Wadau, wiki iliyopita tulimpata Miss Universe Tanzania mpya. Naye ni Bi Amanda Sululu. Anarithi Bi Flaviana Matata ambaye alifika katika Top Ten katika mashindano ya Miss Universe mwaka jana.
Tunamtakia Bi Amanda mema akienda kutuwakilisha katika mashindano ya Miss Universe mwaka huu.