Kutoka Mwanahalisi
Na Aristariko Konga
BALOZI Getrude Mongella, Rais wa kwanza wa Bunge la Afrika (PAP) amelazimika kujiuzulu kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na ajira za upendeleo katika ofisi hiyo.
Hatua ya kulazimishwa kuachia ngazi imekuja baada ya mlolongo wa malalamiko kutoka kwa wabunge wa PAP kutokuridhika na mwenendo wa matumizi ya fedha na uendeshaji wa ofisi hizo.
Nafasi yake imechukuliwa na Dk. Idriss Ndele Moussa, Mbunge kutoka Chad, katika uchaguzi uliofanywa na bunge hilo 28 Mei mwaka huu. PAP ina makao makuu katika mji wa Midrand, nchini Afrika Kusini.
Dk. Ndele aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wagombea wenzake wawili; Lassane Sawadogo, mbunge kutoka Burkina Faso na Mustafa El Gendy, kutoka Misri.
Dk. Ndele aliapishwa na Dk. Mongella kuchukua wadhifa huo mpya, akiwa na kazi ya kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi na utendaji wa PAP, kutokana na maagizo ya wabunge ya 19 Mei, mwaka huu huko Midrand.
Bunge la Afrika pia lilichagua makamu wanne wa rais ambao ni Bethel Amadi (Nigeria), anayewakilisha Kanda ya Afrika Magharibi na Mary Mugyenyi (Uganda) anayewakilisha Afrika Mashariki.
Wengine ni Laroussi Hammi (Algeria) anayewakilisha kanda ya Kaskazini, na Joram Gumbo (Zimbabwe) anayewakilisha kanda ya Kusini mwa Afrika.
Mabadiliko yanatokana na kuwapo tuhuma dhidi ya Mongella kuwa chini ya uongozi wake, ajira zilipatikana kwa misingi ya upendeleo na bila kufuata taratibu za ajira wala sifa za watumishi.
Habari zinasema kuwa katika siku za karibuni, kabla ya mabadiliko hayo, Mongella alijaribu kung’ang’ania ili aendelee na wadhifa huo, lakini alishinikizwa kuachia ngazi, jambo ambalo lilikamilika 28 Mei mwaka huu.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk. Thomas Kashilila, alipoulizwa juzi Jumatatu, alikiri kuwa na taarifa za Mongella kuacha wadhifa huo, ingawa ofisi yake haikuwa na taarifa rasmi kutoka PAP.
“Tumepata taarifa kupitia njia nyingine, lakini hatuna taarifa rasmi kuwa kaacha wadhifa huo,” alisema Dk. Kashilila.
Mwenendo wa Mongella uliishakuwa hoja hadi wakuu wa nchi za Afrika kuunda kamati maalum ya kufanya uchunguzi wa usimamizi na uendeshaji wa PAP.
Taarifa zinasema bunge lilijadili kwa kina taarifa ya kamati hiyo na kujiridhisha kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya fedha.
Katika hatua ambayo haikutarajiwa, inaelezwa kuwa serikali ya Tanzania imekubali kubeba mzigo wa kulipa fedha zote ambazo Mongella alituhumiwa kuzitumia vibaya.
Taarifa zinasema awali, hata baada ya serikali ya Tanzania kuchukua mzigo huo, Mongella alishauriwa ajiuzulu ili kulinda heshima ya Tanzania, lakini aligoma kufanya hivyo.
Wabunge wa Bunge walilalamika kwa viongozi wakuu wa nchi za Afrika juu ya uongozi wake kwa ujumla, ambao wanadai haukuwa na dira wala tija.
“Kuna madai pia kwamba aling’ang’ania kubaki katika nyumba ya Bunge na alipolazimishwa kuondoka akaamua kuhama na fenicha zote za ndani akidai ni zake, jambo ambalo si la kweli,” alisema mbunge mmoja wa Bunge la Afrika kutoka Tanzania ambaye hakupenda kutajwa jina.
