Star Jones kabla hajapunguza uzito na baada ya kupunguza
Arusi ya Star Jones na Al Reynolds 2004
Star Jones na Al Reynolds wakiwa kwenye Honeymoon
Star Jones na Al Reynolds baada ya Star kupunguza uzito
BEFORE AND AFTERHaya leo nimekuwa umbea. Nimesikia habari kuwa Star Jones na mume wake Al Reynolds wanaachana. Kwa kweli mambo ya kuachana ni mambo ya kawaida hapa Marekani, lakini hii imekuwa habari kubwa.
Kama mnakumbuka walivyofunga ndoa ilikuwa habari kubwa kweli. Yaani Star Jones wakati huo alikuwa ni moja wa wanawake wa ile show, THE VIEW. Alikuwa anapendwa kweli na watazamaji.. Watu walivyosikia anaolewa kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 42 walifurahi kweli ingawa walisema huyo mume wake anacheza upande mwingine (anapenda wanaume wenzake). Sasa baada ya kutangaza ndoa, alikuwa anatangaza details mpaka chupi atakayovaa mpaka watu wakaona kinyaa.
Mara baada ya kuolewa kwake alianza kupungua uzito, kawa mbaya wengine walisema kawa kama kinyago, halafu alitolewa kwenye THE VIEW. Alikataa kusema alipunguza uzito kwa njia gani. Kumbe alifanyiwa opresheni ya kupunguza tumbo. Watu walimchukia kwa vile alificha siri yake kwa miaka mitatu.

Sasa wanaachana. Nikitazama picha za Star kabla hajaolewa na sasa namwona mtu mwingine na alivyo sasa.
Hivi ni kwa nini mara nyingi watu wakifunga ndoa ya kifahari ndoa haidumu? Utakuwa watu walifunga ndoa simple lakini zinadumu miaka na miaka na wanapendana hasa.
Wadau mnasemaje?
Kwa habari zaidi someni: