President Barack Obama |
Kwa ufupi;
Akizungumza na Mwananchi Jumapili Profesa Ibrahim
Lipumba ambaye ni mchumi kitaaluma, amesema kuwa ujio wa Rais Obama
unaweza kuleta neema hasa kama atakuwa ameambatana na wataalamu wa
masuala ya maendeleo.
Hii itakuwa ziara ya pili ya Rais Obama katika Bara la Afrika.
Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa ujio wa Rais
Barack Obama wa Marekani nchini, ni fursa nyingine kwa Tanzania kukuza
uchumi na kuimarisha uwekezaji.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mchumi kitaaluma, amesema kuwa ujio wa
Rais Obama unaweza kuleta neema hasa kama atakuwa ameambatana na
wataalamu wa masuala ya maendeleo.
Hii itakuwa ziara ya pili ya Rais Obama katika Bara la Afrika.
Ziara
yake ya kwanza aliifanya wakati wa awamu yake ya kwanza madarakani,
wakati ziara ya safari hii ni kipindi chake cha lala salama.
Rais
Obama alianza rasmi awamu yake ya kwanza kama Rais wa Taifa kubwa,
Januari 20, 2009, wakati ng’we yake ya mwisho ilianza Januari 21, 2013.
Rais
Obama anatarajiwa kufanya ziara hiyo mwishoni mwa Juni mwaka huu,
ambapo Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi za mwanzo za Afrika Mashariki
kutembelewa na kiongozi huyo.
Ziara ya Rais Obama inafanyika baada
ya ziara ya Rais Xi Jiping wa China aliyeitembelea Tanzania Machi 28,
mwaka huu, ambapo Tanzania ilikuwa nchi yake ya kwanza kuitembelea kwa
Afrika tangu achaguliwe kuwa rais, Machi 14, 2013.
Akizungumzia
ziara hiyo tarajiwa, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (Cuf),
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mchumi, alisema amani, utulivu na
uimara wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi kwa kulinganisha na nchi
nyingine za jirani, vimechangia kuwapo kwa ziara hiyo.
Profesa
Lipumba alisema pia ugunduzi wa rasilimali za asili kama vile gesi,
mafuta na madini ya urani ni sababu nyingine iliyomfanya Rais huyo kuja
nchini.
Hivyo aliwashauri viongozi wa Serikali kujipanga kwa ajili ya kufungua mlango huo mwingine wa uchumi na uwekezaji.
Alisema
pamoja na hali hiyo pia kuna mambo ambayo yanaweza kuchafua taswira ya
nchi kama vile ubovu wa miundombinu ya barabara, msongamano wa magari
barabarani na msongamano wa meli bandarini wakati zikisubiri kushusha
mizigo.
Jumatano ya wiki hii, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,
John Kerry alitangaza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ushirikiano kati ya
Marekani na Afrika, kwamba Rais Obama hivi karibuni atafanya ziara
Afrika.
Ingawa Kerry hakutoa maelezo zaidi ya nchi gani za Afrika
ambazo Rais Obama atazitembelea, lakini baadhi ya vyombo vya habari vya
Nigeria vilieleza kiongozi huyo atafanya ziara Tanzania, Rwanda na
Nigeria.
Kiongozi wa kwanza wa Afrika kukutana na Rais Obama tangu
awe Rais wa Marekani, alikuwa Rais Jakaya Kikwete aliyekutana naye Mei
2009, Washington, Marekani.
Kwa nini ni Tanzania na Rwanda
“Kenya
asingeweza kwenda kutokana na suala la Rais na Makamu wake kutuhumiwa
kuhusika katika mauaji ya kimbari yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu
2007/2008, kwani msimamo wa Marekani ni kutaka wahusika wa vitendo vile
wakamatwe na kufikishwa mahakamani. Hivyo kwake kuwatembelea watuhumiwa
asingeeleweka,” alisema Profesa Lipumba.
Alibainisha kuwa Rwanda
ina uhusiano wa karibu na Marekani na pengine suala la mgogoro wa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) litachukua nafasi.
Kulingana
na taarifa za Ikulu ya Marekani, Rais Obama alikuwa amepanga muda wake
mwingi wa awamu ya pili ya uongozi wake kujihusisha na masuala ya
Afrika.
Katika mstari wa kwanza, makala inasema Rais Obama ataidhuru Tanzania. Hii inamaanisha atailetea madhara. Neno sahihi lingekuwa ataizuru.
ReplyDelete