Showing posts with label Miss Universe. Show all posts
Showing posts with label Miss Universe. Show all posts

Thursday, December 20, 2012

Miss Tanzania Vazi la Taifa Katika Mashindano ya Miss Universe 2012


Wadau, hebu cheki hii Vazi la Taifa aliyovaa Miss Tanzania 2012, Winifrida Dominic, katika Mashindano ya Miss Universe. Samahani lakini sioni UTanzania! 
Miss Tanzania Winfrida Dominic performs onstage at the 2012 Miss Universe National Costume Show at PH Live in Las Vegas, Nevada December 14, 2012. The 89 Miss Universe Contestants will compete for the Diamond Nexus Crown on December 19, 2012. REUTERS/Darren Decker/Miss Universe Organization/Handout



Miss Bostwana 2012
Miss Ethiopia 2012


Saturday, May 28, 2011

Flaviana Matata - Miss Universe Tanzania 2007



Wadau nampenda mrembo wetu Flaviana Matata aliyeshiriki katika Miss Universe mwaka 2007. Alifanikiwa kuingia katika Top 10! Yeye hakuona haya kuwa na kipara, kuvaa nguo zenye 'African accent' na kuongea kiswahili! Sasa hao wanaokuja nyuma yake wanazidi mno kuiga uzungu. Hakuna ubaya kuomba mtafsiri, mbona wazungu, walatino wanawatumia. Ambao watafika mbali katika mashindano kama Miss Universe/Miss World ni wale ambao wanaonyesha mapenzi kwa nchi yao na siyo kutaka kuwa carbon copy ya mzungu.

Wednesday, October 22, 2008

Mambo si ndo Hayo - Flaviana Matata


Mnamkumbuka mrembo wetu, Flaviana Matata aliyefanikiwa kufika katika Top Ten wa mashindano ya Miss Universe mwaka 2007? Watu walimpenda na kusifia kipara chake. Sasa yuko South Afrika akiendelea na shughuli zake za modelling. Hivi karibuni ametoka katika matangazo (print ad) kwenye gaztei la True Love.

Flaviana, endelea na moyo wa kutaka kujiendeleza katika fani ya modelling. Na usiache huo mtindo wako wa 'natural'. Mungu akubariki!

*************************************************************

Picha na maelezo ya chini kutoka Michuzi Blog:

Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata ambaye hivi sasa yuko nchini Afrika ya Kusini ameendelea kupanda chati baada ya kunyakua tangazo katika jarida la True Love.
Flaviana ambaye anaonekana amevaa mavazi mawili tofauti ukurasa wa 73, ameweza kupata mkataba huu.

Akieleza mkataba huu wa kutangaza nguo Flaviana alieleza," Huu ni mkataba mmoja tu, na hivi punde narajia tangazo langu la televisheni pia lianze kuonekana hapa South Africa na bara la Afrika".

Flaviana hakuwa tayari kuzungumzia mkataba wake mwingine hadi itakapoonekana lakini alieleza wazi kuwa hivi sasa anaendelea kupata mialiko mingi ya kazi (casting).

Flaviana Matata aliwakilisha nchi yetu kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Miss Universe nchini Mexico ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya 6. Hivi sasa yuko nchini Afrika Kusini akifanya kazi ya uanamitindo.

Sunday, August 17, 2008

Hongera Flaviana Matata!

Kutoka Jiachie Blog

Pichani ni Miss Universe Tanzania 2007 Flavian Matata akiwa nchini South Afrika ambapo ameuchinja kwa kusaini mkataba wa mwaka Mmoja na Kampuni ya kubwa ya mitindo ya Ice Model Agency,pamoja na mambo mengine Flavian Matata anatarajia kutua mapema mwezi huu nchini Tokyo Japan chini ya mwaliko wa kampuni ya Wilna International Limited ya Japan ambapo atajaribu zali na kampuni kubwa ya mambo ya Ulimbwende nchini humo ya Jones.Blog ya JIACHIE inamtakia kila la kheri mlimbwende huyu katika kuifanikisha ndoto yake zaidi katika masuala ya Modeling.
*****************************************************************
Na mimi nampongeza Flaviana kwa kupata mkataba na moyo wake wa kuendelea na modelling. Naomba afike mbali katika fani huo. Flaviana ni wa pekee, na tusisahau alivyofika mbali katika mashindano ya Miss Universe. Bado wanazungumzia kipara chake. Flaviana ni mfano wa kuigwa.

