Showing posts with label Ramadhani. Show all posts
Showing posts with label Ramadhani. Show all posts

Saturday, June 28, 2014

Salamu za Ramadhani Kutoka Sec. of State John Kerry

 
U.S. Secretary of State, John Kerry

Secretary of State John Kerry on Ramadan Kareem

Press Statement

John Kerry
Secretary of State
Washington, DC
June 27, 2014




As the holy month of Ramadan begins, I wish the millions of Muslims here at home and so many more all around the world Ramadan Kareem.

Ramadan is a time for peaceful reflection and prayer, a time for acts of compassion and charity -- universal values and aspiration ingrained in every human heart.

Across the globe, Muslims will assemble and celebrate a rich tradition with fasting and prayer, as generations have done every year since the time of the Prophet Muhammad. Here in America, Muslims will commemorate Ramadan in ways that reflect the great diversity of our country and the spirit of community that binds us together.

The diversity and patriotism of America’s religious communities are sources of strength for all of us, and our freedom to worship is a powerful reminder of the traditions we share. E Pluribus Unum – From Many, One. And from many faiths, we stand together in one shared country.\

Along with many of our Ambassadors all over the world, I will host an Iftar celebration at the State Department in Washington, DC. This event will bring together leaders from across the Muslim community to join together and reflect on our shared values.

On behalf of the U.S. Department of State, I wish all Muslims around the world a peaceful Ramadan and joyful month.

Friday, August 02, 2013

Rais Kikwete Afuturu na Wasanii wa Bongo Fleva Ikulu


PICHA KWA HISANI YYA IKULU
 


 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Filamu na  Bongofleva,Hemed Suleiman.



 Rais Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,TV,Mbwiga Mbwiguke.





 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii Mkongwe wa Bongofleva,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crazy G K.



 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa bongofleva na muigizaji wa Filamu hapa nchini,atambulikae kwa jina la kisanii Zuwena Mohamed a.k.a. Shilole.






Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii wa Bongofleva,Ally Kiba na mdogo wake Abdull Kiba.


 


Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongofleva mara baada ya kufturu.Kutoka kushoto,Snura,Keisha,Mwasiti,aliyechuchumaa ni Shilole,Dj Fetty ,Mwanahawa Abdul a.k.a Quee Doreen.





 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya pichani shoto Mwasiti Almas na kulia Zuwena Mohamed
a.k.a Shilole wakiwa sambamba na Mtangazaji wa Clouds FM,Dj Fetty wakipakua
ftari kufuatia mualiko wa Rais Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu,jijini Dar jana.






 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a

Bongofleva wakipata ftari kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar jana kufuatia

mualiko wa Rais Kikwete.


 Rais Kikwete akisalimiana na msanii wa bongofleva,Lawrence Malima a.k.a Marlow, kulia
kwake ni Ally Kiba pamoja na Abdul Kiba na kushoto ni Mtangazaji wa East Africa
Radio, Samisango



 Rais Kikwete akisalimiana na msanii wamuziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda na kulia kwake ni msanii wa bongofleva,Cassim Mganga,wakati wa kupata ftari jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar.






 Rais Kikwete akiwasabahi baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya,mara baada ya
kupata ftari mapema jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar, Rais Kikwete
aliwaalika wasanii mbalimbali kupata ftari ya pamoja Ikulu jana jioni.

Tuesday, July 16, 2013

Rais Kikwete Afuturu na Watoto Yatima Ikulu leo Jioni

Picha na Maelezo Kwa hisani ya Ikulu




Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasabahi baadhi ya watoto yatima walioshiriki katika futari aliyoiandaa ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watoto yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam walihudhuria futari hiyo.








Baadhi ya watoto yatima wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.

 PICHA NA IKULU

Tuesday, July 09, 2013

Ramadhan Karim


RAMADHAN‬ KARIM
Uzuri wa Ramadhani si tambi kwa iliki
     bali ni kusoma Qur-an kwa wingi.
Wala si uji kwa ndizi
bali ni kumuomba MOLA atuhifadhi.
Tena si chapati kwa mchuzi
bali ni kuacha yote ya kipuuzi.
Na wala si juisi kwa sambusa za nyama
bali ni kuomba istighfar kwa Maulana.
Pia wala si daku la wali wa nazi kwa jodari
bali ni tahajudi kwa wingi.

"MOLA ATUWAFIKISHE KUUDIRIKI MWEZI WA
RAMADHANI NA KUPATA FADHILA ZAKE".

