Hata na mimi yamenipata! Yaani posta Tanzania kuna wizi! Hata haya hawana!
*************************************************
Kutoka Michuzi Blog:
Msaada Kwenye Tuta - Posta Kulikoni??
Kwanza nakupa pongezi mkuu wa nanihii kwa kuendeleza libeneke. Udumu. Kuna ujumbe ningependa kuutuma kwa jamii kupitia globuni.
Hivi karibuni nilitumia huduma za posta kutuma kipeto chenye mipira miwili ya kandanda kutoka kwa Obama kwenda Mwanza. Mpira mmoja ulikuwa mpya kabisa na manailoni, mwingine ulikuwa umetumika kidogo.
Kuna mwizi bila aibu akafungua kile kipeto, akatwaa mpira mpya na kuurudishia uliotumika kidogo kisha akafunga lile kasha. Aliyetumiwa zawadi alilipa kodi za TRA kwa ajili ya kupokea mipira miwili kama ilivyoonyeshwa kwenye fomu za customs kwenye mzigo ule bila kufahamu kwamba mzigo umeibwa nusu. Alishangazwa alipofika nyumbani.Tukio hili limenisikitisha sana.
Inawezekana mwizi huyu amejaaliwa uwezo wa kifedha kuliko wadau waliokuwa wanausubiri mpira kwa hamu lakini bado ameona awaibie.
Mie bwana bila ya kwenda Mlingotini wala Sumbawanga nimelivalia njuga suala hili na sina shaka kwamba nitakapofikia mwisho wa ufuatiliaji wangu mpira huo utamtokea puani mwizi huyo.
Naomba kuwatahadharisha wadau mnaohitaji kutuma vipeto kutoka ughaibuni kwenda nyumbani. Kuna wezi wa vipeto wamejichanganya na wafanyakazi wa posta. Mabosi wa Posta mmesikia hili? Fanyeni usafi idara ya vipeto, kuna wezi wamejichanganya kwenye ofisi zenu.
Kama posta za ughaibuni zinaweza kufikisha vipeto vya watu na kuviacha mlangoni vikafika, kwa nini sisi tushindwe?
Mdau mwenye Usongo na mbaya wake
kuna dada mmoja alinitumia DVDs kuto Texas zikapotea baada ya kufika tanzania. Shirika la posta kama mnasoma hii maneno badilikeni.
ReplyDelete