Kuna sinema aina ya Documentary, itatoka hivi karibuni kuhusu ile meli maarufu ya ziwa Tanganyika, M.V. Liemba. Hiyo meli bado ni imara na inaendelea kufanya kazi japo ina miaka karibu 100!
Kwa habari zaidi na kuona clip nenda: http://www.liemba.org/
Wataalamu wa vyombo vya majini wanafahamu tofauti.Ni S.S.Liemba na si M.V.Liemba
ReplyDeleteLiemba ilipoundwa ilitumia injini ya mvuke na hivyo kuwa na jina lilionza na ss yaani steam ship. Baada ya kufanyiwa ukarafati na kuwekewa injini ya mafuta ilacha kutumia kianzio cha ss na kuwa mv yaani motor vehicle. Hivyo kwa sasa ni sahihi ni M.V Liemba na si S.S Liemba
ReplyDeleteKweli, huo mwanzo wa jina kwa vifupisho s.s. ulibadilishwa na kuwa m.v. baada ya ukarafati. Na m.v. ni "motor vessel" na siyo "motor vehicle".
ReplyDeleteTumeanza kutafuta msaada wa hali na mali ili kuwawezesha Marine Services Company Limited kuendelea kukiendesha na kukiweka katika hali njema chombo hicho muhimu cha kihistoria ambacho ni kiungo muhimu sana kibiashara, kitamaduni n.k. kwa wakazi wa maeneo ya Ziwa Tanganyika yanayohudumiwa na chombo hicho. Yapo maeneo mengi huko ambako bila Liemba, mambo ya maisha yataparaganyika.
Kwa jinsi hiyo, tunatafuta pia nyaraka na taarifa zozote muhimu kuhusu m.v. Liemba pamoja na filamu tajwa.
Mhandisi Joseph Bhwana
"Rafiki wa Liemba"
consult@juasun.net
Filamu hiyo juu ya m.v. Liemba imekamilishwa na sasa inaoneshwa sehemu mbalimbali na matamasha mbalimbali huko Marekani.
ReplyDeleteHapa Tanzania, jitihada bado zinafanyika kuiwezesha m.v. Liemba kuendelea kutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa eneo la Ziwa Tanganyika na nchi jirani yake ambao hasa wanaitegemea sana.
Nimepata bahati wiki iliyopita ya kusafiri katika chombo hicho kikongwe na chenye historia lukuki kutoka Kigoma hadi Mpulungu na ilikuwa "tukio lenye mvuto tele" kwangu.
M.v. Liemba bado inaweza kutoa huduma na kutunza historia nzuri iliyo nayo kwa miaka mingi, ikifanyiwa matengenezo kama ilivyo kawaida kwa vyombo vya majini vyote.
Mhandisi Joseph Bhwana
Rafiki wa Liemba
consult@juasun.net