Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

Saturday, October 29, 2016

Taarifa Kutoka CCM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Ndugu Christopher Ole Sendeka, Msemaji wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa akizungumza kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo tarehe 28/10/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

Ndugu wanahabari,

Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari zinazolenga kukejeli, kudhihaki, kukatisha tamaa, kubeza na kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake katika kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Kumekuwepo na makala zinazoandikwa na magazeti mawili ya nje ambazo hutolewa kila baada ya miezi miwili na ambazo zinapotosha na kuandika habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania.

Pia, yapo magazeti mawili ya ndani ambayo yamekuwa yakitoa makala mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kumchafua Mheshimiwa Rais na kuichafua taswira ya nchi yetu.

Tumesikitishwa na waandishi wa makala hizo walioamua kujivua uzalendo na kushiriki mpango wa kuiharibu heshima na taswira ya nchi yetu kwa maslahi ya maadui zetu wa nje na baadhi ya wanasiasa. Tunafuatilia kujua nini kinawasukuma kufanya hivyo na kwa maslahi ya nani ilhali sote ni Watanzania. Je ni tamaa ya madaraka tu au mengine? Hakuna anayepinga ukosoaji bali unapaswa uwe ukosoaji wenye nia njema kwa nchi.

Ndugu wanahabari,
Mtakumbuka hivi karibuni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufisadi ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari aliyoiita ya tathmini ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Katika taarifa yake hiyo, alidai kuwa alileta msisimko mpya katika siasa za Tanzania, kwamba ameshirikiana na wenzake kuionyesha nchi yetu maana ya demokrasia na kukosoa juhudi za serikali na wateule wa Rais.

Demokrasia kimsingi ni dhana inayohusisha ushiriki na kuheshimu mawazo ya wengi katika kufikia uamuzi. Ikiwa maana halisi ni hii, tunajiuliza ni ipi demokrasia aliyoionyesha Lowassa ambayo leo anajisifu kuwa nayo?
-          Tulishuhudia akiwa mgombea urais wa chama ambacho hakijui, hakushiriki kukijenga wala kutoa mchango wowote unaompa hadhi ya kupeperusha bendera huku katiba na kanuni ya chama hicho  ikivunjwa.  Kidemokrasia, anayepewa fursa ya kupeperusha bendera ya chama chochote makini duniani ni kiongozi au mwanachama aliyethibitika kwa imani na matendo, kuzielewa, kuzitekeleza, kuzitetea falsafa, itikadi na malengo ya msingi ya chama hicho. Mgombea ni taswira halisi na alama muhimu inayoakisi dhamira ya chama husika machoni kwa wananchi.

-          Demokrasia ya kweli lazima ianzie ndani ya chama, ni demokrasia ipi iliyotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea, kuvigharamia na walivyovitumikia kwa kuamua kumteua mgombea “MTUNGUO” (ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania). Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kilidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia.

-          CHADEMA watuambie njia iliyotumika kuwapata wabunge wa viti maalumu. Ni demokrasia gani inayotoa fursa kwa baadhi tu ya viongozi  kuteua wabunge ambao wanakiwakilisha chama chote. Ambapo kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA walikosa watu wanaowafahamu na kuamua kuwateua wanawake maswahiba wao ndani ya CCM. Msingi wa kawaida wa kupata wabunge wa viti maalum ukiacha kura za maoni, kigezo kingine muhimu ni mchango wa mgombea/mwanachama huyo katika kukijenga na kukitumikia chama chake. Yaliyotokea kwa CHADEMA kwenye wabunge wake wa viti maalum ni mapya kwenye ulimwengu wa demokrasia. Inahitaji wataalamu wa sayansi ya siasa kufanya utafiti wa aina hii mpya ya demokrasia.
Tulidhani baada ya mwaka mmoja kupita, wenzetu hawa wangelikuwa wamejifanyia tathmini, kujikosoa, kujisahihisha na hata kufanya uungwana wa kuwaomba radhi wanachama wao kwa uvunjifu mkubwa wa misingi ya demokrasia, katiba na kanuni za vyama vyao.

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutochukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko, yasiwe ni nyimbo za kuburudisha au kutoa matumaini hewa kwa wanachama na wananchi. Kanuni mojawapo ya demokrasia ndani ya vyama ni lazima ionekane katika muundo wake na katika utekelezaji wa muundo huo.

