Showing posts with label Ng'ombe. Show all posts
Showing posts with label Ng'ombe. Show all posts

Thursday, August 02, 2012

Rais Kikwete Atoa Kifuta Jasho cha Ng'ombe kwa Wananchi wa Monduli

RAIS KIKWETE ATOA KIFUTA JASHO CHA NG'OMBE KWA WANANCHI WA MONDULI

(Picha na Habari Kutoka Ikulu)



 Rais Jakaya Mrisho kikwete akizindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jashp cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009


Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi ng'ombe mmoja wa wakaazi wa Monduli walioathririka na na ukame mwaka 2008/2009 ambapo walipoteza mifugo yao yote. Hafla hii imefanyika leo Monduli. Picha na Ikulu.


SERIKALI itakuwa inagawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha karibu mifugo 800,000 iliyopotea kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

Ahadi hiyo imetolewa leo, Alhamisi, Agosti 2, 2012 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipozindua Mradi wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo kwa waliopotelewa mifugo yote katika Wilaya ya Monduli kwenye sherehe iliyofanyika Makuyuni wilayani humo.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiwemo wakuu wa wilaya na wabunge wa mkoa huo, Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa kundi la kwanza la wananchi ikiwa ni mitamba minne na dume moja la kisasa kwa kaya 16 za mwanzo.

Uzinduzi huo ni wa pili kufanywa na Rais Kikwete chini ya Mradi huo wa kwanza wa aina yake kubuniwa na Serikali katika historia na wenye thamani ya sh. Bilioni 12.9.

Februari 19, mwaka huu, Rais Kikwete alizindua Mradi kama huo katika Wilaya ya Loliondo kwenye sherehe zilizofanyika mjini Loliondo. Kesho Agosti 3, 2012 Rais Kikwete anatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika mji wa Loliondo.

Saturday, May 22, 2010

Mtume!!!

Jamani huo mchezo wa kupambana na ng'ombe dume (bull) huko Hispania una athari zake. Yaani huwezi kuamini lakini huyo jamaa bado yu hai!

Mnaweza kusoma story hapa:

http://www.nypost.com/p/news/international/gored_matador_gets_spain_and_suffering_uKtLPXB9Snnc3d4BRNZPUN

Tuesday, September 30, 2008

Mwanamke ajifanye Ng'ombe na Kukimbiza watu



Ukisikia vituko basi ongeza na hii! Huyo mama, Michelle Allen, wa Middletown Ohio, kajifanya ng'ombe. Nasema kajifanya lakini inaelekea alidhania ni ng'ombe kabisa.

Alikimbiza watoto huko kwao na hata kukojoa kwenye baraza la nyumba ya jirani yake!
Mara akaingia barabarani na kusabisha magari yasimame. Si ajabu walikuwa wanamshangaa.
Polisi wanasema walipomkamata alikuwa ananuka pombe.

Alifikishwa mahakamani leo asubuhi hivyo hivyo kama alivyo pichani.
Kwa habari zaidi someni:

Friday, February 01, 2008