Showing posts with label Miss World. Show all posts
Showing posts with label Miss World. Show all posts

Saturday, January 24, 2009

Miss Brazil Afariki Dunia


Mrembo Miss Brazil, Mariana Bridi (20) amefariki dunia leo asubuhi huko Brazili baada ya kuugua ugonjwa wa bacteria usio na tiba. Hivi karibuni alikatwa sehemu ya tumbo na mikono na miguu yake kusudi bacteria usisambae zaidi mwilini mwake. Jitihada za kumwoka hazikufanikiwa. Aliwahi madkatari walidhani ana ugonjwa kwenye njia ya kupitisha mkojo. Bridi aliwahi kushiriki katika mashindano ya urembo wa Miss World. Alikuwa mmoja wa warembo watano bora.
Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.
Kwa habari zaidi someni:

Saturday, December 08, 2007

Warembo wa Afrika 1967

Hao ni warembo wa Afrika, wa mwaka 1967. Hapa wanapiga posi kwenye hoteli huko London tarehe 10, Novemba 1967 kabla ya mashindano ya Miss World.

Kutoka kushoto ni Miss Tanzania (Teresa Shayo), Miss Uganda (Rosemary Salmon), Miss Nigeria (Rosalind Balogun) na Miss Ghana (Araba Vroon). Mamiss weusi wengine kutoka Afrika walikuwa Miss Kenya (Zipporah Mbugua), na Miss Gambia (Janie Jack).

Kuona wote walioshiriki bonyeza hapa: http://www.geocities.com/komw3/MW1967Delegates.html

Picha ilipigwa na Leonard Burt.