Monday, July 30, 2012

Rais Kikwete Afutarisha Mkoani Lindi


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Magharibi na waumini wengine wa Mkoa wa Lindi aliowakaribisha katika futari Ikulu ndogo ya Mkoani Lindi leo Julai 30, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru waalikwa kwa kuhudhuria katika hafla ya futari aliyoandaa

Tuesday, July 24, 2012

Nawatakia Ramadhani Njema!

Nawatakia wadau waislamu wote Ramadhani Njema!

Monday, August 15, 2011

Madiwani Wafuturu Ikulu na Rais

Picha za Mh. Rais Kikwete na Mama Salma na madiwani wa Dar katika futari Jumamosi jioni Ikulu. Zimeletwa na Kaka Michuzi.












Wednesday, August 11, 2010

Nawatakia Ramadhani Njema!


Nawatakia wadau waIslamu mwezi mtukufu wa Ramadhani Njema! Nilipita Roxbury, Boston leo jioni na kuona WaIslamu wakienda kuswali mskiti mkuu wa New England. Nilifurahi sana kuona wengi wakielekea huko.
**************************************************************
Ramadan Begins Today, Muslims Start the Month of Fasting


By Hassan El-Najjar

Ramadan Mubarak!

Today, Wednesday, is the first day of the Islamic month of Ramadan (Ramadhan), of the year 1431 Hijriya, corresponding to August 11, 2010.

Adult Muslims all over the world start fasting this month as required by their religion. They abstain from eating, drinking, smoking, and having sexual activity from dawn to the sunset.

Fasting is the fourth way of worshipping God after the proclamation of faith, performing prayers, giving the poor tax (alms or charity), and followed by the pilgrimage, Haj.

For more information about Ramadan fasting, see the following articles:

Saturday, September 19, 2009

Iddi Mbaraka!

Nawatakia wadau waIslamu, Iddi Njema!

Monday, August 31, 2009

Ramadhani Njema Kutoka Jamii Forums


JamiiForums.com The Home of Great Thinkers inapotimiza miaka 3 tangu kuanzishwa kwake, inapenda kuwatakia watanzania wote pamoja na wadau wote mitandaoni mfungo mwema na kuwatakia kila lililo jema katika mwezi huu.

"Enyi Mlioamini! Funga ya Ramadhani imefaradhishwa kwenu kama ilivyokafaradhishwa kwa wale waliokuwa kabla yenu ili mpate TAQWA"(QURAAN Surah Al-Baqarah 2:183)Unakaribishwa kwa mijadala huru ili ushiriki na wazalendo wenzako. Tembelea www.JamiiForums.com
JF Management

Saturday, August 22, 2009

Ramadhani Karim!

Ninawatakia wadau WaIslamu wote Mfungo Mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Rais Obama Atuma Salamu za Ramadhani



Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umefika. Rais wa Marekani, Barack Obama amewatumia waislamu wote salamu. Nadhani ni mara ya kwanza kwa rais wa Marekani kutuma salamu za Ramadhani kwa waislamu nchini Marekani na duniani pote. Nampongeza Rais Obama kwa ushujaa wake wa kutoogopa maneno ya wazungu wasioelewa kuwa dunia imebadilika.

Tuesday, September 02, 2008

Mwezi Mtukufu wa Ramadhan

Nasiha 40 Za Ramadhan

http://www.alhidaaya.com/

Zitekeleze Ufaidike na Mwezi Mtukufu

1. Anza kwa kuzingatia mwezi huu mtukufu uwe wa kujihesabu, kutenda amali nyingi na kujirekebisha hali yako na uhusiano wako na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) uwe bora zaidi:

2. Kumbuka kwamba huu mwezi ni mgeni ambaye amekutembelea kisha ataondoka, hivyo mpokee mgeni wako na mkirimu kwa mazuri yote anayostahiki.

3. Tahadhari na kutokufunga bila ya sababu au udhuru wowote, kwani kufanya hivyo, Swawm yako haitolipika hata ukifunga mwaka mzima.

4. Swali kwa wakati wake, usiache Swalah ikakupita. Na jua kuwa ukiwa huswali Ramadhaan huna Swawm kwa mujibu wa fatw za Maulamaa wengi.

5. Soma sana Qur-aan kadiri uwezavyo kwani ni mwezi ulioteremshwa Qur-aan. Kamilisha msahafu mzima japo mara moja, ukishindwa basi hata nusu yake, robo yake.

6. Zidisha ibada za Sunnah, kama Sunnah zilizo Muakkadah (zilizosisitizwa) na zile Ghayri Muakkadah (zisizosisitizwa). Tazama ratiba katika kiungo kifuatacho: Ratiba Ya Swalah Za Sunnah Zilizosisitizwa Na Zisizosisitizwa

7. Chukua fursa kuomba du'aa sana kila mara nyakati za kukubaliwa du'aa, khaswa ukiwa bado katika Swawm. Tumia wakati wa baina ya adhana na iqaamah kuomba du'aa na haja zako kwani ni wakati wa kukubaliwa du'aa. Vile vile nyakati za thuluthi ya mwisho ya usiku.

8. Iborishe Swalah yako kwa kuiswali ipasavyo na kuzidisha khushuu (unyenyekevu).

9. Usiache kuswali Taarawiyh pamoja na jama‘ah, usiondoke hadi Imaam amalize upate thawabu za Qiyaamul-Layl.

10. Tahadhari na kufanya israaf ya mali, chakula na neema nyinginezo, kwani israaf ni mbaya na itakuondoshea neema ulizojaaliwa.

11. Tumia wakati wako vizuri na zingatia kwamba umri wako unazidi kupunguka.

12. Mwezi huu ni wa ibada na sio kula, kulala na kufanya ya upuuzi.

13. Zoesha ulimi wako uwe umerutubika kwa kumtaja Mola wako, usiwe miongoni mwa wasiomkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ila kidogo tu.

14. Chukua fursa kufanya da‘awah. Amrisha mema na kataza maovu, kwani yule unayemuongoza atakapotekeleza mema, utazibeba nawe thawabu zake pia. Tuma ujumbe wa dini kwa wenzako. Chapisha idadi nyingi ya makala zenye mafunzo ya dini, chapisha du'aa ugawe misikitini, vyuoni, majumbani. Unaweza kupata makala na du'aa mbali mbali katika
www.alhidaya.com

Pia kama una uwezo zaidi rekodi mawaidha yaliyomo ndani ya tovuti na wagawie wenzako upate ujira zaidi. Gawa bure na usiuze, kwani si ya kuuzwa.

15. Fanya kila aina ya wema uwezavyo, patanisha waliokhasimiana, msaidie mwenye haja na muokoe mwenye shida.

16. Wakumbuke wazazi, ndugu, jamaa na marafiki katika du'aa zako kwani kuwaombea wao bila ya wao kujua Malaika hukuombea na wewe vile vile.

17. Wasiliana na ndugu, jamaa kwani ni jambo lililosisitizwa sana na lenye kukuongeza umri, kheri na baraka nyingi. Walio mbali na wewe wasiliana nao kwa simu.

18. Unapohisi njaa, wafikirie masikini wasio na uwezo wa kula, na utambue kuwa uko katika neema ya Mola wako.

19. Muombe msamaha uliyemdhulumu kabla hajalipwa mema yako.

20. Mfuturishe aliyefunga upate thawabu zake juu ya thawabu zako.

21. Omba maghfirah na msamaha kwa Mola wako, kwani tambua kwamba Yeye ni Mwingi wa Msamaha na Mwingi wa Rahma.

22. Ikiwa umetenda maasi kisha Akakusitiri Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), tambua kuwa hiyo ni onyo utubie na weka azma kutokurudia tena.

23. Ongeza elimu ya dini yako kwa kujifunza tafsiyr ya Qur-aan, Hadiyth, Fiqhi n.k. upate kuongeza taqwa.

24. Sikiiza mawaidha japo moja kwa siku kwani kusikiliza kunaleta taathira kubwa ya kuongeza Iymaan na Ucha Mungu.

25. Jiepushe na marafiki waovu na vikao vyao na ungamana na marafiki wema na vikao vya kheri.

26. Usipoteze muda wako kutazama televisheni vipindi visivyokupa faida na dini yako, bali tumia wakati wako kwa yatakayokuongezea elimu na ucha Mungu.

27. Usiharibu Swawm yako kwa kunena ya upuuzi, au Ghiybah (kusengenya), au kubishana au kupandisha sauti. Jizuie unapokuwa na hamaki.

28. Fika msikitini mapema zaidi, kwani hivyo ni dalili ya hamu na mapenzi ya ibada na kuwa karibu na Mola wako.

29. Waamrishe na kuwafunza mema ya dini yao walio katika majukumu yako; mke, mume, watoto, ndugu, jamaa n.k. kwani wako karibu yako zaidi na kukutii.

30. Usijaze tumbo sana katika suhuur (daku) kwani itakufanya uwe mvivu na ushindwe kukaa macho nyakati za asubuhi na mchana na ushindwe kufanya ibada vizuri na kusoma sana Qur-aan.

