The Obama's & The Biden's mara baada ya kuapishwa
(Picha zote kutoka CNN.Com)
Wadau, leo mchana Senator Barack Hussein Obama, ameapishwa kuwa Rais Marekani. Alitumia jina lake kamili bila aibu. Wengi walisema atatumia Barack H. Obama kwa vile waMarekani wengi hawapendi jina la Hussein kwa vile inawakumbusha Uislamu na Saddam Hussein. Pongezi kwa Obama kwa kuheshimu jina aliyopewa na wazazi wake!

Sasa anaanza kazi ngumu ya kuwa Rais Marekani. Mungu ampe nguvu na amlinde yeye na famila yake.
Pongezi zake nyingi na tunamtakia
ReplyDeletemafanikio. Pongezi pia kwenu wapiga kura. Ni mfano mzuri sana kwetu na kwa vizazi vyetu vijavyo.
Tunamuombea Mungu amlinde.
Ron,
London.
Obama ni rais wa Afrika pia! Ni rais wetu. Baba yake ni Mkenya hivyo tunamtambua kama mwafrika mwenzetu. OBAMA OYEE!
ReplyDeleteHiyo ni historia ambayo itakumbukwa milele, wabaguzi wajue kuwa kila jambo lina wakati wake chini ya jua na sasa ni wakati wa Obama kukalia kiti, kuongoza Taifa kubwa Duniani ni wakati wa White House kukaliwa na Black Family na hiyo ni mipango ya MUNGU.
ReplyDeleteDada hizo koma za kwa juu "apostrofu" kwenye hayo majina zinafanya kazi gani?
ReplyDelete