Monday, May 21, 2007

Misuko





Kuna wakati wanawake waafrika walipenda nywele zao walizozaliwa nazo, yaani nywele za kipilipili. Walikuwa wanazisuka kwa mitindo mbalmbali na kuzipamba na vitu kama 'rafia'.

Jamani, mnakumbuka yale mabunda ya rafia yalikuwa yanauzwa bei ya juu pale Kariakoo na hata kuuzwa kwa magendo baada ya 'Miezi 18' kile kipindi baada ya vita vya Kagera. Na ilikuwa mtu akisuka nayao basi ndo anaonekana mtu wa maana. Siku hizi ni weave! Zamani Tanzania walikuwa wanaita wigi, 'nywele ya maiti'. Sasa zinauzwa kila kona.

Kulikuwa na klabu/ saluni maalum za kusuka nywele. UWT (Umoja wa Wanawake Tanzania) nao walikuwa na sehemu zao za kusuka nywele.

Nakumbuka nilivyokuwa nasoma Zanaki, mwanafunzi mwenzangu Margaret Makame, alinisuka mtindo wa mistari, lakini iliyogeuzwa (mfano hapo juu). Walimu walikuja juu, eti nimesuka kizungu! Duh, siku hizi si kitu cha kushangaa.

5 comments:

  1. We chemi chemiponda mbona "controversial" sana? Unajifanya kuzifagilia nywele halisi za kiafrika wakati wewe mwenyewe una nywele za marehemu plastiki. Au ndo yaleyale ya waafrika, "fuateni ninachosema siyo ninachotenda"? Usitake kujipa umaarufu usiostaili na kama huna mpya basi kaa kimya. Wewe mtu papai halafu unajifanya nazi.

    ReplyDelete
  2. Anonymous wa 10:00am ndo maana nilisema zamani. Siku hizi mambo yamebadilika.

    ReplyDelete
  3. Huyo anonymous wa 10:00am ndo yule mshamba anayesoma heading tu. Hebu soma full story ndo utoe comment.

    ReplyDelete
  4. anonymous wa 10:00 mi naona wewe ndio mshamba. inakuwaje kumkamia mwenzako namna hiyo? mbona ameeleza vizuri katika story yake. hata zile picha zinaonesha za zamani. wewe ukienda kanisani au msikitini fuata mahubiri yanasemaje la kama utataka ushindane na vitendi vya mhubiri utakuwa umekosea hapo.

    ReplyDelete
  5. Samahanini jamani, mimi naheshimu sana blog ya dada chemi na nisingependa kuichafua, ila naomba special parmissino kwanza toka kwa dada yangu chemi ili nimtukane huyo anony wa saa 10:00 ameniboa kishenzi, hivi katokea wapi kwanza mbona dizaini zake mkulima mkulima hivi, halafu iko kama anahasira na kila mtu, kakulupuka tu kutukana watu hata hawajui, mshenzi sana we dada/kaka kweli, da chemi samahan kwa matusi nnahasira kishenzi, siku njema.

    ReplyDelete