Wednesday, June 04, 2008

Miss Unvierse Tanzania 2008 - Amanda Sululu

Wadau, wiki iliyopita tulimpata Miss Universe Tanzania mpya. Naye ni Bi Amanda Sululu. Anarithi Bi Flaviana Matata ambaye alifika katika Top Ten katika mashindano ya Miss Universe mwaka jana. Tunamtakia Bi Amanda mema akienda kutuwakilisha katika mashindano ya Miss Universe mwaka huu.



Tuesday, February 12, 2008

Flaviana Matata


Picha Asante Michuzi Blog

Miss Universe Tanzania, 2007, Flaviana Matata (20), alienda Budapest, Hungary hivi karibuni kwenye sherehe ya Budapest Opera Ball. Ni sherehe inayofanyika kila mwaka na ni tafrija yenye hadhi kubwa nchini Hungary. Wanasiasa, wakuu wa nchi, mabalozi na watu mashuhuri kutoka nchi hiyo na jirani barani Ulaya huhudhuria. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mrembo kutoka Afrika kuhudhuria hafla hiyo.

Sasa kuhusu ombi la Michuzi kwa msaada kwa Flaviana kuendelea na Modelling. Namshauri apeleke habari zake, Trump Model Management. Sasa hivi wanae MSudani Artong Arjok.

Hiyo kazi ya modelling ni know-who na namshauri pia afanye networking kali akiwa safarini. Hao warembo wenzake wanaweza kumsaidia pia.

Namshauri pia ajifunze lugha mbalimbali pia kama Kifaransa, Kispanish, Kijereumani. Sijui ana kipaji gani cha Kiingereza, maana kwenye Miss Universe waliweka Sub-titles alivyokuwa anaongea.
***********************************************************************************
OMBI LA KAKA MICHUZI
Mrembo wetu hivi majuzi alialikwa hungary kuhudhuria hafla maalumu ambapo warembo wa dunia nzima walialikwa kushiriki. hizi ni baadhi ya picha za safari hiyo inayoonesha kwamba bado flaviana anatambulika kama mmoja wa warembo bomba duniani baada ya kushika nafasi za juu miss universe mwaka jana. tatizo hadi leo anasota waya bongo wakati wenzie wote wamepata nafasi za kufanya kazi na kampuni kubwa za mitindo. mdau mwenye uwezo ajitokeze amsaidie kuendeleza kipaji chake. unaweza kuwasiliana nami kupitia issamichuzi@gmail.com nitafikisha ujumbe. hima wadau na tumsaidie mrembo wetu huyu aliyelera sifa kwa nchi hii. asije akaishia hapo alipo kwani umri wake bado wa miaka 20 unadai kabisa kufanya maajabu zaidi kwenye ulimbwende.

Saturday, February 09, 2008

Marudio - Tupende Urembo Asili




Baada ya kuandika kuhusu matako makubwa, na kusoma feedback yenu, nimeona niongee kuhusu mashindano ya urembo. Asante kaka Ndesanjo kwa kunichokoza!

Hivi karibuni Miss Tanzania 2005, Bi Nancy Sumary alienda kwenye mashindano ya Miss World na kafanikiwa kutwaa taji la Miss Africa. Kwa kweli lazima nimpongeze maana toka mashindano ya Miss Tanzania ifufuliwe miaka ya 90, hakuna Mtanzania aliyefanikiwa kuingia katika raundi za fainali na hata kutwaa taji lolote.

Kwa kweli Tanzania imepata sifa kubwa katika dunia ya mashindano ya U-Miss. Pia Tanzania imepata sifa kuwa ina wanawake wazuri, lakini nauliza ni uzuri wa aina gani? Maana sioni kama ni uzuri unayafuata maadili ya kiafrika bali ni uzuri wa kizungu!Nikitazama picha na kanda za video za Miss Ilala, Miss Kinondoni, Miss Utalii, na mashindano mbalimbali za u-Miss huko Tanzania nashangaa nachoona. Kwa kweli naona wasichana weusi wakijaribu kuiga wazungu!

Wengine wanapaka make-ups usoni ambazo zimetengezwa kwa ajili ya wazungu wakati make-up za weusi zipo. Yaani ni vichekesho mpaka wengine wanaonekana vituko. Najua hapo niatambiwa nawaonea wivu lakini si kweli na naomba mnisikilize kabla ya kunipa hukumu.

