Wednesday, October 17, 2007

Concert ya Rose Muhando Dallas, Texas



Kanisa la wa Tanzania na watu wote wanaotumia lugha ya kiswahili wanapenda kuwatangazia wadau wote wa blog hii popote walipo kwamba yule mwanamzuki machachari wa nyimbo za injili kutoka nyumbani Tanzania Dada ROSE MUHANDO atakuwa na onyesho kabambe katika kanisa hilo.

Onyesho hili la aina yake litaanza saa kumi kamili jioni siku ya jumapili tarehe 21.10.2007. Dada ROSE MUHANDO ni muimbaji aliyetokea kupendwa ndani na nje ya Tanzania, uimbaji wake wa nguvu na hisia kali unavutia watu wengi.

Rose Muhando ameshashinda tuzo mbali mbali za uimbaji.
Kwa wale watakaopenda waandaliwe malazi tunaomba wawasiliane nasi kupitia:
Email: umojachurch@yahoo.com,
Simu: 214 554 7381,
682 552 6402,
au 214 341 7287.
Kanda zote za Rose zitauzwa moja kwa moja kutoka ukumbini.
Kanisa lako ulipendalo la Umoja.

ANWANI NI:

Trinity Hillcrest Church

12727 Hillcrest Road • Dallas, TX 75230

9 comments:

  1. Hongereni wote mliofanikisha ziara ya dada Rose US. Mungu awabariki

    ReplyDelete
  2. i wish angekuja pia London, huyu ni mfano!!Mungu ambariki sana!!

    ReplyDelete
  3. Dada Chemi, una habari kama Dada Rose atafika Boston au New York?

    ReplyDelete
  4. MIMI BINAFSI SIKUFAGILII ROSE,WHY? KWA SABABU KIPAJI UNACHO LAKAINI UMEONA KUIMBA KITANZANIA HAKAUFAI HIVYO UMEAMUA KUIMBA KIAFRIKA YA KUSINI ,KUIMBA KI KWELA KWELA TANZANIA TUNASIKITISHA SAANA HIVI KWELI NI LINI TUTAACHA KU-EMBARACE STAILI ZA KISANAA ZA MATAIFA MENGINE ?
    NI KWA NINI TUNAONA FAHARI KAMA WAJINGA VILE KUIGA STAILI ZA MATAIFA MENGINE?

    YAANI MUZIKI WA DANSI WA KITANZANIA NDIO KABISA IT'S TUMBLED,SHATTERED AND HIT THE ROCK BOTTOM! YAANI HUKO KILA BENDI NI KUIGA UKONGO TUU NA ETI TULIVYO WAJINGA TUNAJIVUNIA HICHO NA KUWAPROMOTI HAO WANAMUZIKI! KWELI INATIA KINYAAA PERIOD!

    HAYA NILIFIKIRI MUZIKI WA GOSPEL HUKO NI SALAMA .DOH1 KILA MTU SASA KUANZIA KWAYA YA KUJITONYAMA MPAKA ROSE MHANDO YAANI NI STAILI YA KIKONGO (MASEBENE) MPAKA KWAITO AU KIZULU
    .HII NI AIBU TENA CHA KUSHANAGAZA BENDI INAYOJARIBU KUIGA KWA BIDIII KAMA ROSE MHANDO AU TWANGA PPT NDIO SISI WAPENZI TUNAZIONA NDIO BAB KUBWA
    HIVI AM I THE ONLY ONE HERE!
    SOMETHING HAS TERRIBLY GONE WRONG KATIKA KAZI ZA SANAA ZA MUZIKI WA TANZANIA IWE NI GOSPEL AU HATA MUZIKI WA KIDUNIA

    JAMANI TUPENDE UTANZANIA WETU HAO TUNAWAIGA KWA SAUTI (MARIAM MAKEBA ) AU KOFI OLOMIDE NK WAO MABONA HAWATAKI KUIGA CHETU ? AND WHY?
    ROSE MHANDO I RECOGNISE THAT YOU ARE TALENTED, THA'S UNDISPUTABLE.BUT THE TRUTH IS YOU NEED TO UTILISE YOUR TALENT TO CREATE AND PROMOTE YOUR OWN CREATIVITY ,A MEAN IMBA KITANZANIA UMASHUHURI WAKO WA KUIGA SAUTI ZA KIKWELA KWELA ZA AFRIKA YA KUSINI NA BACKING YA VYOMBO YA KIKONGO UTAVUMA LEO TUU TENA BILA HESHMA YA KISANII NA KESHO HISTORIA INAHAUNT SANA TUU NA HISTORIA YA KISANII SHALL SLAP YOU ON THE FACE
    HIVI NDIO KUSEMA HAIWEZEKANI KABISA KUIMBA AU KUPIGA MUZIKI KITANZNIA?

    ReplyDelete
  5. Nilikuwa nampenda sana Rose lakini nipokuja kugundua wimbo wa moyo wangu amebadilisha lugha tu kutoka kwa wimbo wa rebecca malope ndio hapo taratiibu hamu ikaanza kunitoka.Nikaja kugundua nyimbo nyingine nyingi kaiga ndio maana album ya kitim tim haikuwa nzuri kama ya mwanzo kwa sababu nyimbo za kuiga zilikuwa chache na halisia hazikuwa kazi nzuri makini. Kweli kuiga kunaudhi sana Rose sauti anayo sijawahi kusikia mtz mwenye sauti kama yake.tumwombee aitumie kwa ufasaha. hivi haya maoni huwa wenyewe wanayaona lakini wajirekebishe???

    ReplyDelete
  6. Shukurani kwa ujumbe kuhusu Dada Rose Muhando. Amemaliza Texas, sasa wiki hii Oct 27-28, atakuwa Maranatha Fellowship Church, Peoria IL, karibu na Chicago. More Info: Pastor Edwin (309) 673-6736

    ReplyDelete
  7. Sisi huku nyumbani TZ tunapenda kujua ziara ya dada Rose imekuwaje. je watu wamefurahia nyimbo zake? Je ujumbe wake umefika?. Tupatieni taarifa juu ya ziara hiyo ilivyokweenda

    ReplyDelete
  8. Rose Mhando Bwana Akubariki

    ReplyDelete
  9. Dada Rose Mhando apunguze kuiga 'beats' za Dark.. City Sisters wa Africa Kusini!!

    ReplyDelete