MBUNGE ISHUNGISA AFARIKI NA MJUKUU WAKE
Na Happiness Katabazi
ALIYEKUWA
Mbunge wa Pili , wa Jimbo la Karagwe ambaye alifariki Jana jioni,
Laurent Ishungisa , mjukuu wake ambaye ni Mfanyakazi wa Kampuni ya Simu
ya TIGO, Gody Tibyampasha naye amefariki alfajiri ya kuamkia Leo
Katika eneo la Skansaka karibu na Mitambo ya IPTL Wilaya ya Kinondoni
kwa ajali ya Gari.
Kwa mujibu wa Msemaji wa msiba wa Inshungisa,
Medard Birusya alisema Gody alikutwa na umauti huo wakati akiendesha
gari lake wakati akitokea kwenye msiba wa Babu yake Mabibo Hosteli
kurudi nyumbani wake Tegeta kupumzika.Miili ya marehemu wote imeifadhiwa
Katika Hospitali ya Mwananyamala.
Birusya akitangaza Ratiba ya
misiba hiyo miwili jinsi watakavyoiendesha hivi punde nyumbani kwa Mtoto
wa marehemu Ishungisa, Grace Byampanju eneo la Mabibo Hosteli, alisema
msiba wa mbunge Ishungisa uliokuwa ukifanyika Mabibo Hosteli kuanzia
Kesho asubuhi utaamishiwa nyumbani kwa wazazi wa marehemu Gody eneo la
Tegeta kwasababu Mama Mzazi wa Gody ni Mtoto pia wa marehemu
Ishungisa.Baba wa Gody ni Daktari Mstaafu Dk. Dominic Tibyampasha.
Birusya
alisema , Jumatatu miili ya marehemu ambao ni Babu na Mjukuu wake
itaagwa Tegeta na Kisha itasafirishwa kupelekwa Wilayani Karagwe kwa
ajili ya kuzikwa.
Birusya alisema Mbunge Ishungisa atazikwa
Disemba 24 Mwaka huu ,Katika Kijiji Cha Nyakaiga na mjukuu wake marehemu
Gody ambaye ameacha Mke na Mtoto wa Miezi mitatu atazikwa Disemba 25
Mwaka huu Katika Kijiji Cha Kiruruma. Ni masikitiko makubwa.Mungu
tunaomba utupe moyo wa subira na uvumilivu maana huyu Israel Mtoa roho
za watu anafanyakazi yake bila huruma.
Ishungisa alifariki
Disemba 19 mwaka huu, nyumbani kwa mwanae Grace, Mabibo Hosteli baada ya
kuugua kwa muda mrefu.Miili ya marehemu wote imeifadhiwa Katika
Hospitali ya Mwananyamala Dar Es Salaam.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Disemba 20 Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment