PICHA ZA HABARI : UZINDUZI WA WASATU NORTHAMPTON , UINGEREZA
Na Freddy Macha
Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilizunduliwa kwa vigelegele
na muziki mjini Northampton , katikati ya Uingereza jumamosi iliyopita. Tafrija
hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na wenzao
wa Kenya, Uganda, Kongo , Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na Mheshimiwa
Balozi Dk Asha Rose Migiro.
WASATU ilibuniwa mwaka jana kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na
mcheza sarakasi Fab Moses na promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema
Kitilya.
Asilimia 20 ya kipato cha onesho zilitolewa na WASATU kwa walio Northampton; kwa maafa ya
mafuriko ya maji karibuni Tanzania.
Pichani: Watanzania na wasanii wenzao wakijimwaga ukumbi wa The Eastern District Social
Club, Northampton
Furaha na shangwe ya WASATU
Balozi Migiro (katikati) na mwana
WASATU- mcheza ngoma asilia, Khadija Ismail. Wa kwanza ni Mtanzania, Salma
Kashinde
Muziki motomoto,
Northampton
Bango la shughuli
Balozi Migiro akihutubia tafrija
Mpiga sasafoni mkongwe na
mwanaWASATU- RamaSax- mzawa wa Tanga akipuliza vituz
WASATU. Toka kushoto
nyuma, Rama Sax, Saidi Kanda, John Londo, Fab Moses , Freddy Macha
Mbele : Khadija Ismail na Neema Kitilya. Picha na Shah
Vitumbua vya Neema Kitilya
Nyama Choma
Mwana WASATU Fab
Moses akionesha vituko vyake vya Sarakasi
Mwanamuziki wa Kikongo aliyehamia Tanzania miaka mingi, Kawele
Mutimanwa na bendi ya “Afrika Jambo” jukwaani Northampton
Mwanamuziki mlemavu na msanifu picha, Kea , toka Kenya
aliyetengeneza tangazo la WASATU
Mwanamuziki wa Kikongo Mboka Lia ( anayejulikana kwa jina “Burkina Faso”)
ndani ya nyuzi na sakata sakata la WASATU
Mwanamuziki mlemavu aliyekomaa- mtunzi, mwimbaji
na mpiga gitaa hatari, John Londo – mwana WASATU aliyebobea. Kileleni
Northampton bila kukosa.
No comments:
Post a Comment