31. Usijaze tumbo sana katika iftwaar (kufuturu) kwani itakushinda kusimama Qiyaamul-Layl au kuzingatia Aayah za Qur-aan zinaposomwa na Imaam.

32. Punguza kwenda madukani/sokoni khaswa kumi la mwisho kwani utakosa kheri na thawabu nyingi zilizomo katika masiku hayo ya thamani kubwa.

33. Tilia hima kubwa kuswali Qiyaamul-Layl kumi la mwisho upate Laylatul-Qadr, usiku ambao ibada yake ni bora kuliko miezi elfu.

34. Jitahidi ufanye I'tikaaf msikitini katika kumi la mwisho japo siku chache, upate fadhila zake na uchume mema mengi pamoja na kupata Laylatul-Qadr.

35. Tambua kwamba siku ya 'Iyd ni siku ya kumshukuru Mola wako na sio siku ya kutenda yale uliyojizuia ya maovu katika Ramadhaan.

36. Siku ya 'Iyd , wafanyie wema wazazi, watembelee ndugu, jamaa na marafiki kuboresha uhusiano wako nao.

37. Usiache kutoa Zakatul-Fitwr - wakumbuke maskini, yatima na wanaohitaji na wasaidie na kuwagawia chochote wabakie katika furaha.

38. Tamka Takbiyrah siku ya 'Iyd kwa sauti unapokwenda msikitini ili kuwakumbusha wengine wanaokwenda au kufuatana nawe ili nawe waweze kupiga Takbiyrah hizo.

39. Weka azma baada ya Ramadhaan kujiendeleza katika hali ya ibada uliyokuwa nayo katika Ramadhaan, ukifanya hivyo itakuwa ni dalili ya kukubaliwa Swawm yako.

40. Funga Sita Shawwaal upate thawabu za Swawm ya mwaka mzima.

Wednesday, June 18, 2008

Shughuli Washington D.C. Jumamosi 6-21-08

Taarifa ya shughuli Washington DC Jumamosi

Jumuia ya waislam wa Washington D.C inawaalika watu wote kwenye hitma ya pamoja siku ya jumamosi hii Juni 21, 2008 saa tisa jioni. Tunanatarajia kuwa na hitma ya kuwarehemu marehemu na kuongelea mambo na mipango ya kufanya wakati wa mfungo mtukufu wa Ramadhani hapa D.C

Anuani ni:
North four corners local park,
211 south wood avenue,
silver spring, md, 20901.

Wote mnakaribishwa kutakuwa na soda kwa wingi, juisi nyama choma na mapochopocho ya kila aina. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na:

IDDY SANDALY -3016135165,
MGANGA MUHOMBOLAJE -2023740988,
SALEH LONDA -2402738871,
MAYOR MLIMA-3018068467
ZAINAB (ZAINA) BUZOHERA-2404132359, ASHURA (BONTO)-2404217017,
NURU MWAMENDE-2406039364.

Thursday, September 13, 2007

Ramadhani Njema


Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umefika. Nawatakia waislamu wote Ramadhani Njema.

********************************************************************************
Nimepata salamu hizi za Ramadhani kwe e-mail:

Asalaam alaiykum,

Mimi ni RAMADHANI, Nilimpa ujumbe Rajab akuletee, Nikamtuma na Shaaban akuambie kuwa nipo njiani.

NAKUJA na mke wangu SWAUMU na watoto wetu watatu: 1.Rhma, 2.Maghufira, na3.Tauba. Pia sijamuacha rafiki yangu wa damu QURAAN, na ndugu yake QIYAMU LAIL.

Sitokaa nawe kwa muda mrefu, nitakua nawe kwa mwezi mmoja tu, ukisha tutaondoka kumpisha, EID -EL-FITRI na hatimae Sitat – Shawwal, ambao watawasili kwa kupishana.
Utupokee kwa mapenzi yako yote, na ututunze kwa kipindi hiki kifupi kwani tukiagana huna uhakika wa kutuona tena mwakani.

RAMADHANI MUBARAK !!

“Enyi Mlioamini! Funga ya Ramadhani imefaradhishwa kwenu kama ilivyokafaradhishwa kwa wale waliokuwa kabla yenu ili mpate tauba” (QURAAN Surah Al-Baqarah 2:183) (Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumchamungu)

Nakutakia maandalizi ya funga njema ya mwezi mtukufu wa Ramadhan…shahar tauwba..

M.M. Juma