Showing posts with label The Surrogates. Show all posts
Showing posts with label The Surrogates. Show all posts

Friday, March 13, 2009

Surrogate


Unaweza kutengeneza Surrogate hapa: http://chooseyoursurrogate.com/

Monday, June 16, 2008

Seti la - The Surrogates huko Taunton, MA

Extras wakingojea kuitwa kwenye set. Kabla ya kwenda tulipanga foleni na kukaguliwa costume/nguo zetu na mwongoza sinema, Jonathan Mostow. Ilinikumbusha enzi za Tabora Girls, na JKT. Kama nywele nguo au viatu havikumfaa unatolewa na kupelekwa wardrobe/make-up. Hatukuruhusiwa kuvaa make-up. Kulikuwa na watu wenye makrimu za kufuta make-up kwenye uso za watu ukikamatwa umevaa. Pia ukionekana msafi, mtu alikuwa anapita na kutupaka make-up ya uchafu. Moja wa majengo kwenye set.

Moja wa kondoo waliotumika kwenye shoot.
Huyo nguruwe naye ni mwigizaji.


Wazazi wa watoto waliokuwa extra waliangalia shoot. Ona nyaya za umeme. Ilibidi watumie magenerata kwa vile hakuna umeme hapo.



Hao kuku nao ni waigizaji! ASPCA (Chama cha Kulind ahaki za wanyama) walikuwepo kuhakikisha usalama wa wanyama wote kwenye seti.




Siku hiyo kulikuwa na extras 300! Hapa tumemaliza siku na tunangojea check-out....kupata receipts zetu.



Wadau, kwanza samahani kwa kuchelewa kuposti hii habari ya seti. Nilikuwa na matatizo ya komputya.


Hii ni costume niliyovaa siku ya kwanza kwenye set ya The Surrogates. Nilikuwa mpita njia na nilimpita Bruce Willis kama mara kumi na tano. Alikuwa anatembea na kushangaa mji wetu wa Dreads. Siku ya pili sikupiga picha ndo ilikuwa scene ya kuchoma moto maiti.

Kibao kinatueleza sehemu ya kusubiri mpaka kuitwa kwenda kwenye seti. Kampuni ambayo inatengeneza hii sinema ni Walt Disney. Walikodi mabasi ya kutupeleka huko, na haikuwa mbali.

Seti enyewe ilikuwa Paul Devers School, ambayo zamani ilikuwa shule maalum kwa ajili ya watoto wenye magonjwa ya akili. Kuna majengo kibao. Ni kama ghost town, maana majengo yote ni abandoned. Walituweka nje kwenye mahema, kwa vile walisema majengo hayako salama kwa vile zina asbestos ndani.

Thursday, June 12, 2008

Sinema - The Surrogates

Huyo farasi naye yumo kwenye sinema
Kwa mbali unaweza kuona maiti (mdoli) juu ya vijiti maalum kabla ya kuchomwa. Nilikuwa kwenye basi nilivyopiga hii picha. Crew walikuwa kwenye mapumziko. Haturuhusiwi kupiga picha kwenye seti. Kwa mbali unaweza kuona makaburi feki.

Wadau, samahani kwa ukimya. Nilikuwa Taunton, MA kwenye shooting ya sinema, The Surrogates. Stelingi wake ni Bruce Willis na Ving Rhames. Mimi niliigiza mle kama Dread yaani binadamu wasiopenda Usurrogate. Ilikuwa poa sana, nilimpita Bruce Willia mara kadhaa kama mpita njia. Kumwona kwa karibu ni mrefu, mwembamba. Ving Rhames si mrefu kama nilivyotegemea lakini ni kibonge. Alicheza kama nabii wa Dreads.

Leo tuliangalia maiti inachomwa. Lakini haikuwa maiti ilukwa mdoli. Lakini ukiona utasema ni mtu huyo. Nakuambia kuna wataalamu wa special effects. Mdoli alichomwa kama wahindi wanavyochoma moto maiti. Walikuwa na zimamoto wa Taunton Fire Department pale kuzima baada ya wao kumaliza kuipiga picha. Nakuambia mdoli alitengenezwa kifundi kiasi kwamba walivyosima moto tuliona fuvu na mifupa!

Nadhani The Surrogates itakuwa sinema kubwa ya summer 2009.

Friday, June 06, 2008

Sinema - The Surrogates


Wadau, mnakumbuka mwezi wa tatu niliitwa kwenye audition ya sinema, The Surrogates, ambayo stelingi wake ni Bruce Willis. Bahati mbaya sikupata role niliyofanyia audition, ila wiki ijayo wananichukua kwa siku mbili kucheza kama Dread. Nitakuwa mchafu mchafu na nitavaa nguo zilizochakaa hasa. Jana nilienda kwenye fitting ya costume, nilichukia kweli kuonekana kama ombaomba, lakini ndo hivyo tena. Sinema hiyo. Nitawapa updates wiki ijayo.
Hadithi ya The Surrogates inatokea mwaka 2054. Watu wanaishi maisha yao kupitia Surrogates robots ambazo wanafanana na binadamu lakini ni warembo na wazuri. Inatokea wimbi la kuliwa kwa maSurrogates na Bruce Willis ndiye anatafuta ni akina nani wako nyuma ya njama hiyo. Hao Dreads ni watu ambao wanataka kuishi kama binadamu.

Wednesday, March 12, 2008

Audition yangu leo


Leo nimefanya audition kwa ajili ya sinema mpya, The Surrogates. Stelingi wake ni Bruce Willis. Hadithi yake ni ya Science Fiction.

Role niliofanyia audition ni mama moja mwenye hasira ambaye anamwua character wa Bruce Willis kwa kumpiga risasi kichwani. Ila siye mwenyewe ni kloni yake.
Ilibidi nifanye 'pantomine', yaani kuigiza bila kifaa. Sasa waliniambia nijifanye nimeshika bunduki na naifyatua baada ya kusema line. Hapo ilibidi nikumbuke mazeozi ya SAR (semi-automatic rifle) ya enzi za JKT.
Ilikuwa audition safi sana kwa vile niliambiwa kuchangaya action na maneno. Haya sisi actors tunaambiwa ukifanya audition tegemea hapo ndo mwisho, ukiitwa tena ni bahati wakikuchagua ni kama kushinda bahati nasibu! Haya tuone mambo yatakavyokuwa.

Ila nilifurahi sana kuona waigizaji wengi weusi waliitwa kufanya audition.

Kwa habari zaidi ya sinema, The Surrogates bofya HAPA: