Showing posts with label Salvatory Rweyemamu. Show all posts
Showing posts with label Salvatory Rweyemamu. Show all posts

Saturday, May 17, 2014

Private Brian Salvatory Rweyemamu Azikwa Leo Mjini Dar es Salaam

 Private Brian Salvatory Rweyemamu -JWTZ  (1987-2014) amezikwa leo mjini Dar es Salaam katika makaburi ya Kinondoni. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

The Late  Private Brian Rweyemamu 1987-2014


Picha kwa hisani ya Ikulu:





Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Bw. Salva Rweyemamu na mkewe Isabella wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wao Private Brian Salva Rweyemamu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014




Dada wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu wakiweka shada la maua wakati wa mazishi katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salva Kikwete wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Private Brian Salva Rweyemamuwakati wa mazishi  katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014

Thursday, May 15, 2014

Tanzia - Private Brian Salvatory Rweyemamu (JWTZ)




 
Private Brian Salvatory Rweyemamu JWTZ (19? - 2014)

Bwana Salvatory Rweyemamu wa Kinondoni Dar es Salaam, anasikitika kutangaza kifo cha mtoto wake mpendwa Private Brian Salvarory Rweyemamu aliyefariki alfajiri ya kuamkia leo tarehe 15 Mei, 2014 katika hospitali ya Jeshi Lugalo alipolkuwa akitibiwa.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Bwana Salvatory Rweyemamu Kinondoni jirani na Vijana (Mango Garden).

Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki walioko Dar es Salaam, Kagera, Malawi, Afrika Kusini, Uingereza na Canada.

*************************************** 
Asante Kaka Michuzi kwa Taarifa.
Poleni sana familia ya Rweyemamu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.