Umefika wakati vyama vya siasa vinapaswa kujifunza kuuza sera ili kujijenga na sio kusubiri matukio kwa ajili ya kupata huruma ya wananchi. Tunasubiri kushuhudia na kusikia demokrasia itakavyoendeshwa katika uchaguzi wa ndani wa vyama hivyo ambapo kuna taarifa mmoja wa vigogo amefanikiwa kupata kiasi cha dola milioni 15 zitakazomsaidia kupanga safu yake ya uongozi.

Katika kutimiza mpango huo, tayari yapo mawasiliano ya mara kwa mara ya baadhi ya viongozi wakitoka Zanzibar na sehemu zingine za nchi kuja Dar es Salaam, na imeonekana dhahiri mazungumzo yao kutowashirikisha viongozi wenzao waandamizi kwani yanalenga kufanikisha mpango huo.

Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli, ameendela kufanya juhudi kubwa katika kuijenga nchi kwa kuimarisha utendaji na nidhamu ya utumishi serikalini, kukusanya mapato na kusimamia matumizi sahihi ya fedha, kupambana na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na kusimamia haki, usawa na wajibu kwa raia. Mwenzetu anayaona haya kuwa ni kuufanya utumishi wa umma kaa la moto.

Juhudi hizi na nyinginezo ikiwemo ununuzi wa ndege mpya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, afya kwa kununua vitanda vya wazazi, kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari  na nyinginezo hazipaswi kukatishwa tamaa kwa maslahi ya wachache, ni vyema kuziunga mkono kwa maslahi ya taifa letu.

Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Rais Dk. Magufuli madarakani, CCM inawaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono katika dhamira yake safi ya kuwaondolea kero, kuboresha huduma za jamii na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na;-
                                                CHRISTOPHER OLE SENDEKA
MJUMBE WA NEC NA MSEMAJI WA CCM
28/10/2016.

Saturday, June 18, 2016

Dk. John Pombe Magufuli Kukabidhiwa Uenyekiti wa CCM Julai 23

SAFARI YA DK. MAGUFULI KUKABIDHIWA UENYEKITI CCM YAIVA, MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM KUFANYIKA JULAI 23, 2016
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, Kikao hicho kimejadii na kupitisha kuwa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utafanyika Julai 23, 2016, ambapo mkutano huo unatarajiwa kumchagua Rais Dk. John Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya Taifa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, Kikao hicho kimejadii na kupitisha kuwa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utafanyika Julai 23, 2016, ambapo mkutano huo unatarajiwa kumchagua Rais Dk. John Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya Taifa. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Hii ndiyo taarifa rasmi kama ilivyotolewa na Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, baada ya Kikao hicho cha Kamati Kuu ya CCM, kilichofanyika leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Picha zote na Bashir Nkoromo, Kwa picha nyingine kem kem za kikao hicho>BOFYA HAPA

Sunday, December 06, 2015

Balozi Wilson Masilingi Aanza Ziara ya Kutembelea Vyama Vya Siasa DMV

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi leo Jumamosi Desemba 5, 2015 alihudhuria mkutano wa Halmashauri ya CCM tawi la DMV ikiwa ni moja ya ziara zake anazotarajiwa kuzifanya kutembelea matawi ya vyama vya siasa nchiMarekani yenye lengo la kudumisha mshikamano na ushirikiano wa Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao.

Akiongea kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV Mhe. Wilson Masilingi amesema lengo kuu ni kuwa karibu na vyama vya siasa kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano ndani ya Jumuiya za Watanzania nchini Marekani na pia kuvitambua kama sehemu na sura ya Diaspora na kutoa wito kwa Watanzania waishio Marekani kuelekeza nguvu katika kuwekeza nyumbani bila kujali ufuasi wa chama unachoamini au kushabikia, wote ni Watanzania.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliiomba Halmashauri hiyo ya CCM DMV kusaidia katika maendeleo ya Tanzania kwa kupanua wigo wao pamoja na kwamba lengo lao ni siasa na siasa ni sehemu ya maisha ya jamii na maendeleo ya jamii yanategemea siasa, kwa hiyo basi mnaposikia kuna muwekezaji yupo tayari kuwekeza Tanzania msisite Ubalozi upo wazi na utafanya kila liwezekanalo kuhakikisha muwekezaji huyo hapati vikwazo vyovyote.

