Monday, May 21, 2007

Sinema ya Arusi ya Mariamu


Umewahi kuona sinema iitwayo, ‘Arusi ya Mariamu’? Sinema hiyo ilitengenezwa 1985 nchini Tanzania na Ron Mulvihill na marehemu Nangayoma Ng’oge.

Sinema hiyo ni fupi, dakika 36. Lakini ni hadithi tamu sana. Mariamu (Amadina Lihamba) ana funga ndoa na Sekondo (Godwin Kaduma). Wanapendana sana, lakini Mariamu anaanza kuugua ugonjwa ambao madaktari wanashindwa kumtibu. Sekondo anashauriwa ampeleke kwa mganga wa kienyeji atiibiwe. Huko inakuwa balaa maana kumbe Mariamu ana waoga wa waganga wa kienyeji. Kwani alishuhudia kifo cha baba yake ambaye naye alikuwa mganga wa kienyeji. Alifariki akikusanya mitishamba kwa ajili ya kutibu wagonjwa. Je, Mariamu atapona?

Sinema hiyo inapatikana http://www.grisgrisfilms.com/html/marriage_of_mariamu.html
Ron Mulvihill alirudi Tanzania 1994 kutengeneza sinema ya Maangamizi the Ancient One.

3 comments:

  1. da Chemi habari a Mpakanjia umeiondosha?

    ReplyDelete
  2. Hapana cheki Archives au bonyeza April upande wa kushoto. Huwa stories zinahamia archives nikibandika blog mpya.

    ReplyDelete
  3. nani kakwambia hizo ni simena, hayo ni maigizo tu

    ReplyDelete