Showing posts with label Naibu Katibu Mkuu. Show all posts
Showing posts with label Naibu Katibu Mkuu. Show all posts

Saturday, December 17, 2016

Naibu Katibu Mkuu Mpya wa CCM Akagua Mali za Chama Dodoma

MPOGOLO AKAGUA MALI ZA CHAMA LEO MJINI DODOMA, LUHWAVI AMKABIDHI KILA KITU HADI MSAIDIZI
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, kuhusu jengo la mikutano la CCM, lililopo Kilimani mjini Dodoma wakati Naibu Katibu Mkuu huyo mpya alipotembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kukagua mali za CCM, leo. Kushoto ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya CCM, Innocent Msena na kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki.
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, kuhusu jengo la mikutano la CCM, lililopo Kilimani mjini Dodoma wakati Naibu Katibu Mkuu huyo mpya alipotembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kukagua mali za CCM, leo. kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki.
 Mafara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo ukiwa mbele ya jengo hilo la mikutano la CCM
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, akimoji jambo, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara Rajabu Luhwavi baada ya kukagua jengo hilo, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.
KIWANJA
🔻
 Meneja wa Miliki wa Makao Makuu ya CCM, Abdallah (kulia) Msangi akimpatia maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (wapili kushoto), alipoenda kukagua kiwanja cha CCM kilichopo eneo la Kilimani mjini Dodoma, akiwa katikaziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi.
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki akiongeza maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo alipoenda kukagua kiwanja cha CCM kilichopo eneo la Kilimani mjini Dodoma, akiwa katikaziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, akimuonyesha mwisho wa shamba la CCM, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu huyo alipoenda kukagua kiwanja hicho kilichopo eneo la Kilimani mjini Dodoma, akiwa katikaziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma, leo.

NYUMBA YA CCM YA NAIBU KATIBU MKUU-BARA
🔻
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akiwasili kukagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, mkoani Dodoma, leo
 Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya CCM, Innocent Msena akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, aliyefika kukagua nyumba ya Chama atakayoishi, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uenedeshaji Filbert Mdaki akionyesha sehemu ya jikoni, wakati Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo alipokagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama leo mjini Dodoma. Kushoto ni Luhwavi
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akikagua meza kwenye jiko, alipokuwa akikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma leo. Kulia ni Msaidizi Msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mbwana Kambangwa.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akikagua kabati la jikoni, alipokuwa akikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma leo
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo wakati wakiizunguka kuikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo baada ya kuikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.

KUKAGUA MAGARI WHITE HOUSE
🔻
 Msafara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Rajabu Luhwavi, ukiwa umepumzika kwa mda katika jengo la White House la Makao Makuu ya CCM kabla ya kuanza kazi ya kukagua magari, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo (wapili kushoto), akipatiwa maelezo na Fundi wa magari, Ramadhani Mbelwa (kushoto), kuhusu hali ya magari yaliyoharibika, Mpogolo alipokuwa akikagua magari hayo akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo amhoji jambo Fundi wa magari ya Chama, Ramadhani Mbelwa (kushoto), alipokuwa akikagua magari mabovu ya Chama, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo. Kulia ni Luhwavi.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akionyeshwa gari lililofunguliwa boneti, kupata uthibisho wa gari tatizo la gari, alipokuwa akikagua magari mabovu ya Chama, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimshukuru Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi baada ya kumalizika kazi ya kukagua baadhi ya mali za Chama, mjini Dodoma leo.
KUNZIA SASA HUYU NDIYO BOSS WAKO, SIYO MIMI TENA: Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimtambulisha aliyekuwa Msaidizi wake, Mbwana Kambangwa(kulia), kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo kabla ya kuagana, mwishoni mwa ziara ya Mpogolo kukagua mali za Chama, mjini Dodoma, leo. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

Saturday, November 07, 2015

Rais Magufuli Akutana na Maktibu Wakuu na Manainbu Waziri


 
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Rished Bade na  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Katibu Mkuu Utumishi Mhe HAB Mkwizu  na  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  katika picha ya pamoja Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Wednesday, June 24, 2009

Uteuzi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara kama ifuatavyo kwa lengo la kujaza nafasi zilizokuwa wazi pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi kwenye Wizara kama ifuatavyo:-

1. Bwana ELIAKIM CHACHA MASWI - ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) atakayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kabla ya uteuzi huo, Bwana Maswi alikuwa Kamishna Msaidizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha na Uchumi.

2. Bwana JUMANNE ABDALLAH SAGINI – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI atakayeshughulikia Elimu ya Msingi na Sekondari. Kabla ya uteuzi huu Bwana Sagini alikuwa Mratibu wa Mradi wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

3. Dr. SHAABAN RAMADHANI MWINJAKA – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko. Kabla ya uteuzi huu Dr. Mwinjaka alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Makamu wa Rais.

4. Bi. ELIZABETH JOKTAN NYAMBIBO – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huu Bi. Nyambibo alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.

5. Bwana ULEDI ABBAS MUSSA – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Bwana Mussa alikuwa Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji kwenye Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

6. Dr. PATRICK S. J. J. MAKUNGU – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Kabla ya uteuzi huu Dr. Makungu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa ‘Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology’, Arusha.

Uteuzi huu unaanza tarehe 13 Juni, 2009.

(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU MKUU KIONGOZI

IKULU,
DAR ES SALAAM.

23 JUNI, 2009