Thursday, August 24, 2006

Kajambanani?

Kila siku asubuhi nikiamka nafungua TV kuangalia taarifa ya habari kwenye Fox 25. Kuna mzungu mwanaume mnene ndo anchor wa Beacon Hill studio (Dowtown Boston) na anapendwa na wengi, anaitwa VB. Na huko kwneye studio yao Dedham kunakuwa na akina Dada Anquenette (mweusi), Gene Levanchy na Kim Carrigan. Leo nikafungua na nikasikia sauti ya ajabu. VB kajamba tena kwa sauti. Nikajiuliza kama VB kaweka microphone matakoni kusudi tumsikie. Nikasema sijui kala nini jioni yake. Kwanza nikamwonea huruma maana najua hawezi kuamka kukimbia chooni mpaka break ikaja. Bora yuko nje maana studio utajaa harufu ya mishuzi. Basi kila baada ya sekunde chache anaachia. Nikasema huyo mzungu kala maharagwe na hajayazoea nini! Cha kushangaza kawa anaongea bila kujali kitu.

Kukaa kidogo huko kwenye studio kuu, anchor Gene Levanchy naye kajamba. Kim Carrigan kamtazama kwa dharau kubwa na kushika pua lake. Gene na VB wakamwuliza kama yeye hajambi na kawa kama kasirika kuuliza hivyo. Kim kajifanya hayumo kwenye mambo ya kujamba. Basi kwenye break aliamka kwenye kiti halafu tukasikia mjambo pwaaaach. Tukasikia kila mtu studio anacheka. Kumbe wenzake walimwekea ‘Whoopee cushion’ (Kimpira kinachotoa mlio kama mtu kajamba). Ukikalia inatoa mlio kama vila mtu kajamba. Kima katoka haraka uso mwekendu!

Basi ndo VB kaelezea kisa cha yeye kuwa anajamba jamba. Kumbe kwenye magazeti waliandika habari ya intern huko White House kusema kuwa rais Bush anapenda kujamba ofisini. Heh! Rais mzima anjamba! Tena mbele za watu. Lakini kwa nini watu washangae, ni bindamu na vayakula anavyopenda ni vya kiMexico ma nacho, refried beans, na maburrito na bia. Lazima zitafanya tumbo ijae gesi. Sijui kama yuko na Rais mgeni kutoka nchi nyingine anaachia mishuzi. Tumekwisha jua kuwa anapataga ashki.

Haya sasa fikiria uko kwenye basi au subway (treni). Watu wanajamba huko hasa kama umejaa, tena vile vya kimya kimya vya kuniuka hasa! Bora hizo zenye milio mikubwa. Cha kuchekesha mtu anabanwa gesi, anaachia kimya kimya inanuka halafu watu wanalalamika na huyo aliyetoa analamika. Huwezi kujua nani kajamba.

Wazungu wengine hawana haya, wanajamba, halafu wanasema, “Oh Excuse me” Utajibu kweli? Kama unamjua labda utasema, “You’re excused”. Wamarekeni weui wana usemi, “You smelt it, you dealt it!” (Umesikia ushuzi hivyo wewe ndo umejamba), Ukiwa na weusi ni bora kunyamaza na ubane pua.

Na hapa Marekani watu wanatajirika kwa kuuza vidonge vya kuzuia watu kujamba. Phazyme, Beano, Papaya pills, vina soko kubwa.

Kabla sijamaliza lazima nikumbuke Bongo na usafiri wa treni Third Class Bongo (Central Line). Watu walikuwa wanabanana safari ndefu, watu wana jamba jamba, na huwezi kuwalaumu maana choo hakuingiliki na inabidi usubiri mpaka treni isimame kwenye kituo halafu ushuke haraka na kujisaidia pembeni. Basi Thedi ikapewa jina, KAJAMBANANI! Unasafiri daraja gani, Nasafiri, KAJAMBANANI bwana hela sina ya First!

Lakini baada ya maajabu niliyoona leo nangojea kusikia kama kutakuwa na Official Fart Day! Siku ya kujamba. Kumbe kujamba ni sifa, wazungu bwana!

4 comments:

  1. Du hiyo yapaka kuuachia wazi kwenye TV ni kali.Lakini ukifikiria sana lazima kuona aibu kujamba ni utamaduni tuliofuzwa.Nazani zamani za enzi watu walikuwa wanaachia tu.Angalia watoto huwa wanaachia tu halafu tunawafunza kuwa kuona aibu

    ReplyDelete
  2. Ninachokifurahia sana kwenye blogu yako ni habari za filamu! Napenda kusikia kuhusu filamu popote duniani-hongera kwa hili.

    ReplyDelete
  3. Dada Chemi Che Mponda umeniacha hoi na habari hii ya ushuzi kwenye TV mbavu sina. Leo ni mara yangu ya kwanza kuona blog yako unafurahisha sana dada. Hivi wewe ni mtoto wa yule mzee wa chama gani sijuwi cha siasa? nilikuwa nasoma article zako daily news zamaniiii sana.
    ni mimi wako:- edwardmkwelele@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  4. Haya jamani, Dada Chemi kawapa habari za kujamba na mimi nawaletea picha za vijambio...

    Pitieni: http://mikundu.blogspot.com/

    ReplyDelete