Kwanza tutazame hao wanaopelekwa na nchi zao katika mashindano hayo. Ukiangalia walio kwenye Miss World na Miss Universe, washindi wote wana hulka (characteristics) za kizungu. Tutazame waafrika wanaoenda, cheki nywele zao, zinafanana na wazungu, yaani zimenyoka kabisa. Na kama tunavyojua, sisi wenye asili ya Afrika nywele zetu ni za kipilipili. Hawa wanaweka dawa au weave! Wanaficha nywele zao za asili, sijui wanazionea haya.

Je, wanaona haya kusuka nywele zao au kuonyesha mtindo wa nywele enye asili ya Afrika?Haya, tutazame shepu zao, wote ni wembamba, hakuna mnene, hata hips za maana hawana. Na kama ana matako ni kiasi, sio ile boxi, wowowo, yokohama inayopendwa Africa. Yaani wanafanya mazeoezi eti kusudi wapunguze matako yao.

Na hao weusi kutoka Marekani na Ulaya wanafanya liposuction na surgery kupunguza matako yao asili, eti iwe ya kizungu fleti. Huko Afrika tunasema mtu mwembamba ana shida, hana raha, mgonjwa, lakini mzungu anasema ni uzuri. Na sisi tunaiga! Basi unakuta akina dada hata Tanzania, “Oh nafanya diet!” Kheh! Kisa anataka kufanana na mtu amliyemwona kwenye gazeti.

Hawajui kuwa hizo picha zinafanyiwa editing na air brushing. Kwa hiyo dada zetu wanashinda njaa kusudi wawe wembamba! Hawajui kuwa hao wanaofanikiwa kwenda kwenye u-Miss, wanajitapisha, na kujinyima chakula kusudi wasinenepe, na ukweli hawana raha.

Haya tuangalie wanavyotembea na kuongea…wanaongea na kutembea kizungu! Jamani na hata macho hawasahau, maana wanatia contact lenses zenye rangi ya bluu na kijani kusudi wawe na macho ya kizungu! Doh! Matokeo ni kuwa hao siyo watu tena bali na madoli.

Na kuhusu rangi ya ngozi, ni lazima niulize, je, umewahi kuona mshindi mweusi tii? Hao weusi wanaofanikiwa wengi ni weupe. Basi hao dada zetu wanajichibua na madawa ya ajabu. Ubaya ni kuwa usoni wanaonekana weupe lakini miili yao bado rangi yao ya asili. Mwisho wanakuwa na rangi mbili. Halafu wengine baadaye wanajikuta wana kansa ya ngozi shauri ya dawa hizo za kujichibua.Ubaya ni kuwa kama nchi ya kiafrika inataka kushinda mashindano kama Miss World, Miss Universe ni lazima mtu wao awe Mdoli wa kizungu.

Mfano, miaka mingi Nigeria walikuwa wanapeleka mrembo wao ambaye alikuwa mrembo Nigeria lakini mbaya kwa wazungu. Mwaka 2001, waliamua kumpeleka Mdoli wa kizungu, yaani dada fulani, mwembamba, futi sita na kashinda. Na tazama kesi ya aliyeshinda Miss Universe 1996, Miss Venezuela, Bi Alicia Machado…baada ya kashinda, alinenepa kweli! Yaani aliongezeka kama kilo 20! Basi majaji wakasema watamvua taji lake kama hatapungua! Dada wa watu alilia na kusema kachoka kashinda njaa!

Na tuanganlie hatima ya hao wanaoabudu hiyo standard ya kizungu na kuwa wembamba. Wanapambana na magonjwa kama Osteoperosis, yaani ugonjwa wa mifupa kuvunjika kwa urahisi, utapialmlo, na magonjwa wa akili. Ndiyo, mtu ambaye kila saa anawaza kujikondesha na kuwa hatapendwa kama si mwembamba ana ugonjwa wa akili.

Je, madaktari huko Tanzania wako tayari kutibu hayo magonjwa wa kisasa?Mashindano ya U-Miss yataendelea kuwepo, na dada zetu wataendelea kutaka kushindana na kufanana na madoli wa kizungu. Bahati mbaya ndo dunia ya leo. Lakini napendekeza tuwe na mashindano ya Miss Bantu, Miss Tanzania asili pia. Mashindano hayo yawe na nia ya kusifia uzuri asili wa mwanamke wa kiafrika. Tusisahau tulikotoka. Na hao wazungu wakiona tunajipenda basi wao wataanza kuheshimu maadili zetu.

UPDATE - Flaviana Matata aliwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya Miss Universe 2007 na kufika kwenye Top 10. Bado wanamzunguzia.

