaendelea kuwapasha.

Kwa habari zaidi soma:

http://www.variety.com/article/VR1117991604.html?categoryid=13&cs=1


Thursday, August 28, 2008

Afande Chemi!

Wadau tangu jana ninaigiza katika sinema, Edge of Darkness, hapa Boston. Stelingi wake ni Mel Gibson na Robert DeNiro.

Ninacheza kama askari polisi wa kike (background). Nitaitwa mara kwa mara kuigiza kwenye background hadi wanapomaliza ku-shuti mwezi Desemba. Nilipatwa na butwaa nilipopigiwa simu wiki mbili zilizoipita na kuambiwa kuwa nimechaguliwa na mwongoza sinema, kuwa askari kanzu wa kike. Na tena si kwa siku moja tu.

Haturuhusiwi kupiga picha kwenye set hii nimepiga mwenyewe Dressing Room. Ninavaa bastola bandia na madude mengine wanaovaa polisi wa Boston.
Mel Gibson mtu poa sana, jana alikuwa anatuchekesha kwenye set, leo alikuja kula lunch kwenye meza tuliyokuwa tunakula. Kaongea vizuri tu na sisi. Tulishangaa kuona mtu "A" list kama yeye anafanya hivyo. Mara nyingi wanaenda kula kwenye trela au hoteli lakini siyo na extras.
Haya nitawapa updates.

Mcheza sinema, Gbenga Akkinabe (The Wire) mwenye asili ya Nigeria anaigiza kwenye hiyo sinema kama mpelelezi. Nimeongea naye kidogo, alisema kuwa ana marafiki wengi kutoka Tanzania huko New York.