Aidha, uongozi wa Mongella umelalamikiwa kwa kushindwa kufanya jambo la maana wakati uliendelea kugharimu rasilimali za nchi za Afrika.
Mjadala wote wa kumuondoa Mongella ulikuwa unaripotiwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari vya Afrika Kusini na Namibia. Kuna wakati Mongella alilazimika kukatisha kikao cha Bunge hilo na kufanya mazungumzo ya faragha na makamu wake wawili.
Baada ya kikao hicho cha siri, Mongella aliamuru waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia kikao waondoke, jambo ambalo lilifanyika.
Naye mbunge mpya wa Tanzania katika PAP, John Cheyo amesema Mongella atakumbukwa kwa kuwa rais wa kwanza wa PAP.
Ni MwanaHALISI iliyowahi kuandika katika toleo Na. 73 la Novemba 28 hadi 4 Desemba 2008, kwamba Mongella alikuwa anatuhumiwa kutenda makosa ya kukosa uaminifu, wizi na utoaji ajira kinyume cha taratibu.
Kuhusu wizi, Mongella anatuhumiwa kutafuna dola za Kimarekani 138,000 sawa na Sh. 180 milioni za Tanzania, mali ya PAP.
Katika tuhuma za utoaji ajira, Mongella anatuhumiwa kuajiri jamaa zake ndani ya Sekretarieti ya Bunge hilo, kinyume cha taratibu. Tayari Bunge limeagiza kufuta ajira zilizofanywa na Mongella.
Kwenye moja ya magazeti ya Tanzania leo tarehe 15.06.2009 limeongelea suala la Dkt Slaa kukusudia kuhoji Bungeni kuhusu matumizi ya TZS milioni 180 kumlipia Dkt. Mongella huko Bunge la Afrika kama fedha zilizopotea chini ya utawala wake.
http://www.news24.com/News24/Africa/News/0,,2-11-1447_2519234,00.html
lingekuwa bunge la CCM asingeondoka na angejitetea kuwa maadui zake wa kisiasi wanamchafulia jina kwasababu amefanikiwa sana.
ReplyDeletetukiacha kulindana na kuogopana hivyo ndivyo inavyotakiwa Tanzania tuwe tunaendesha shughuli zetu. wababaishaji wote piga chini, huruma ni kazi ya watumishi wa mungu na red cross.
mwenyewe amesema kuwa hajalazimishwa kujiuzulu bali amemaliza mkataba wake. sasa tuamini lipi? ameshinikizwa kujiuzulu au amemaliza mkataba wake kwa mujibu wa sheria?
ReplyDeletenaomba jibu
...the Pan African Parliament (PAP) president Getrude Mongella, (65) has resigned the position following accusations of financial mismanagement and ‘lack of confidence’ from the members of the said parliament....
ReplyDeleteSI KWAMBA KAMALIZA MKATABA, KAJIUZULU KUTOKANA NA TUHUMA!
Huyu Mama nafikiri imo ubadhilifu na upendeleo ni sehemu ya genetic makeup yake.... Maana kama mtakumbuka mwaka 1995 alikuwa Mwenyekiti wa kikao cha kinamama duniani kilichofanyika "BEIJING" alikwenda na mwanae wa KIUME kama private advisor/secretary/,,,, wake na kijana akawa anakula allowance za UN kila siku.. what is 138,000 USD for such a person with alot of allowances and all kids working in good positions?? Is it.....
ReplyDeleteSio mara ya kwanza!
ReplyDeleteKatuangusha, kama alivyotuangusha kwa nafasi ya Sec. General wa Mkutano wa Wanawake wa Beijing!
Baada ya kutoka Beijing tu, Boutros Boutros-Ghali (بطرس بطرس غالي) kamtimua shauri hiyo hiyo ya ubadhirifu wa pesa za ki-mataifa na nafasi yake ikachukuliwa na Mama wa Jamaika!
Fisadi mkubwa huyo!
kazoea kuwapa ndugu zake kazi. Alipokuwa Katibu mkuu wa wanawake, kamleta ndugu yake Bi. Kiswaga. Kwa bahati nzuri, UN haikumfukuza huyo Kiswaga!
ReplyDeleteHuyo mama kachanjwa! Alikuwa karani tu katika ofisi ya waziri mkuu, Sokoine. Sokoine alivyokufa Mongella alikuwa mstari wa mbele katika kulia. Tena alikuwa analia mpaka utadhani atatoa machozi ya damu! Kapandishwa cheo and kupata vyeo asiyostahili kabisa! Siku za mwizi ni arobaini!
ReplyDeletehuko huko beijing, kawachangisha wajumbe wa Tanzania kusaidia malipo ya hafla waliyofanya na hali Tanzania ilikuwa imemtumia pesa zaidi za hafla za namna hiyo kupitia Ofisi yetu ya Ubalozi, endapo angefanya hafla hizo!
ReplyDeleteLakini yeye kadai apewe hizo pesa na kusiweka kwenye akaunti yake!
Hayo hayo ndio yalimharibia. UN na wapenzi wake, kama akina Ford Foundation na wengine walikuwa wametoa pesa nyingi kwa ajili ya hafla za namna hiyo.
Mongella na makarani wake wa ndugu zake ndio wanajua wenyewe jinsi hizo pesa zilivyotumika.
Ghali kakasirika; kamtimua!
Aibu kuwa kwa taifa letu tunaomba misaada kwa taifa kumbe watu wanakula kilaini na bado sasa Tanzania imejaa rushwa na ufisadi hata nje za nchi wanajua Tanzania nimafisadi wakuwa tena sisi watanzania tulioko nje yanchi wakijua sisi niwatanzania wanajua sisi ni mafisadi looh! aibu gani hii jamani halafu uniambie mimi nirudi kuja kunyanyasika sirudi ng'o hata kwa mtutu wa bunduki bora niwe kibaraka marekani kuliko ninyanyasike na elimu yangu CCM aibu tupu na uwizi mtupu usinibanie maoni yangu
ReplyDeleteWatanzania hivi hizi aibu tutazipeleka wapi ??? Kila upande Ufisadi, EPA, Rushwa hata kwa Mongela? Nilijua muomba Mungu hachoki. Alimuajiri Mama Fulani anayeishi Chang'ombe ambaye tulikuwa tunafanya naye kazi. Hivi sasa huyo mama ni Fisadi mkubwa, anafuga ng'ombe maeneo ya wanaoshi watu mbolea anamwaga hovyo, hasa kipindi cha mvua tunaipata. Ukienda kwa Bwana Afya Temeke wanaogopa kwa vile anakula sahani moja na Mongela. Mungu si Athumani. Arobaini imefika. Watanzania tuamke sasa michango ya Walala hoi inaliwa na Wakubwa. Tutalala hadi lini? 2010 naomba ufike haraka tufanye mabadiliko. (Naomba usibane kutoa maoni yangu haya tafadhali)
ReplyDeleteDr. Slaa Baba yetu usichoke. Hivi Tanzania ingekuwa na uwezo wa kulipia wezi, kwa nini basi isiwalipie ma-EPA, Rais kapanda ndege hadi kwa Obama kuomba msaada kwa wananchi wake wa Tanzania. Obama akisikia haya si atagoma kutoa huo msaada. Mbona mnatia Rais wetu aibu jamani wana-CCM? Ukisikia mwizi katokea CCM. Hizi aibu hadi lini Watanzania wenzangu. Wanawake walikuwa wanaaminika kumbe mwanamke mwenzetu katutia aibu kiasi hiki? Looooooo ! (Naomba ussibanie maoni yangu)
ReplyDeleteMongela machozi ya maskini umeona matokeo yake? Ulipompa Mama Kitambi utajiri kwa kuwa alikuwa anakufiichia siri umeona matokeo yake sasa? Na bado tunasubiri mengine, hilo ni part 1 part2 bado kabisa !!! Najuuta kukufahamu !!! Najuuta kuwa mwanamke !!
