Habari kutoka Uingereza zinasema ndege ya British Airways aina ya 777 imeanguka huko London. Ndege ilikuwa inatua katika uwanja wa ndege ya Heathrow lakini ilikosa nguvu za umeme na ilibidi ifanya- glide. Glide enyewe haikuweza kufikisha ndege njia ya lami ya kutua ndege!
Ndege ilikuwa imetokea Beijing, China. Mungu ni mwema hakuna mtu aliyekufa. Ndege ilikuwa na abiria 136, kati yao 19 waliumia.
Kwa habari zaidi someni:
Mswalie mtume Dada Chemi haikuanguka hiyo ndege ilitua vibaya tu. Hivi ndege ingeanguka hapo airport angepona mtu kweli?
ReplyDeleteHiyo ni Crash maana hata ile chuma ya matairi ya ndege ilinyofoka!
ReplyDeletesikatai matairi yameng'oka lakini nino "Kuanguka" likikaa katika sentensi moja na neno "Ndege" is something very serious. Sio kama inavyoonekana hapo kwenye picha.
ReplyDeleteAnonymous wa 8:00am, asante sana kwa maelezo yako. Ndege ime crash land, nadhani ni zaidi ya kusema ilitua vibaya.
ReplyDeleteWadau wengine mnakarishwa kutoa maoni hapa. Ndege imeanguka au ilitua vibaya?
Ndege ime -crash land sio kuanguka, maana ingeanguka kama walivyosema wengine ingekuwa kizaa zaa. Unajua hizi lugha za wenzetu saa nyingine huwezi kupata neno la kutafsiri kwa kiswahili likaleta maana ile iliyokusudiwa hivyo ni vyema kutumia hilo neno la kiswanglish au english moja kwa moja. Maana ukisema ilianguka watu wanaweza elewa vingine. Ndege inapo crash land, rubani angalau bado anakuwa na uwezo wa kuiongoza hiyo ndege somehow ingawa inakuwa na technical problem/problems, lakini kuanguka anakuwa hana uwezo kabisa si unajua, kama embe dodo linavyodondoka mtini!
ReplyDeleteNi bora ndege ik crash land kunakuwa na survivals kuliko ianguke!