Saturday, June 02, 2007

Designer Mustafa Hassanali ajibu hoja za Michuzi blog


Wapendwa wasomaji, kule kwa Michuzi, watu walikuwa wanaongelea sana juu ya nguo alizovaa Flaviana Matata, kwenye mashindao ya Miss Universe. Hasa designer Mustafa Hassanali alitajwa sana.


Sasa kampuni yake imefanya Public Relations na kujibu hoja waliozotoa wasomaji kule. Kweli blogu ya Michuzi imekuwa nzito kuliko site yoyote ya waTanzania.

Photo (Designer Mustafa Hassanali poses with model and Former Miss Tanzania, Nancy Sumary pic from Michuzi Blog)
***********************************************************************************

PRESS RELEASE Dated 1 June 2007
FLAVIANA'S WARDROBE SAGA


First and foremost, we at Mustafa Hassanali Couture would like to congratulate Ms Flaviana Matata for performing well at the Miss Universe Pageant which is attributed to the young girl’s zeal, zest and support from her organisers, sponsors and the people who voted for her. Flaviana prior to being a Miss Universe Tanzania 2007 had an opportunity to be cast to showcase our “Namaste” Collection in January 2007.

Pictures of that Show were published in Issa Michuzi Blog amongst many others. Since May 28 2007, the finals of the Miss Universe pageant, The Issa Michuzi Blog has been flooded with comments, remarks, feedbacks and allegation in regards to the Her Wardrobe, this has been intensified more so, since her arrival back from Mexico.

Mustafa Hassanali would like to clarify, refute and abstain from the following remarks:“bora wangempa deal hassanali ila waliogopa bei si unajua these stingy idiots hu just think of themselves....”
we Appreciate that, the Anonymous, thought of us…. But we would want to make clear, we design, create, construct and embellish as per the clients budget. All good and quality product does come with a price tag. “The biggest hindrance to creativity is budgets” Mustafa Hassanali“

Hivi kaka Michu,gauni lile"jeupe"ambalo hasa ndilo lilitukosesha sisi watz ushindi kwa"mwanamke wetu Flaviana"lilitengenezwa na"designer"wa kitz Hassanali au?? Kama Hassanali ndiye alilitengeneza gauni lile"baya"adhabu yake ni kupigwa bakora hadharani,manake halikutoa kabisa dada yetulets me know kaka Michu,nani hasa alitupokonya ubingwa huu kwa kutumia hila ya kumpa auni baya"jeupe "dada yetu?”

We hereby attest that Ms Flaviana Matata On stage evening gown, Official National Costume, Bikini, Pre-final rehearsal segment gown and her welcome home gown were NOT A MUSTAFA HASSANALI CREATION. Each designer has its own creative IQ which makes that their selling point. We respect it.

As they say “one mans meat is another mans poison” Kwa Kiswahili “Mkia was Nguruwe………….”“michuzi hakuna uzalendo wa kijinga tena la sivyo tutaacha kufagilia, wabunifu wa kibongo hawajafikia viwango kwa hiyo hakuna kuvaa nguo zao kwenye mashindano ya kimataifa la sivyo itakuwa aibu tu, vaeni nguo zao hukohuko bongo mkishatoka mnavaa nguo zenye mvuto zilizo kwenye international standardkwa lile gauni hata kumi bora wamempa sababu alikuwa unique and creative on her own beauty”

we @ Mustafa Hassanali would like to inform the person who wrote this comment, That fashion designers just like other professionals have their Identity. I would like to enlighten the said person that its passion for our work, just like the rest of you, drives us for our daily livelihood. As they Say Charity Begins at Home, Ailinda Sawe of Afrika Sana is a Professional Designer and one of the first in Tanzania with a Degree.

Ally Rhemtullah is another qualified designer from USA whilst Elly Mlaki studied in UK. The Late Kiiza Kahama studied in Paris. We Have So many professional DESIGNERS in Tanzania some who are trained and others are Qualified by Experience.

“Hivi ni nani aliye-design Night Gown yake?? Lile Gown lilikuwa baya kusema ukweli. Jamani Tanzania Designers wengi wabovu sana yaani hata tungemnunulia nguo kutoka Walmart angependeza sana kuliko lile gown baya. Angekuwa na Gown bomba angeweza kushinda. Lakini hata hivyo hongera sana Flaviana Matata.”

As stated Earlier that it was NOT A MUSTAFA HASSANALI.What Ms Flaviana Matata Wore during the pageant, had nothing to do with the Qualification status of designers in “Bongo” but its entire her own judgement, she is above 18yrs old, and that of her Organisation Miss Tanzania Universe.Mustafa Hassanali did design two over the Top Evening Gowns for Miss Flaviana Matata as her personal wardrobe which was commissioned and paid for by Flaviana personally.

