Monday, April 12, 2010

Ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi Nchini Algeria:

Kutoka kulia ni watendaji wa wizara mzee Rajabu, mama Kibaya, mh: mkurugenzi wa elimu prof. Abel, mh: Katibu mkuu Alhaji Hamis Dihenga, mkurugenzi mkuu mtendaji wa bodi ya mikopo mh: Nyatega na afisa ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Walipokutana na wanafunzi University of Blida.


Imeandikwa na ndau Mdurban the King - Algiers, Algeria.


Ujumbe mzito wa wizara ya elimu na ufundi ukiongozwa na mheshimiwa katibu mkuu wa wizara hiyo mh. Alhaji, professor Hamisi Dihenga akiambatana na mkurugenzi mkuu wa elimu ya juu prof. Abel, mkurugenzi mtendaji mkuu wa bodi mh.Nyatega, maafisa watendaji wakuu wa wizara Mama Kibaya na mzee Rajabu na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa mh. Flavian Komba.

Ziara hio ya siku7, ya kutembelea na kujua matatizo na maendeleo ya kielimu ya wanafunzi wakitanzania wanaosoma Algeria. Ujumbe huo uliweza kutembelea vyuo mbalimbali na pia kukutana na wanafunzi hao.

Wanafunzi hao walionesha furaha na shukrani kwa serikali ya Tanzania kwa kuonesha kuwajali raia wake kwani Algeria inatoa scholarship kwa bara zima la Africa na baadhi ya nchi za Ulaya na Asia, lkn haikuwahi kutokea kwa serikali zao kuwatembelea wanafunzi wao. Hivyo ilitoa picha nzuri kwa Tanzania.

Pia ujumbe huo uliweza kukutana na waziri wa elimu ya juu, Sayansi na technologia, wizara ya Utalii na Mazingira. Katibu mkuu alifurahishwa na mapokezi mazuri aliyoyapata kutoka kwa serikali ya Algeria na wanafunzi hao. Serikali kwa ujumla imeridhika na ubora wa elimu ya juu inayotolewa nchini Algeria.

Katibu mkuu aliweza kuchangia chama cha wanafunzi hao (ATSA) dollar 1500 na mkurugenzi mkuu mtendaji wa bodi ya mikopo naye alitoa binafsi dollar 1000 kwa chama hicho, hapo awali chama kilipokea dollar 2000 kutoka kwa mh. Membe waziri wa mambo ya nje pindi alivyo tembelea nchi hiyo hivi karibuni.Ujumbe huo mzito umerejea nchini tarehe 10/04/2010

No comments:

Post a Comment