Monday, January 14, 2008

Ugonjwa wa Orthorexia


Kama uko Marekani lazima unamfahamu mtu mwenye ugonjwa wa Orthorexia.

Orthorexia ni ugonjwa ambayo unahusu chakula. Mgonjwa anapima na kuchambua kila kitu anacho kula na kunywa. Lazima kila chakula kinachoingia mdomoni mwake kiwe, 'healthy' cha kuleta afya bora.

Mfano mtu hali cereal mpaka kasoma label ya boxi na kuchambua kila kitu mle na kina calories ngapi. Hata maji ya kunywa si ajabu hataki maji ya kawaida bali anataka kunywa protein water.

Hata akienda restaurant kula lazima aombe food lable inayochambua kila kitu kwenye chakula anachoagiza. Mfano ina mafuta kiasi fulani, vitunguu, nyama, caroti, celery, spinach nk. Halafu anapima kiasi anachokula na kutupa kilichobaki.

Bongo watu tunashukuru kula ugali wetu na mchuzi, kitoweo. Hatupimi kiasi cha calories, tunaangalia shibe. Hatusemi au mchuzi umeungwa na nazi hivyo imejaa cholesterol na siwezi kula! Au nyama ina mafuta hivyo siwezi kula.
Nimegundua watu kama hao si watu wa kuwa nao karibu. Wanakuwa na hasira za karibu shauri ya kuwa na njaa! Pia watu wamekufa na huo ugonjwa, yaani wamekufa kwa njaa!
Kwa habari zaidi za Orthorexia someni:

1 comment:

  1. Weee Chemi wacha kuwadanganya watu wale mavitu ya kunenepesha halafu kinachonichekesha mtu anaetoa ushauri wa afya yeye mwenyewe afya yake hiko hatarini AKA obesse.mimi nilikuwa mnene karibia sawa na wewe au zaidi hata ya wewe kwa miezi kama mitano sasa hivi nimepunguza 4 dress sizes. presha yangu ilikuwa ikipanda sana wakati nilikuwa sijawahi kuwa na matatizo kama hayo I watch what I eat na mazoezi.ukiendekeza kula hovyo hovyo madhara yake sio kupendeza na afya yako pia na nilikuwa na loose temper very easy yaani hata kwa kitu kisichokuwa na maana nilikuwa mvivu sana wa kila kitu sijui wewe mtazamo wako na wangu unaweza kuwa tofauti ila guys dont starve urself ukawa anorexia maana ningumu sana kutibika huu ugonjwa the only way is to eat sensiable

    ReplyDelete