Wednesday, November 26, 2008

Barua kutoka kwa Michael Jackson

Asante mdau D.C. wa Dar kwa kuniletea hii. Ni utani lakini nadhani Michael Jackson anajuta kujikrimu mwili mzima. Bahati ana hela na anaweza kupata check-up mara kwa mara, maana wengine wanaojichuna hivyo wanakufa kwa kansa ya ngozi (skin cancer). Na hivyo siku hizi tunasikia anaumwa umwa, lazima itakuwa atahari za jinsi alivyoharibu mwili wake. Mbona kaka zake wazuri, lakini yeye alijiona mbaya. Anasema alivyo sasa ndo jinsi Mungu alivyotaka awe. Khaa! Si Mungu anakutaka uwe kamalivyokuumba?

***********************************


Message from Michael Jackson

TO ALL MY BLACK BROTHERS AND SISTERS

It is with a heavy heart and regret that I come to you my fellow black brothers and sisters.
Had I known that one day America would be ruled by a black man, I wouldn’t have changed my color.

Please tell me what I should do now?

Yours truly

Michael Jackson (Fellow Black)

8 comments:

  1. You should keep on being mweupe bandia. Umetufanya tuwachukulie kina Michael Jackson wawili kitofauti.
    Watu wengi tunampenda sana mwanamuziki Michael Jackson kwa umahiri wake katika sanaa ya muziki.
    Lakini pia watu wengi hatumpendi mtu mmoja Michael Jackson kwa kuuasi Ueusi wake.
    Pamoja na hayo, ni uhuru wake binafsi juu ya mustakabali wa maisha yake.
    Ila kwa kuwa anawiwa kuijutia nafsi yake, pole zake nyingi, kwa maana wahenga walishanena, 'majuto ni mjukuu'
    Kumbe, majuto huzaliwa na matokeo ya matendo yenye kwenda kinyume.
    Hii nd'o Blackman Revolution, twajivunia. Na mwenzetu akiweza, ajumuike nasi.
    Ni hayo tu Da' Chemi.

    ReplyDelete
  2. Michael "hajajikrimu" kama unavyosema. Ana ugonjwa ambao color pigmentation inaondoka. Huu ugonjwa unaitwa "Vitiligo". Mmoja wa waandishi wa habari wa Fox News station, anao na aliamua kutoa make up ya kumfanya aonekane mweusi ili watu wauelewe huu ugonjwa. Alisema Michael ni mmoja wa watu ambao wameathirika na huu ugonjwa.
    http://timeinmoments.wordpress.com/2007/12/20/fox-anchor-has-vitiligo/

    ReplyDelete
  3. Hata mie niliwahi kusikia kuwa michael alipatwa na ugonjwa wa kupata rangi nyeupe,huo ugojwa ni mbaya sana,unaanza taratibu then unasambaa mwili mzima.ambao tumepona tuombe tusiupate.

    ReplyDelete
  4. wewe anon wa pili hapo juu unayedai jamaa hajajichubua....hiyo pua yake unaionaje?...ni pua ya kibantu hiyo?....huoni kwamba imechongwa hiyo.......na kama aliichonga ili ifanane na mzungu basi na rangi yake ilikuwa lazima ilazimike kufanana na mzungu.

    ReplyDelete
  5. Da Chemi habari za leo,
    Haya hii inaonyesha ni jinsi gani tulivyowepesi kutoa negative judgement tunaposikia mabaya ya wenzetu, badala ya kutafuta ukweli kwanza.
    Michael Jackson hakujichubua, bali alizaliwa na ugonjwa chronic wa ngozi unaoitwa "Vitiligo" au "Leucodema" ambao umekuwa ukiprogress kidogo kidogo tangu akiwa mtoto,huu ni ugonjwa serious sana wa ngozi ambao unasababisha kupotea kwa skin pigmentation(kwa weusi ni ile rangi nyeusi ya juu ya ngozi)na kumfanya kuwa na mabaka meusi na meupe ya ngozi,sasa imagine kama uko kwenye showbussiness na hali kama hii, ina frustate sana. Ugonjwa huu pia unamfanya mtu kuwa sensitive na jua(ndio maana Michael anatembea na Mwamvuli pamoja na sunglasses wakati wote).
    Matibabu anayopata Michael toka kwa madaktari wake ni kujaribu kuisawazisha rangi ya ngozi yake kwa kutumia madawa na miyonzi mikali sana ambayo side effects zake ndio kama hizo kuwa mweupe kupita kiasi. Sasa imagine nywele za kiafrika na ngozi kama ya mzungu wapi na wapi? hana choice inabidi atreat nywele zake ziendane na ngozi.
    Halafu pia sasa hivi lazima watu mfahamu kuwa media especially za Marekani ziko very biased hasa kwa mastaa weusi. Michael Jackson has always and still is King of the Pop anayeheshimiwa sana duniani.
    Ndiye mwanamuziki pekee mwenye the biggest selling record of all time kwa kuuza over 50million copies za "Thriller"peke yake duniani, achia album nyingine,na hii ilimuwezesha kuwa kwenye Guiness book of World Records, mpaka sasa hakuna aliyevunja hiyo record.
    Michael pia ni mmoja wa wanaotoa hela kibao kwenye charities na humanity organizations duniani.
    Kwa hiyo basi ukiachia mambo mengine ambayo ni challenges za kawaida kabisa kwa mastaa wakubwa(eg. kufilisika),na mabalaa mengine,tunarudi pale pale kwamba wazungu watafanya kila wawezalo kummaliza Michael maana hawataki kusikia the fact kwamba yeye ndiye king of pop na sio huyo kikaragosi wao Elvis Presley.
    Hiyo barua feki eti toka kwa Michael Jackson is a big joke!!
    Peace.
    Maggie,
    Canada.

    ReplyDelete
  6. Ninyi wadau mnaosema Michael ana ugonjwa wa ngozi 'vitiligo.' Siyo kweli, hayo ni madai yanayotolewa na Michael mwenyewe katika kujitetea au kuhalalisha kubadili rangi. Ingekuwa suala tu ni Vitiligo basi angefanya kama alivyofanya Thomas yule reporter wa Fox Newsp; atumie make up zinazoshabihiana na ngozi yake! Wala asingechonga pua! Kwahiyo msimtetee eti ana 'skin condition' hayo siyo madai ya kweli!

    ReplyDelete
  7. ALIJICHUBUA! SIYO UGONJWA HUO! WENYE HUO UGONJWA WANAKUWA NA PATCHES ZA WEUSI! MJ NI MWONGO!

    ReplyDelete