Tuesday, December 09, 2008

Ni Dhambi kula kwa Mama Ntilie?

Jamani! Hivi ni dhambi kula kwa Mama Ntilie? Ni lazima kula chakula cha kizungu kwenye hoteli za kifahari ili uonekane mtu? Khaa! Sielewi kwa nini magazeti wanamchora mrembo Miriam Odemba kwa kula kwa Mama Ntilie. Nakumbuka nilivyokuwa Daily News kulikuwa na Mama Ntilie waliokuwa na chakula kizuri kweli kweli tena kitamu! Of course usafi ni muhimu, na wengi walijitahidi kwa usafi kuliko hata ungekula hotelini.

Wadau mnaonaje?

9 comments:

  1. Mimi naona ndio kwanza anaonyesha mfano mzuri kwa kula kwa mama ntilie.

    ReplyDelete
  2. Sio aibu kabisa tena namsifia. Mimi naimisi sana mama ntilie.Mara nyingi nirudipo bongo na mama wangu wa kizungu na watoto wangu huwa nawapeleka kwa mama ntilie nao wajisikie maisha yangu ya ujana.
    Nampa hongera sana.Binadamu hawezi kutupa ya zamani eti kwa ajili ya.......

    Malisa BG

    ReplyDelete
  3. sidhani kuwa katika masharti kuwa mrembo au maarufu kuna kipengele ambacho kinakuzuia kula kwa mama ntilie ni swala la kawaida sana mbona

    ReplyDelete
  4. Tatizo la watu wengi hawajui kwa nini Odemba alifika alipo, kula kwa mama ntilie siyo kitu cha kushangaza wengi wao hawakubali na hali halisi ila wanatoa shutuma tu huyu anajaribu kuwaendeleza au kuwaonyesha umaarufu ni kivuli siyo kitu muhimu kama kinavyoonekana miongoni mwa watu, pili anajaribu kuwakwamua kina mama au kinababa wa kitanzania kujikwamua kiuchumi.

    ReplyDelete
  5. Sasa walitaka ale kwenye hoteli za wazungu?

    ReplyDelete
  6. ..kwanza chakula cha mama ntilie kiko bomba kuzidi vyakula vya hoteli zao.unajua watu wamekosa kitu cha kuandika so wanaandika chochote wanachotaka....

    ReplyDelete
  7. Hongera Odemba kwa kula chakula asilia,kwa nini tunataka maisha ya juu na wakati hatupati pesa ivyo,utakuwa mamis wengi wanaharibika kutafuta mabuzi ya kuwapeleka mahoteli makubwa ya kizungu kwa kuhofia kula chips vumbi na kwa mama ntilie,sio mama ntilie wote wachafu,mimi nina shangazi yangu msafi kalisha watu sana posta na mabosi na matai yao,niambie leo yuko wapi kashaanza kupiga na trip za china na sasa ana duka kariakoo ni Umama ntilie huu huu sasa kwa nini waTZ mdharau kiana hiyo jamani,
    hawa hawa dada zetu mamiss mkiwaona na mabuzi hotelini mnawatoa kwenye magazeti dada zenu malaya,na wakienda kwa mama Ntilie mnawatoa sasa wajifungie ndani?

    Pia kuna mfano wa miss mtangazaji now yuko Califonia unaambia siku moja yuko Dar kwenye kipindi chake anajitangazia eti hawezi kwenda Kariakoo hata siku moja,kwa madai ukienda uko unaonekana mshamba,

    BIG UP MIRIAM ODEMBA
    WAONESHE MFANO VIJIMISI VISHAUZI WA BONGO

    ReplyDelete
  8. wooooow i luv that, kwan tatizo liko wapi jaman tena hiccho cha huko ndo healthier zaid kuliko hayo majank food cjui ya wapi huko mac cjui steers.

    ReplyDelete
  9. Sio dhambi absolutely.She has right to eat anywhere she feels like.Its her personal decision wala sio ya jamii.People take chill pill.Miriam live your life and let the hater be your motivation!

    ReplyDelete