Wednesday, September 30, 2009

Kituo cha Reli ya Kati - Tabora

Wadau, mliosoma Tabora, mnakumbuka hii kituo cha Reli? Bado iko vilevile haijabadilika! Mnakumbuka usafiri wa CENTRAL LINE?
Picha kutoka: http://www.5cense.com/EA/Tanz_cent.htm

10 comments:

  1. da Chemi umenikumbusha mbali sana, si utani. Boys walikuwa hawathubutu kupata treni moja na wanaume - Milambo.

    kuhusu kituo, wahindi wamealikwa kuua kila kitu - tunarudi nyuma. wasomi wa kufanya hiyo kazi tunao, si kuna chuo cha reli hapo? lakini tukaambiwa wageni ndiyo hodari zaidi....

    ReplyDelete
  2. Enzi zile unaenda stesheni DAR! Behewa nzima imetengwa kwa ajili ya TABORA GIRLS! au MILAMBO! au TABORA BOYS! Those were the days!

    ReplyDelete
  3. Mimi nacho kukumbuka zaidi ni 'SAFARI FOOD'! Mnapewa biskuti, orange squash, matunda na vitu vingine. Tulikuwa tuna tunzwa enzi hizo!

    ReplyDelete
  4. Nakumbuka tulifunga shule, tuna ticket zetu mikononi,taxi zilishakodiwa na tupo hapo kituoni, ndo tukapata habari treni imeharibikia maeneo ya Morogoro. Tulilala hapo kituoni usiku kucha mpaka saa saba mchana ndo tulisikia honi. Mizigo yangu ilipata ulinzi ambao haijawahi kuupata kuhofia wale vibaka wa stesheni. Pana baridi asubuhi!

    ReplyDelete
  5. Kweli Tabora asubuhi pana baridi. Nami niliwahi kulala stesheni, tuliambiwa kuna vibaka na wanyonya damu usiku!

    ReplyDelete
  6. Iko vile vile kama mkoloni alivyoiacha!

    ReplyDelete
  7. Ungekuwa mhindi au hukukulia Tanzania ningekuelewa...kiswahili gani hiki "mnakumbuka hii kituo cha Reli? Bado iko vilevile haijabadilika!"

    ReplyDelete
  8. Hiki kituo kinanikumbusha kipindi tukitoka SHYCOM siku moja rafiki yangu aliibiwa begi lake hapo. Nilikuwa makini sana Tabora na Dodoma maana wezi wa hapo walikuwa professional.

    ReplyDelete
  9. Tehehe! Wezi professional kweli hapo Tabora. Mwenzetu aliibiwa hela iliyokuwa ndani ya sidilia! Tena alikuwa amevaa shati aina ya pullneki (Turtle neck)!

    ReplyDelete
  10. haha eti aliibiwa pesa iliyokuwa kwenye sidiria....wewe pia ni pia ni professional comedian

    ReplyDelete