Wednesday, January 02, 2008

Kenya inageuka Rwanda


Loh! Nimefuatilia habari za vurugu na mauji Kenya. Mambo yanayotokea huko ni ya aibu.

Hasa kwa vile ni nchi ya Afrika Mashariki inayojulikana duniani kama nchi enye amani na utulivu.

CNN wanasema kuwa waKikuyu wanauliwa na waJaLuo! Wanasema hadi leo zaidi ya watu 300 wamekufa. Hivi, Kenya hakuna FFU wa kutuliza hizo ghasia?

Kisa cha vurugu ni matokeo ya uchaguzi. Mzee Mwai Kibaki kashinda katika uchaguzi, lakini watu wanadai kuwa Mzee Raila Odinga, ndiye mshindi wa kweli. Wanasema kuwa kambi ya Kibaki imechezea kura zilizopigwa kusudi Kibaki aonekane kama mshindi.

Nilikuwa naongea na mKenya (MKikuyu) hivi majuzi kabla ya uchaguzi. Alisema kuwa Mzee Odinga hawezi kushinda maana ni MJaLuo, hajatairiwa na hivyo si mwanaume. DUH! Kwa hiyo mwanaume mwenye govi si mwanaume kamili. Mbona mwenye govi anaweza kumtia mtu mimba?

Nashukuru kuwa Bongo hatuna ukabila na chuki kiasi cha kuuana! Mungu Ibariki Kenya, na Afrika Mashariki!

5 comments:

  1. Yaani wao wanaheshimu mtu kutokana na kilichoko miguuni mwake badala ya kumheshimu kutokana na kilichoko kichwani mwake.

    ReplyDelete
  2. Hao Kikuyu wanakosea. Mjaluo ni mwanume kamili maana ana givi, hajapungukiwa kitu. Kutairi ina maana kuondoa nyama hasa sehemu ya binadamu. Hivyo JaLuo ni mwanaume kamili.

    ReplyDelete
  3. Machafuko na vurugu zilizotokea hivi karibuni na zinazidi kuendelea nchini Kenya, zimesababishwa na walafi wa utawala kujihusishwa na kuiba kura ili wabadilshe matokeo ya maslahi ya wananchi. Wameweka maslahi yao mbele ya maslahi ya wananchi ila wakati huu wamegundua kwamba wananchi hawatavumilia huo tabia. Hao ambao wanadhani kwamba mwenye govi si mwanamume wanakosa busara kweli kweli. Hawaoni fikra zao kama ziko kinyume na wakati. Ukabila, ubaguzi, uchoyo, ufisadi, na kadhalika zinatumaliza sisi wakenya. Jambo ambalo limenitia usumbufuni. Kitu ambacho ninaheshimu kwa wenzetu watanzania ni vile hawana ukabili kama sisi. Hali ya nchi yetu inanisikitisha sana. Haiba ya nchi yetu ambayo yamechukua muda zaida ya arubaini kujenga, yamebomolewa na wanasiasa laghai. Mungu atusaidie wakati ufwatayo na wale wote wameathiriwa na ghasia hizi nchini humo na jirani...

    (Kutoka mkenya fulani anaoishi ng'ambo ambao anahuzunika) :-(

    ReplyDelete
  4. We Chemi unaandika mambo gani hayo sometimes unabore. Ebo!

    ReplyDelete
  5. waafrika wanafki sana. wanajifanya hawawaheshimu watu wenye magovi, mbona hao kina George Bush, Tony Blair na Gordon Brown wote magovi na bado mnawalamba matako kila siku?

    Hamna "ideology" hamna "consistency"

    ReplyDelete