Showing posts with label Rep. Joe Wilson. Show all posts
Showing posts with label Rep. Joe Wilson. Show all posts

Wednesday, September 16, 2009

Rais Obama Anavyotukanwa Hapa Marekani!



Yaani lazima nikubaliane kabisa na Rais mstaafu Jimmy Carter, aliyesema leo kuwa watu wanamfanyia Rais Obama vituko na kutomwonyesha heshima kama Rais.

Mfano, wiki iliyopita Rais Obama alikuwa anatoa hotuba bungeni. Aliposema kuwa katika 'mpango wake wa afya' wasio na makaratasi hawatapewa huduma, mzungu Joe Wilson, alifoka, 'You Lie!" (Mwongo). Wilson alizomewa.

Katika historia ya Marekani hakuna rais aliyewahi kuzomewa akiwa anatoa hotuba Bungeni. Huwa watu wankunja uso na kuguna, lakini kufoka hivyo ilikuw haijawahi kutokea. Watu wanasema Rais Obama angekuwa mzungu, Wilison asingethubutu kufanya hivyo.

Rais Carter anasema hiyo mizozo na fujo tunazaoona kwenye mikutano ya wananchi (Town Hall) ni kutokana na wazungu kushindwa kukubali kuongzwa na mtu mweusi. Hawawezi kutukana Rais Obama waziwazi hivyo wanafanya fujo. Hata kuleta bastola kwenye mikutano anayohotobia Rais Obama.

Niliwaambia ubaguzi bado uko Marekani. Watu walibisha....mnaona sasa?