ABOUT MUSTAFA HASSANALI COUTURE

Mustafa Hassanali Couture is renowned for its elegance, style, flamboyancy, glamour and glitz that has made it one of the most sought after fashion house in TanzaniaHaving been showcased throughout South, Central, Eastern Africa and Italy, this has influenced his cosmopolitan approach to the world of Fashion in Tanzania. It is his exquisite handwork, detailed beadwork and creative ensemble embellishments that make its designs alive. Whether it’s the corporate wear, Traditional costumes or a Wedding Ensemble… Mustafa Hassanali handles each piece with great care and gives the utmost attention to whole outfit right from first client contact to delivery, a personal touch all through.

True to its policy, each design and Outfit is a masterpiece of work…. A duplicate is NEVER created.That is what makes it unique, a Truly Mustafa Hassanali Affair.
Issued By:press@mustafahassanali.netTel: +255-71-5303880
P.O.BOX 10684 DAR ES SALAAMTANZANIATel: +255-78-4303880+255-22-2668555E-mail: press@mustafahassanali.netURL: http://www.mustafahassanali.net

Monday, May 28, 2007

Flaviana afika Top Ten - Miss Japan ashinda!






Kwanza nampongeza Miss Tanzania, Flaviana, Matata kwa kufika katika Top Ten (kumi bora) ya mashindano ya Miss Universe. Ingawa hakufika katika Top 5 atafika mbali maana mabilioni ya watu wamemwona. Pole zake Miss USA, alianguka jukwaani kwenye evening gown segment.

Nilijua Miss Japan atashinda. Alivyopita na swimsuit yake alivyokuwa anatingisha matako, kwa swing, macho yote yalikuwa kwake. Flaviana alivyovaa ili bikini niliona kama ana aibu fulani, bora angetembea kama anacheza ngoma watu wangemshangilia. Flaviana alijitahidi sana lakini kuna wakati niliona kama alikuwa nervous hasa pale kwenye Evening gown, na hata mwanzo walivyokuwa 77 na alikuwa jukwaani.

Lakini kunyoa kipara kilimsaidia kwa kiasi fulani, ila ingekuwa vigumu ashinde awe Miss universe maana moja wa wadhamini wakuu ni kampuni inayotengeneza manukato ya nywele. Miss Jamaica naye alishindana na nywele za rasta.

Lakini leo jioni waTanzania tuliweza kujivunia si mchezo, maana ni mara ya kwanza kuona Miss Tanzani anafika mbali kiasi hicho katika hayo mashindano. Naomba Flaviana akirudi Tanzania afundishe na atoe ushauri kwa wasichana wengine kuhusu jinsi ya kushiriki katika hayo mashindao na kushinda.

Natumaini Trump Model Agency watampa contract.

Good Luck Flaviana! -

(Miss Tanzania Flaviana Matata akipiga pozi na Miss Italy na Miss Nigeria. Photo from Michuzi Blog)

Msisahau kutazama mashindano ya Miss Universe leo jioni. Flaviana anasifiwa kweli, hasa kwa vile amenyoa kipara na anajiita 'natural African woman'.

Kwa habari na picha zaidi nenda:

http://tv.yahoo.com/miss-universe-2007/show/41744/photos/1

http://www.elpasotimes.com/entertainment/ci_6006480

Saturday, May 12, 2007

Miss Universe 2007 - Je, atakuwa Flaviana Matata wa Tanzania?




Kwa kweli mwaka huu nangojea kwa hamu siku ya May 28th. Siku hiyo NBC itonyesha Live mashindano ya Miss Universe itakayofanyika huko Mexico City.

Mwakilishi wa Tanzania, Flaviana Matata yumo. Kwa kweli weusi kutoka nchi zingine wana weave na wigi kichwani, lakini yeye kanyoa upara! Kama vile kusema, napenda uafrika wangu! Naomba afike mbali katika hayo mashindano.

Na hata kama hata pita msishangae mkisikia kuwa amepata modelling contract, au yuko kwenye matangazo ya magazeti na TV. Sasa hivi hao models weusi wa kiafrika ni mali kweli hapa. Washukuru akini Alek Wek, na Iman kwa kupendwa waafrika katika u-model hapa USA. Zamani ilikuwa model mweusi lazima awe mweupe karibia ya mzungu na awe na nywele ndefu!

Black Beauty juu! Waafrika tujipende!