Thursday, March 26, 2009

Jamaa Ananuka!


Robert Pattinson

Jamani, leo asubuhi nimeshangaa sana nilipofunga TV na kusikia watangazaji wakisema kuwa, mcheza sinema, Robert Pattinson' ananuka! Tena walisisitiza kuwa jamaa ananuka vibaya sana. Wanasema haogi na haoshi nywele zake. Je, anapiga mswaki? Pattinson anaigiza kama mnyonya damu (vampire) kwenye sinema, Twilight. Yaani wakawa wanamsema vibaya na hata kumwita 'skunk' (mnyama ananuka huyo). Yaani kunuka kwa mtu ni habari! Kweli ilikuwa slow news day.

Halafu cha kuchekesha huyo Pattinson aliwahi kulalamika kuwa alivyokuwa Marekani alishindwa kumpata bibi ingawa ni mzuri na anaongea na lahaja ya Uingereza. Labda angekuwa msafi angefanikiwa. Anavyopendwa na wasichana hapa Marekani ni balaa. Ila wakiisikiahiyo harufu mapenzi yatapungua. Unasikia kwenye TV msichana anasema, "nikikutana na jamaa na ananuka....kwa heri!"

Waliosoma historia wanajua kuwa hapo zamani za kale wazungu walikuwa na tabia mbaya ya kutokuoga. Walishangaa walipoenda sehemu mbalimbali duniani na kukuta watu wanaoga mara kwa mara. Inadaiwa kuwa Malkia Elizabeth wa kwanza alikuwa anaoga mara moja kwa mwezi na hivyo walimwona msafi mno. Walisema kuwa kunuka ni jambo la kawaida na kuwa na uchafu mwilini ni vizuri maana ni kinga dhidi ya magonjwa, huko waafrika wanajitahidi kuoga kila siku. Nani mshenzi?

Kwa kweli hapa Marekani, kuwa na (Body odor/B.O.) ni mwiko. Or course watu kuna watu ambao wananuka, na mtu unaweza kufukuzwa kazi ukienda na kikwapa. Watakuambia hizo deodorants, shampoo na sabuni zina kazi gani! Hebu tumia! Matokeo yake pua zetu hapa Marekani zimekoshwa (sanitized). Yaani ukisikia kikwapa unaona balaa. Mara nyingi unakuta ni hao ombaomba na wasio na makazi (homeless) ndo wanakuwa wachafu.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.trendhunter.com/slideshow/robert-pattisons-body-odor-problem

http://www.mtv.com/news/articles/1607791/20090326/story.jhtml

http://www.suntimes.com/entertainment/zwecker/1496176,CST-FTR-zp26.article

6 comments:

  1. Kwi, kwi, kwi! Mzungu asipooga utamjua nywele zinanasiana na piangozi yao inaoyesha uchafu. Mapesa yote aliyonayo na anashindwa kuoga. Nimeona hata maekta wenzake wanamlalamikia!

    ReplyDelete
  2. LOL! Kwli walikosa habari. Wamekasirikia kwa vile mabinti wao inamwona kama Mungu mdogo!

    ReplyDelete
  3. DAH! Hii kiboko! Sasa wafike Afrika na vikwapa ni jambo la kawaida watasemaje? Mzungu kaonewa!

    ReplyDelete
  4. Labda wazungu wa USa ndio wanaoga kilasiku. Scandnavian wanaoga mara 2 au 3 kwa wiki. Wanasema wanabana matumizi ya nishati. Ila wanatumia deodorants kukata kikwapa. Waafrika tunaoga mara nyingi ila hatutumii deodorants.

    ReplyDelete
  5. Huyu jamaa naona wamemtoa kwenye Frontpage ya jarida maarufu la GQ Mens Magazine, April 2009 issue na ndani wamemsifia sana na kuchapisha mapicha kibao

    http://men.style.com/gq

    ReplyDelete
  6. Aisee hii kali!!! Mwenyewe kwenye Twilight amecheza vizuri sana. Sema sishangai kusia ananuka. Actors wengine sijui inakuwaje, mimi nina jirani yangu hapa marekani ambaye tuko nae apartment moja. Dah, jamaa anananukaaa! Anavaa vizuri lakini haogi wala hafui nguo alafu he is gay. Na ndio maana hata hawezi kaa na boyfriend muda mrefu. Ananuka mno alafu yeye hajijui!

    ReplyDelete