

Mcheza tennis maarufu, Venus Williams, ameshinda taji la Wimbledon tena kwa kumtwanga mdogo wake Serena Williams.
Ni mara ya tatu kwa ndugu hao kugombania taji maarufu ya Wimbledon wakiwa katika top two (washindani wakuu). Na ni mara ya tano kwa Venus kushinda taji la Wimbledon. Serena ameshinda taji hiyo mara mbili.
Tulivyokuwa tunatazama mechi ilielekea kuwa Serena atashinda, lakini Venus alirudi kwa nguvu na kumshinda mdogo.


