Tuesday, January 05, 2010

TANESCO Mwogopeni Mungu!!!!

(Pichani: Askofu Zakaria Kakobe Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam)

KAZI IPO!!!! Naona hii miaka ya karibuni wanazidi kumsumbua Askofu Kakobe!

****************************************************

Kutoka ippmedia.com:

Na Joseph Mwendapole

5th January 2010

Waumini wa Kanisa la Full Gospel Bible Felloship, lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam, wameanza kulinda mabango yao kwa saa 24 na wameapa kuwa iwapo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) litajaribu kuyaondoa patachimbika.

Akizungumza jana na Nipashe kwenye Kanisa hilo, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Zacharia Kakobe, alisema vijana wake wamehamasika na wameamua kulinda kanisa lao kwa saa 24 hivyo Tanesco wasijidanganye kuwa wanaweza kuyaondoa mabango hayo.

"Vijana kama unavyowaona wako hapa kwa saa 24 kuhakikisha tingatinga likija kutaka kuyaondoa halifanikiwi maana huu ni uonevu dhidi ya Kanisa, na wamevaa sare ili iwe rahisi kutambulika kuwa ni waumini wa hapa," alisema Kakobe.

Fulana walizovaa waumini hao zilikuwa zimeandikwa “Tanesco mwogopeni Mungu, baada ya Richmond sasa mmeligeukia kanisa”.

Askofu Kakobe alisema mabango hayo yametengenezwa kwa Sh. milioni 120.

Alisema Tanesco ilijaribu kupitisha nyaya hizo upande wa pili lakini baada ya kujadiliana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilikataa baada ya kubaini hatari ya kupitisha umeme huo mkubwa karibu na makazi ya watu.

"Wasomi walikataa maana wanaujua umeme na madhara yake, sasa walipoona wameshtukiwa kule wakaona waje wapitishe huku kwetu ambako walidhani waumini ni watu wasiojua kitu, cha kushangaza walianza kwa kutwambia kuwa umeme huo hauna madhara baadaye wakasema wakishaweka nyaya zao itabidi mabango haya yaondoke maana ni hatari yakiendelea kuwepo sasa wanajichanganya wenyewe," alisema na kuongeza kuwa yeye ni msomi wa sayansi na anaufahamu vilivyo umeme.

Alisema shirika hilo limekuwa likitoa fidia tangu Ubungo zitakazopita nyaya hizo lakini walipofika kwenye Kanisa hilo hawakuona hata umuhimu wa kuzungumza na waumini ili kufikia muafaka.

Tanesco imeshasema kuwa itatekeleza mpango huo mapema mwaka huu, baada ya utafiti wa wataalamu na ushauri wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kwamba hauna madhara kwa wakazi wa eneo hilo.

CHANZO: NIPASHE

7 comments:

  1. Kweli TANESCO Imejaa mashetani! Wakomeshwe katika jina la Bwana!

    ReplyDelete
  2. wewe unayesema wakomeshwekwa na jina la bwana wewe ni mahakama hacha hizo kama anaonewa aende kwenye vyombo vya sheria apawe haki yake kwanza mipango miji majiji ipo tokea cku enzi hizo sasa kanisa la juzi juzi kalidinali Pengo aliposema Kakobe ni tapeli kwa sababu cheti cha uwasikofu wake ni kufoji watu hawakuelewa maana yake.

    ReplyDelete
  3. hawakeri wala nini ni kuwaletea maendeleo wananchi. ingekuwa waislamu wangekwisha letewa ffu wakapigwa virungu na maneno mengi ya kejeli kama hawakusoma, wapinga maendeleo, siasa kali, mujahidina, magaidi na maneno kama hayo.

    lakini kwa kuwa ni kanisa kila mtu yupo kimya eti aogopwe mungu. kwani nani asiemuogopa mungu?

    umeme lazima upite hapo kama hawataki waende mahakamani kupinga sio kufanya uchochezi.

    ReplyDelete
  4. tanesco wangekuwa wanatoa huduma kama wanavyohangaika kwa kakobe ningewapa big up. dar es salaam haina mipango miji ni usanii tu ili waonekane nao wapo. kama kuna hiyo mipango miji walikuwa wapi wakati anajenga kanisa.au pia walikuwa wapi kupitisha huo umeme (ambao ni wa mgao) waya unatoka wapi unaenda wapi leo hii, which means kuna watu wamekuwa hawapewi umeme miaka yote hii. leo ndio wanataka kuwapelekea kwa kumdhuru kakobe kisa uchaguzi. mkaianzishe hiyo mipango miji yenu manzese kwa mfuga umbwa na tandale kwa mtogole na kiwalani. mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. tumbafu kabisa

    ReplyDelete
  5. Ingawa mimi siyo mwumini wa Askofu Kakobe namuunga mkono kabisa katika sula hii! TANESCO washenzi sana! Na kweli wamwogope Mungu.

    ReplyDelete
  6. Makao Makuu ya TANESCO itapigwa na radi. OHOOOO!

    ReplyDelete