ReplyDeletesie wabongo sijui vipi yaani, ufisadi kila mahali, kha ifike wakati tuone aibu kidogo jamani ah! bila hata haya mtu unaenda kuharibu huko nje afu kuna mtu anasema oh ye ndio spika wa kwanza so what, hapa tunaangalia legacy aliyoiacha huko, ufisadi? ndio tukumbukwe hivyo? ah yaani mi sijui hawa watu wafanyajwe maana ni tamaa tu sio kwamba hana!
ReplyDeleteMama Mongella has disgraced Tanzania and Tanzanian women. SHAME ON HER!
ReplyDeleteHawa ndio mafisadi, na ndio hso hso esnsosngusha Taifa la Tanzania, na Africa kiujumla.
ReplyDeleteHuu ujinga utaendelea mpaka lini? Taifa limlippie nini? na huo ufisadi wake. michosho sana watu kama hawa, Ndioo maana Africa kuendelea shughuli.
ReplyDeleteMmmh Dirty Gertie!
ReplyDeleteEh makubwa kumbe mama kitambi,ananuka rushwa lol i thought she was just a very hard working woman.Aibuuuu hii na wala siamini.
ReplyDeleteThis woman should be taken to court, and face the full wrath of the law. Enough is enough, as a country, we are sick and tired of few people who are tarnishing our image for their personal gains. From what I can remember , she ran for president in 2005; thanks God, she didn't reach far. This woman is not only greedy but also ugly. She neeeds extreme makeover ....
ReplyDeleteHalafu akiwasili kwao Ukerewe atalakiwa kwa maandamano, mithili ya Lowasa na Chenge!
ReplyDeleteMkuki kwa nguruwe; kwa Mmasai, Msukuma na Mkerewe, mchungu!
Tanzania tumeisha!
Mimi nashangaa sana serikali yetu. Mbona imekaa kimya kuhusu hili la huyu mama Mongela mwizi? Angekuwa aliyefanya wizi huu ni mwananchi wa upinzani sijui kama Bungeni kungekalika. Lakini kwa kuwa huyu mama ni mshikaji wa wakubwa hata halisikiki. Natumaini hata wabunge wenzake wanawake wa CCM hawajalisikia kwa hata kwao ni aibu pia !!! Shame on Mama Mongela, Shame on Mama Kitambi aliyekuwa PS wake wakawa wanaiba wote !! Wananchi wa Tanzania tunakoelekea ni kubaya !! Halafu Serikali inasema itamlipia deni hilo. Bila aibu wanatamka hivyo. Hivi mnataka damu imwagike kama Kenya, Uganda, Zimbabwe na kwingineko. (Usinibanie kutoa maoni haya)
ReplyDeleteOh Mungu wangu! Na sasa ndiyo anagombea tena ubunge kwa tiketi ya kifisadi CCM! JK kama kawaida yake keshampigia debe sawa na kina Rosham, Lowasa, Mramba, Chenge n.k.
ReplyDeleteKwa nini tusiamini JK ni sehemu ya tatizo la ufisadi?
Hebu tukumbushane, nani vile waliohusika kutia sahihi mkataba uliolifilisi TANESCO wa IPTL mwaka 1994? Kikwete alihusika kama waziri wa nishati na madini! Na nina mashaka kama hakuhusika na ile kashfa ya gharama hewa za ununuzi wa nyumba kule Italia ambayo sasa imegeuka ya "aliyeshikwa na ngozi ndiye aliyeiba ng'ombe"
Ilikuwa vigumu kwa dili kubwa kama lile kupitishwa na balozi tu bila ya waziri wake kujua.
Natamani Oktoba 31 wananchi wa Ukerewe wamtose.