Mwisho Balozi Wilson Masilingi aliwashukuru Watanzania kwa kuwa mabalozi wazuri nchini Marekani na kuwaasa kuishi kwa kufuata misingi na sheria za nchi ya Marekani.

 Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea jambo na mwenyekiti wa tawi CCM DMV Bwn. George Sebo kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 mkutano uliofanyika Hampton Inn, College Park, Maryland. Picha na Kwanza Production/Vijimambo Blog
Mkutano ulianza kwa sala na kuwakumbuka wote waliotangulia mbele ya haki.

Mwenyekiti tawi la CCM DMV Bwn. George Sebo akifungua kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College Park, Maryland.

Sunday, September 13, 2015

Gharika ya Watu yashuhudia Uzinduzi Rasmi wa Kampeni za CCM

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja kwa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
Sehemu ya gharika ya watu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Sehemu ya gharika ya watu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Ndege ndogo ikipita juu ya  Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasili katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
  Rais Kikwete akimlaki Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasili katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Gharika ya watu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 gharika ya watu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Mama akisaidiwa kwenda kupata huduma ya kwanza baada ya kuhemewa na gharika ya watu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
Nyomi  ya watu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015

Utenzi ukisomwa  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Sehemu ya gharika ya watu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
  Sehemu ya gharika ya watu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
  Sehemu ya gharika ya watu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Kikwete, mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana wakiwa na furaha katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
  Rais Kikwete, mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana wakiwa na furaha katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Kada mashuhuri wa CCM Visiwani Zanzibar Mzee Borafia akiongea katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Umati ukishangilia katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 CCM OYEEEEEE....anasema kada huyu katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Kikwete akimpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Mohamed Gharib Bilali baada ya kuhutubia katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume  akihutubia kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
Viongozi wakiwa jukwaa kuu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Wanahabari wakirekodi tukio hilo la kihistoria kw kila aina ya vifaa vya kisasa ikiwemo drone ya kupigia picha kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Msanii Diamond na kundi lake la Wasafi wakitumbuiza kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
  Msanii Diamond na kundi lake la Wasafi wakitumbuiza kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai akisoma ratiba ya mkutano   kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubia umati kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiwa amehemewa kwa gharika ya watu  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Rais Kikwete akihutubia kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Rais Kikwete akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Rais Kikwete akifafanua jambo wakati akihutubia kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Diamond na kundi lake wakitumbuiza  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Jukwaa kuu likifurahia onesho la Diamon na kundi lake  wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Rais Kikwete akirejea tena mbele kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dkt Ali Mohamed Shein  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
Rais Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana wakijiandaa kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dkt Ali Mohamed Shein  kwenye Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015.
 Msaada unatolewa kwa mama aliyepoteza fahamu  kutokana na wingi wa wananchi wakati wa mkutano huo
 Nyomi mkutanoni hapo
  Rais Kikwete na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein wakionesha Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia gharika hiyo ya watu katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Sehemu ya wananchi, wanaCCM  na viongozi uwanjani hapo
 Dua ikisomwa  baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Kikwete na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa Rais Kikwete wakipongezana kwa   furaha baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Gharika ya watu ikiondoka kwa furaha na amani baada ya mkutano uliofana wa uzinduzi wa  kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Kikwete akiaga wakati akiondoka Unguja kurejea Dar es salaam  baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Kikwete akiaga wakati akiondoka Unguja kurejea Dar es salaam  baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Kikwete akimnyakua mtoto wakati  akiondoka baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Kikwete akimbeba  mtoto huyo  baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
  Rais Kikwete akipata picha na watoto  baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
  Rais Kikwete akiaga baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Kikwete akiagana kwa furaha na wananchi  baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Kikwete akiagana kwa furaha na wananchi  baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
  Rais Kikwete akiaga wakati akiondoka Unguja kurejea Dar es salaam  baada ya  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
 Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akiagana na viongozi wa CCM wa Visiwani wakati akiondoka Unguja kurejea Dar es salaam  baada ya kuunguruma katika  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015
"....CCM JUU!" anasema Rais Mstaafu Benjamin Mkapa wakati akipanda ndege kuondoka baada ya kuhudhuria kuunguruma katika  uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015. PICHA NA IKULU