
Jamani, leo nimejua ubaguzi bado upo nchi hii. Wesley Snipes amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwenye gereza la serikali (federal). Kisa hakulipa kodi aliyostahili kulipa! Denzel Washington alikuwa mahakamani akitoa shuhuda kuhusu jinsi Snipes alivyo mtu mwema. Pia Woody Harrelson alitoa shuhuda. Snipes mwenyewe alimwomba hakimu amwonee huruma! Lakini wapi! Jaji kampa kifungo cha juu kabisa miaka mitatu. Alisema awe mfano kwa wengine!
Ninaamini angekuwa mzungu kama Tom Hanks au Tom Cruise angepewa probation, au kifungo cha siku chache au miezi michache.
Marekani lazime ulipe kodi. Kama hulipi utakamatwa tu. Kama si leo basi hata baada ya miaka!
Wadau mnasemaje?
Kwa habari zaidi someni:


