Showing posts with label One Game. Show all posts
Showing posts with label One Game. Show all posts

Monday, October 05, 2009

IBUA Film Star Awards - Tanzania


WACHEZA FILAMU CHIPUKIZI KUSAKWA TANZANIA

Mchakato wa kutafuta na kuibuwa vipaji vya waigizaji chipukizi linaanza rasmi na litahusisha mikoa ya Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Zanzibar na Dar es Salaam.
Uibuaji na ukuzaji wa vipaji vya wasanii chipukizi wa filamu ambao hawajawahi kushiriki katika filamu au tamthilia yoyote itawahusisha watanzania wenye vigezo vya kuwa na umri wa miaka 16 na kuendelea, awe na akili timamu, awe ni raia wa Tanzania na ajue kusoma na kuandika.
Mchakato utahusisha kufanya usaili katika mikoa husika hadi watakapopatikana kumi bora ambapo washiriki watachuana kumtafuta msanii chipukizi wa filamu Tanzania.
Mwaka huu kampuni mbali mbali zimejitokeza kudhamini mashindano haya lakini yatatajwa hapo baadaye
Mshindi wa IBUA Film Star Tanzania atajinyakulia zawadi ambayo itatangazwa baadae na pia atapata mkataba wa kushiriki filamu mbali mbali za wasanii wa ndani na nje ya nchi.
Mshindi atapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi kupitia kipindi maalumu kitakachoonyeshwa hapo baadae.
Fomu za kushiriki shindano la IBUA Film Stars Tanzania zinapatikana mikoa husika kama ifuatavyo Arusha (Club Silk), Mwanza (Salma Cone), Mbeya (CPMTL Stationery mkabala na ofisi ya mkuu wa mkoa), Dodoma (Zunny Ice Cream Parlour), Zanzibar (Ofisi za Zenj FM), Dar es Salaam (TCC Chang’ombe, Shear Illusions mlimani City, Royal Salon Sinza, Zizzou Fashions). Fomu zitaanza kupatikana tarehe 10 Oktoba 2009.
Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30 Oktoba 2009 kabla ya kuanza usaili mjini Arusha tarehe 31 Oktoba na 01 Novemba.
Zoezi la usaili litafanyika kabla ya wananchi kupata nafasi ya kutoa maoni na kufanikisha kuwapata washindi.

Jacqueline Wolper
Afisa Uhusiano-YEC PRODUCTION

Thursday, May 22, 2008

Majina Yatajwa - tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania

Press Release Kutoka One Game:

Habari yako ndugu yangu...
Kwa kifupi kinyang'anyiro cha Tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania kinakaribia kufika ukingoni, ambapo leo majaji wametangaza rasmi majina ya waigizaji na filamu zilizoingia katika hatua ya mwisho.
Majina yalitolewa katika ukumbi wa mgahawa wa Hadees Fast Food!
Asante sana kwa ushirikiano wako wa awali!
Tupo pamoja!


****************************************************************
TUZO ZA VINARA WA FILAMU TANZANIA (TANZANIA FILM VINARA AWARDS) 2007 – 2008

Muigizaji Chipukizi wa Kike (Up coming actress)
1. Irene James – Miss Bongo II
2. Irene Uwoya – Diversion Of Love
3. Fatuma Makame – Karibu Paradiso
4. Jennifer Mwaipaja – Silent Killer
5. Grace Michael – Malipo ya Usaliti

Muigizaji Mwandamizi wa Kike (Best Actress in a Supporting Role)
1. Irene Uwoya - Diversion Of Love
2. Mama Frank – Yolanda
3. Irene James – Miss Bongo II
4. Susan Lewis – Behind the Scene
5. Tecla Mjata – Macho Mekundu

Muigizaji Bora wa Kike (Best Actress)
1. Lucy Komba - Diversion Of Love
2. Grace Michael – Malipo ya Usaliti
3. Halima Yahya – The Stranger
4. Elizabeth Chijumba – Copy
5. Riyama Ally – Fungu la Kukosa

Muongozaji Bora wa Filamu (Best Film Director)

1. Gervas Kasiga – Fake Pastors
2. Jimmy Mponda – Misukosuko II
3. Kulwa Kikumba – Macho Mekundu
4. Haji Adam – The Stranger
5. Halfan Ahmed – Copy

Mtunza Sauti Bora (Best Soundman of The Year)
1. Adam Wazir – Fungu la Kukosa
2. Cleophance Ng’atingwa – Kolelo
3. David Sagala – Copy
4. Camillius Kanuli – Fake Pastors
5. Swalehe Juma – Fungu la Kukosa

Mpiga picha Bora wa Filamu ( Best Cameraperson of The Year)
1. Mbalikwe Kasekwa – Misukosuko II
2. Sylon Malalo – Kolelo
3. Rashid Mrutu – Copy
4. Nicholaus Mtengwa – Kilio moyoni
5. Sylon Malalo – Simu ya Kifo

Adui Bora wa Filamu (Best Film Villain)
1. Mohamed Aziz – The Body Guard
2. Irene Uwoya - Diversion Of Love
3. Sebastian Mwanangulo – Misukosuko II
4. Ahmed Ulotu – Silent Killer
5. Elizabeth Chijumba – Copy

Mhariri Bora wa Filamu (Best Film Editor)
1. Moses Mwanyilu – Misukosuko II
2. John Kalage – Miss Bongo I
3. Rashid Mrutu – Copy
4. Hassan Mbangwe – Malipo ya Usaliti
5. Sylon Malalo – Kolelo

Mwandishi Bora wa Filamu (Best Script Writer)

1. Seleman Mkangara – Malipo ya Usaliti
2. Hammie Rajab – Kolelo
3. Kulwa Kikumba - Diversion Of Love
4. Lucy Komba – Utata
5. Elizabeth Chijumba – Copy

Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kiume (Best Actor in a Supporting Role)
1. Aliko Tshmwala – Segito
2. Single Mtambalike – The Stranger
3. Adam Kuambiana – Fake Pastors
4. Halfan Ahmed – Copy
5. Emmanuel Muyamba – Fake Pastors

Muigizaji Chipukizi Bora wa Kiume (Best New And Upcoming Actor)
1. Emmanuel Muyamba – Fake Pastors
2. Laurent Anthony – Karibu Paradiso
3. Hassan Nguleni – Body Guard
4. Yussuf Mlela - Diversion Of Love
5. Uswege – Malipo ya Usaliti

Muigizaji Bora wa Kiume (Best Actor)

1. Single Mtambalike – Agano la Urithi
2. Nurdin Mohamed – Utata
3. Jacob Steven – Copy
4. Haji Adam – Miss Bongo
5. Yussuf Mlela - Diversion Of Love


Mapambo na Maleba Bora (Best Costume And Makeup of The Year)
1. Misukosuko II
2. Macho Mekundu
3. Kolelo
4. Utata
5. Copy

Mtunzi Bora wa Filamu (Best Creater of The Year)
1. Lucy Komba – Utata
2. Nicholaus Mtitu - Diversion Of Love
3. Single Mtambalike – The Stranger
4. Halfan Ahmed – Copy
5. Hammie Rajab – Kolelo

Filamu Bora ya Mwaka (Best Movie of The Year)
1. Behind the Scene
2. The Stranger
3. Diversion Of Love
4. Macho Mekundu
5. Misukosuko II
6. Simu ya Kifo
7. Copy
8. My Sister
9. Silent Killer
10. Miss Bongo I
11. Agano la Urithi
12. Malipo ya Usaliti
13. Utata
14. Kilio Moyoni (Crying Silently)
15. Fake Pastors

Saturday, May 10, 2008

Mchuano ni mkali Tuzo za Vinara!


ONE GAME PRESS RELEASE:

Na Mwandishi Wetu

Ikiwa ni wiki moja tangu jopo la majaji lianze kazi ya kuzipitia filamu zilizowasilishwa na watayarishaji wa filamu nchini ili kuwania tuzo za filamu za Vinara (Vinara Film Award), imeelezwa kuwa kumekuwa na mchuano mkali miongoni mwa filamu hizo.

Taarifa hiyo iliyotolewa na mratibu wa tuzo hizo zinazotolewa na One Game Promotion, Khadija Khalili (pichani), imetanabaisha kwamba mchuano huo umetokana na sehemu kubwa ya filamu hizo kuwa na kiwango cha juu cha ubora.

"Kazi ya kupitia filamu zilizowasilishwa inaendelea vizuri, hivyo tuna imani kuwa kazi itamalizika kwa wakati uliopangwa... Isitoshe, mchuano umekuwa mkali sana tofauti na tulivyodhani, filamu na wasanii vinakabana koo kwa viwango vya ubora," akasema.

Akaeleza, jopo hilo lilimtumia taarifa ya maendeleo ya kazi hiyo iliyoonesha mchuano kuwa mkali miongoni mwa filamu zilizowasilishwa kuwania tuzo hizo zitakazotolewa kwa mara ya kwanza nchini, huku kazi hiyo ikiendelea vizuri.

Aidha, majaji hao wanatarajiwa kumaliza kazi hiyo Mei 17 mwaka huu na kutoa fursa ya kutangazwa majina matano kwa tuzo zipatazo kumi na tisa zitakazowaniwa huku tuzo ya heshima ikipangwa kutolewa kwa msanii aliyetoa mchango mkubwa katika sanaa hiyo. ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Ndovu Special Malt ikishirikiana na Shirika la


Onesho la utolewaji wa tuzo hizo litakalofanyika Mei 30 mwaka huu, limedhaminiwa na KampuniUtangazaji la Taifa (TBC) na Global Publishers.


Wiki chache zilizopita, mratibu huyo alisema kuwa, zaidi ya filamu sabini za Kitanzania zimewasilishwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo hizo kwa mwaka wa 2007/08.

Wednesday, May 07, 2008

Tanzania Breweries yapongezwa - Tuzo za Vinara

PRESS RELEASE kutoka ONE GAME:

TBL yapongezwa kudhamini tuzo za Vinara!

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya bia Tanzania (TBL) hivi karibuni ilimwagiwa sifa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kutokana na kutoa kipaumbele katika kusaidia sekta ya sanaa nchini ikiwa ni pamoja na kudhamini tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania (Vinara Film Award).

Pongezi hizo kwa kampuni hiyo zilitolewa na mmoja wa maofisa wa Baraza hilo Omari Mayanga katika hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja ya majaji wa tuzo hizo iliyofanyika hotelini hapo Jumamosi iliyopita.

Ofisa huyo alisema kuwa, kwa kipindi kirefu kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kufadhili na kudhamini shughuli za sanaa nchini jambo alilosema kuwa limekuwa likichangia sana kujinua sekta ya sanaa nchini ambayo kwa sasa imekuwa ni sehemu ya ajira kwa sehemu kubwa ya vijana.

"Kwa niaba ya Basata, nawapongeza sana hawa TBL kwa kuwa siku zote wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika shughuli za sanaa... Kama hivyo wamedhamini tuzo za muziki na sasa wamedhamini tena tuzo za filamu, siyo kung'ang'ania mpira tu kama makampuni mengine," akasema.

Aidha, ofisa huyo alizitaka kampuni nyingine kuiga mfano wa TBL kujitokeza katika kufadhili au kudhamini shughuli za sanaa nchini hasa kutokana na kuwa sehemu ya ajira kwa kundi kubwa la vijana kwa sasa.

Kampuni hiyo ya bia imejitokeza kudhamini tuzo hizo kupitia bia yake ya Ndovu Special Malt ikishirikiana na kampuni za Global Publishers na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).
Kwa mujibu wa mratibu wa tuzo hizo zinazotolewa na One Game Promotions, Khadija Khalili, baada ya semina hiyo majaji hao walianza kazi ya kuzipitia filamu zilizoingizwa kuwania tuzo hizo, kazi watakayoifanya kwa kipindi cha wiki mbili kabla ya kuibuka na majina ya waliofanikiwa kuingia katika hatua ya mwisho.

"Kazi imeanza kwa kasi na kwa uhakika, muda si mrefu nimetoka kuongea na mwenyekiti wa jopo la majaji ameniambia kuwa kazi inaendelea vizuri, hivyo wana imani kubwa ya kuimaliza kazi hiyo kwa wakati muafaka," akasema.

Siku chache zilizopita, Khalili alisema kuwa, zaidi ya filamu sabini zimeingizwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo hizo.

Saturday, May 03, 2008

Tuzo za Vinara wa Filamu

Press Release kutoka One Game:

Majaji tuzo za Vinara kuanza kazi leo!

Na Mwandishi Wetu

Jopo la majaji wa Tuzo za Vinara wa filamu nchini (Vinara Film Award) leo Jumamosi ya Mei 3, 2008 linatarajiwa kuanza rasmi kazi ya kuziangalia filamu za Kitanzania zinazowania tuzo hizo kabla ya kuzitolea maamuzi.

Mratibu wa One Game Promotion inayoaandaa utolewaji wa tuzo hizo, Khadija Khalili amesema kuwa, majaji hao watatanguliwa na semina ya siku moja kabla ya kuanza zoezi la kuziangalia filamu hizo chini ya usimamizi wa maafisa wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Jopo hilo linaloundwa na wataalamu wa mambo ya filamu nchini wanakutana leo katika hoteli ya Regency ya Mikocheni jijini Dar es Salaam na kuendelea na kazi hiyo kwa siku kadhaa kabla ya kuibuka na majina ya filamu na wasanii walioingia katika makundi ya kuwania tuzo hizo.

"Kikubwa ni kwamba jopo la majaji linategemea kukutana Jumamosi ya Mei 3 (leo) katika hoteli ya Regency Mikocheni kwa ajili ya semina na kuanza kazi ya kuzipitia filamu zilizowasilishwa kwa ajili ya kuwania tuzo za Vinara," alisema Khalili.

Vipengele vinavyoangaliwa ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Muongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu na Mtunzi Bora wa Filamu.

Vingine ni Filamu Bora ya Kutisha, Muigizaji Mwandamizi Bora wa kike), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kiume, Adui Bora kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu ambao wote watapata tuzo. Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa mchango wao kukuza sanaa nchini.

Wiki iliyopita, Khalili alisema kuwa, zaidi ya filamu sabini zimeingizwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo hizo.

Filamu zinazowania tuzo hizo ni zile zilizokamilika kutengenezwa Januari 2007 mpaka Machi 31, 2008.

Tuzo hizo zitakazotolewa Mei 30, zimedhaminiwa na Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia ya Ndovu Special Malt, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Global Publishers.