Showing posts with label Swimming Pool. Show all posts
Showing posts with label Swimming Pool. Show all posts

Saturday, December 14, 2013

Mimi Katika Sinema American Hustle

Mcheza sinama wa Hollywood, Amy Adams akionyesha nguo yake ya kuogogelea ya kuvutia. Mimi niko nyuma yake.
Wadau, sinema America Hustle inatoka wiki hii. Kama utaenda kuiona hebu tazama hiyo scene inayotokea kwenye party kwenye nyumba ya matajiri enye bwawa ya kuogelea. Mimi niko katika scene hiyo tena nimevaa nguo ya kuogelea. Tulipiga hiyo scene mwezi wa pili kukiwa na theluji na barafu nje!

Waigizaji wenzangu wa hapa Boston tumefurahi sana maana wengi tumepata nafasi kuwa katika hiyo sinema, na wengine hata kubahatika kupata nafai ya kuongea.  Kweli waigizaji wa Boston tunapiga htaua.

Wednesday, March 27, 2013

Picha Kutoka Seti ya Sinema Hapa Boston

Wadau, wiki iliyopita nilishiriki katiika sinema inayopigwa hapa Boston. Kwa sasa haina jina lakini mwongoji ana Oscars kadhaa. Siwezi kuwaambia mengi mpaka sinema itoke.  Nguo niliyovaa iko chini ya koti. Na nilivaa wigi enye nywele ndefu.  Lakini sidhani kama nitaonekana, kama nitabahatika kutoka utaniona natongozana na jamaa chuma kweli!

Wednesday, August 20, 2008

Jamaa akifaidi Swimming Pool

Nimeletewa hii picha kwa e-mail. Mnaionaje?